Mizania ya haki; Kile alichopaswa kufanya Makamba jr

Niweke neno......
Jana tayari waliibuka watetezi wake na kudai zile sauti ni za Mnigeria na ni za kutengeneza tu na kwamba Mange ni mzushi tu, wengi walianza kuamini hivyo na kuona ni issue za kupika tu na hazina ukweli wowote.

Kuibuka kwa January na kuanza kukiri kwamba huyo mtu anamjua na wameshaonana na ni shemeji yake, ila kupinga mengine kwa sauti ya wasi wasi (hapa ikaonyesha wazi yaliyomo yamo).

Utata
Dada mtu anasema yule Mzungu ni tapeli tu......kaka mtu anasema jamaa anamdai dada
Yote kwa yote subra ilihitajika na wakakaa chini kwanza japo wakasoma alama za nyakati na kuja na kauli moja kwani mtu mzima ukivuliwa nguo huchutama.
 
9238e9bbe945e16083d6298943955f24.jpg
Nimemtaja yeye kama mhusika mkuu kutokana na nyazifa zake kisiasa, nafasi yake katika jamii na historia yake kwenye uwanja wa siasa na maamuzi mengi yaliyotokana na yeye...kwenye hii skendo iliyoko kwenye hatua za tuhuma yeye ndio muathirika mkuu...kwahiyo busara uvumilivu mkubwa akili iliyo sharp na werevu vilihitajika sana kipindi hiki
Hii ni vita yenye pande nyingi na wapambe wengi...mbinu bora zinahitajika ili kuweza kushinda vita
Vyovyote vile iwavyo kuna kufahamiana kwa karibu kati ya watatu hawa January Mwamvita na muitaliano na kwa vyovyote kulikuwa na makubaliano fulani fulani yaliyohusisha pesa nyingi (za rushwa?)ahadi za upendeleo kwenye mambo fulani nk nk
Kwa kulifahamu hili na zile tambo za bibie Kimange...kwamba ana lundo la ushahidi wa kila aina, Makamba hakupaswa kujibu lolote kwasasa...angekaa kimya akinote kila kitu yakiwemo malumbano ya mitandaoni, angesubiri walau kwa siku kadhaa aone kimange anajua kiasi gani
Kuwalipa haraka haraka vijana wa mtandaoni wakanushe kijinga kabisa na yeye kukimbilia kukanusha kumempa kimange credit moja kubwa sana
Kimange anajulikana alivyo mchokonozi na mdaku, hivyo mpaka jana jioni watu walikuwa hawamuamini kivile na hakukuwa na post nyingi...lakini baada tu ya watuhumiwa kuongea na kukiri baadhi ya mambo mjadala ukageuka mwelekeo na post zikaongezeka maradufu....!
Makamba kama kiongozi aliyekuwa msaidizi wa rais (nafasi kubwa sana hii) alipaswa kuwa na subra katika hili ili mihemko kwenye mitandao ipoe apate pa kuanzia
Bahati mbaya sana the guilty are afraid hiyo ni kanuni ya maisha...alipaniki kwa kuguswa pabaya bila maandalizi
Wakati ushahidi na ukweli ndio vitaleta mizania ya haki...lakini mpaka tutakapofika huko Makamba atakuwa sio huyu tena....!
e7f4f4799bac872b7325d9ed1eb562cc.jpg
WELL SAID BRO
 
Hii kitu kabla ya kukimbilia kwenye mitandao na kukanusha kizembe angewatafuta wanasheria na watu wengine wenye uelewa na uzoefu zaidi kumzidi wakae chini watafakari kwa pamoja....awe mkweli kwao wafuatilie mjadala kimya kimya kisha wajipange... lakini J akaona hili analimudu...!hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kudhani unajua kuliko wengine
Nilikuwa na mtazamo Kama wako haswa kwenye suala la kutoa ufafanuzi Mwepesi katika shutuma nzito. Katika moja ya mbinu za kufanya upelelezi na kuhoji watuhumiwa mara nyingi mtuhumiwa huwa anaachwa au anapewa nafasi ajieleze...na Kama hayuko makini hapo hapo kwenye maelezo yake ndio huwa yanapatikana maswali na vielelezo vya shutuma au kesi husika. Uko sahihi kabisa kwamba jamaa bora angetumia Mwanasheria au Msemaji maalum kutolea ufafanuzi shutuma hizo. Kwa sababu kwa muonekano wa kawaida ni Kama hili suala amelichukulia kirahisi kana kwamba amepewa hiyo $ 1 million ya mboga tu.
 
Hii kitu kabla ya kukimbilia kwenye mitandao na kukanusha kizembe angewatafuta wanasheria na watu wengine wenye uelewa na uzoefu zaidi kumzidi wakae chini watafakari kwa pamoja....awe mkweli kwao wafuatilie mjadala kimya kimya kisha wajipange... lakini J akaona hili analimudu...!hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kudhani unajua kuliko wengine
Hana lolote analojua "we all know elimu ya kuunga.....the form four story then form six halafu makambi ya wakimbizi kugawa vyakula na maturubai. The America story am reserving my comment till later when the truth of this thread akipindishwa. Halfu Mshana Jr utambue kuna mengi sana juu ya mshutumiwa ni watu tu hawajui na utaratibu wetu wa kupeana nyadhifa kwakua baba alikua so and so na kulindana (wengine mtatumbuliwa majipu lakini wana wa wafalme haitawagusa) kiukweli achilia mbali hizo shutuma hana hata sifa ya kuwa kwenye nafasi hizo si kielimu wala kwa utumishi wa umma uliotukuka.
 
Mzee wa msoga ndivyo alivyo huwa anamfukuza mwizi kimyakimya, sasa huyu dogo usalama wake akimbilie kwa watu ili wamsadie kwa sababu wakiendelea kufukuzana huko porini kimyakimya wakiwa peke yao itakula kwake

Hahahaaa. Sipati picha wakikutana porini wawili.
Sizonje muokoe January.
 
Niweke neno......
Jana tayari waliibuka watetezi wake na kudai zile sauti ni za Mnigeria na ni za kutengeneza tu na kwamba Mange ni mzushi tu, wengi walianza kuamini hivyo na kuona ni issue za kupika tu na hazina ukweli wowote.

Kuibuka kwa January na kuanza kukiri kwamba huyo mtu anamjua na wameshaonana na ni shemeji yake, ila kupinga mengine kwa sauti ya wasi wasi (hapa ikaonyesha wazi yaliyomo yamo).

Utata
Dada mtu anasema yule Mzungu ni tapeli tu......kaka mtu anasema jamaa anamdai dada
Yote kwa yote subra ilihitajika na wakakaa chini kwanza japo wakasoma alama za nyakati na kuja na kauli moja kwani mtu mzima ukivuliwa nguo huchutama.
Kweli mkuu, bahati mbaya sana hakuna namna ya ku tag comment ya mtu. Nimewatafuta sana.
 
Asingeweza kukaa kimya,, kuna sehemu mtoto wa kiume ukiminywa lazima upige ukelele,,

February kashikwa ile sehemu mbaya na kimange hakuwa na jinsi Lazima apige kelele za maumivu,, hii sehemu hata ukigongwa na mpira lazima ukae au ulale kifudi fudi.
 
Haya maji yameshamwagika na wakirndelea hata chombo cha kubebea maji nacho kitaharibika.
 
Hii kitu kabla ya kukimbilia kwenye mitandao na kukanusha kizembe angewatafuta wanasheria na watu wengine wenye uelewa na uzoefu zaidi kumzidi wakae chini watafakari kwa pamoja....awe mkweli kwao wafuatilie mjadala kimya kimya kisha wajipange... lakini J akaona hili analimudu...!hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kudhani unajua kuliko wengine
.there your are mshana.mimi naona kama siku hizi watu wazima wamekosa busara kama za watu wa zamani ndio maana watu kama ,makamba,kimambi nk nk nk wanaiteka mitandao kijinga tuu
 
Back
Top Bottom