Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,818
- 730,196
Hii ni vita yenye pande nyingi na wapambe wengi...mbinu bora zinahitajika ili kuweza kushinda vita
Vyovyote vile iwavyo kuna kufahamiana kwa karibu kati ya watatu hawa January Mwamvita na muitaliano na kwa vyovyote kulikuwa na makubaliano fulani fulani yaliyohusisha pesa nyingi (za rushwa?)ahadi za upendeleo kwenye mambo fulani nk nk
Kwa kulifahamu hili na zile tambo za bibie Kimange...kwamba ana lundo la ushahidi wa kila aina, Makamba hakupaswa kujibu lolote kwasasa...angekaa kimya akinote kila kitu yakiwemo malumbano ya mitandaoni, angesubiri walau kwa siku kadhaa aone kimange anajua kiasi gani
Kuwalipa haraka haraka vijana wa mtandaoni wakanushe kijinga kabisa na yeye kukimbilia kukanusha kumempa kimange credit moja kubwa sana
Kimange anajulikana alivyo mchokonozi na mdaku, hivyo mpaka jana jioni watu walikuwa hawamuamini kivile na hakukuwa na post nyingi...lakini baada tu ya watuhumiwa kuongea na kukiri baadhi ya mambo mjadala ukageuka mwelekeo na post zikaongezeka maradufu....!
Makamba kama kiongozi aliyekuwa msaidizi wa rais (nafasi kubwa sana hii) alipaswa kuwa na subra katika hili ili mihemko kwenye mitandao ipoe apate pa kuanzia
Bahati mbaya sana the guilty are afraid hiyo ni kanuni ya maisha...alipaniki kwa kuguswa pabaya bila maandalizi
Wakati ushahidi na ukweli ndio vitaleta mizania ya haki...lakini mpaka tutakapofika huko Makamba atakuwa sio huyu tena....!