Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,845
Ni wazi serikali inapata mapato kwenye hii barabara ambayo ni wazi kuwa iko bado kwenye kipindi cha uangalizi...! Yani mjengaji bado anaifanyia uangalizi kulingana na mkataba lakini hili halizuii serikali kufanya ukarabati udiotokana na mkataba wa ujenzi (naweza kukosolewa kwenye hili
Kwasasa hali si mbaya bado...uharibifu uliopo Kwasasa ni kwenye nguzo za usalama na vizuizi kwa waenda kwa miguu, alama na viashiria vingi vya barabarani, taa za kuongozea magari na taa za usiku
Tunavyoendelea kulivalia macho ya mbao hili litakuja litugharimu mamilioni ya pesa
-vizuizi vingi zaidi vitagongwa bila kubadilishwa
-Taa nyingi zitaungua bila kubadilishwa huku nyingine zikigongwa
-milango ile ya vioo inaweza kugongwa na kupasuka bila kubadilishwa
-mashimo madogo hayatazibwa na yataongezeka mpaka kuwa makubwa kabisa
Barabara itazeeka kabla ya wakati wake! Kama serikali inaona ni gharama kuisimamia hii barabara basi iikatie bima kubwa
Mradi wa mabilioni unapopewa matunzo duni inasikitisha mno