Miundombinu ya BRT: usipoziba ufa utaujenga ukuta

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,720
129cf3b783254b6f99f5cd86d8cdbdb0.jpg
niliahidi kuleta hii mada kuhusiana na hii miundombinu ya barabara ya Strabag/BRT
Ni wazi serikali inapata mapato kwenye hii barabara ambayo ni wazi kuwa iko bado kwenye kipindi cha uangalizi...! Yani mjengaji bado anaifanyia uangalizi kulingana na mkataba lakini hili halizuii serikali kufanya ukarabati udiotokana na mkataba wa ujenzi (naweza kukosolewa kwenye hili
Kwasasa hali si mbaya bado...uharibifu uliopo Kwasasa ni kwenye nguzo za usalama na vizuizi kwa waenda kwa miguu, alama na viashiria vingi vya barabarani, taa za kuongozea magari na taa za usiku
6f2b730f6fee3a1bbb22566f557b44ad.jpg
msimamizi anayeiwakilisha serikali kwenye hili ni nani? TANROADS? hawayaoni haya matatizo madogo dogo ya ukarabati?
Tunavyoendelea kulivalia macho ya mbao hili litakuja litugharimu mamilioni ya pesa
-vizuizi vingi zaidi vitagongwa bila kubadilishwa
-Taa nyingi zitaungua bila kubadilishwa huku nyingine zikigongwa
-milango ile ya vioo inaweza kugongwa na kupasuka bila kubadilishwa
-mashimo madogo hayatazibwa na yataongezeka mpaka kuwa makubwa kabisa
Barabara itazeeka kabla ya wakati wake! Kama serikali inaona ni gharama kuisimamia hii barabara basi iikatie bima kubwa
Mradi wa mabilioni unapopewa matunzo duni inasikitisha mno
 
kweli mdau,na jangwani darajani pia kumeanza kuwa na mashimo.Na mifuniko ya chemba za katikati ya barabara imeanza kudidimia chini hii ni hatari.Hasa kipande cha kisutu mpaka makutano ya mtaa wa samora.Wafanyie kazi mapema kabla maafa hayajatokea
Maeneo yenye shida ni mengi na yanazidi kuongezeka
 
129cf3b783254b6f99f5cd86d8cdbdb0.jpg
niliahidi kuleta hii mada kuhusiana na hii miundombinu ya barabara ya Strabag/BRT
Ni wazi serikali inapata mapato kwenye hii barabara ambayo ni wazi kuwa iko bado kwenye kipindi cha uangalizi...! Yani mjengaji bado anaifanyia uangalizi kulingana na mkataba lakini hili halizuii serikali kufanya ukarabati udiotokana na mkataba wa ujenzi (naweza kukosolewa kwenye hili
Kwasasa hali si mbaya bado...uharibifu uliopo Kwasasa ni kwenye nguzo za usalama na vizuizi kwa waenda kwa miguu, alama na viashiria vingi vya barabarani, taa za kuongozea magari na taa za usiku
6f2b730f6fee3a1bbb22566f557b44ad.jpg
msimamizi anayeiwakilisha serikali kwenye hili ni nani? TANROADS? hawayaoni haya matatizo madogo dogo ya ukarabati?
Tunavyoendelea kulivalia macho ya mbao hili litakuja litugharimu mamilioni ya pesa
-vizuizi vingi zaidi vitagongwa bila kubadilishwa
-Taa nyingi zitaungua bila kubadilishwa huku nyingine zikigongwa
-milango ile ya vioo inaweza kugongwa na kupasuka bila kubadilishwa
-mashimo madogo hayatazibwa na yataongezeka mpaka kuwa makubwa kabisa
Barabara itazeeka kabla ya wakati wake! Kama serikali inaona ni gharama kuisimamia hii barabara basi iikatie bima kubwa
Mradi wa mabilioni unapopewa matunzo duni inasikitisha mno

Hizi dosari ndogo ndogo ni very cheap kuzirekebisha lakini watendaji hawapendi kuzifanyia kazi kwakuwa 10% yake ni almost negligible kwahiyo watasubiri iongezeke ndipo wainuke
 
kweli ase wawe makini au wafanye ukarabati kwa sehemu zilizoharibika,kwani kaz ya wale security pia si ni kuangalia miondombinu ya vituo na sehemu walipo.mfano BRT ubungo to kimara vituo ving nguzo zake zimeharibiwa wala hazirekebishwi.
 
Hizi dosari ndogo ndogo ni very cheap kuzirekebisha lakini watendaji hawapendi kuzifanyia kazi kwakuwa 10% yake ni almost negligible kwahiyo watasubiri iongezeke ndipo wainuke
Nchi ya watu wadogo, taifa la kitu kidogo....huu mfumo hautaondoka kwa kutumbua na kubadili teuzi bali katiba pendekezwa
 
Mwaka jana tulikuwa na moja ila ni sahihi kuna uhitaji mkubwa kwenye hili
Maana, naona planning ya miundombinu ni kama ya muda mfupi,isiyozingatia ukuaji wa miji. Mfano kipande cha barababa toka ubungo mpaka mlandizi kilijengwa kwa njia mbili kuishia kimara, na kadhia iliyojitokeza wote tuliona ile misururu ya foleni. Na leo tunaona BRT imeishia kimara, wakati dsm imeshaungana na kibaha kimakaazi.

Unaona hiyo changamoto?
 
Hebu ngoja hili nalo tulitengenezee mjadala
 
mshana jr utaishia kuitwa mchochezi tu. Vituo vingi unaenda kukata ticketi au ku reongeza salio kwenye kadi unaambiwa hakifanyi kadi nenda kituo kinachofuata. Najiuliza mradi mkubwa kama huu mbona hauna usimamizi makini?

Tungeokoa pesa nyingi sana kwa kushughulikia hizi dosari ndogo ulizoziainisha hapa, lakini hakuna mtu anaehangaika nalo japo kuna mtu analipwa mshahara na marupurupu kusimamia hivyo vitu.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom