Miundombinu Tanzania bado sana

Miundombinu Tanzania bado sana

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
6,106
Reaction score
12,273
Kusema kweli Tanzania tuna safari ndefu kwenye miundombinu

Tanzania ukiachana na main roads, barabara nyingi bado ni za vumbi especially mitaani wanakokaa watu. Hata miji mikubwa kama Mwanza na Mbeya, barabara ni changamoto. Mji unaokua kwa kasi kama Kahama bado uko nyuma kwenye barabara. Dar yenyewe ina mitaa mingi ya barabara vumbi, kuna maeneo mengi hatapitiki nyakati za mvua. Ikifika kiangazi barabara zinajaa mchanga. Tuna safari ndefu sana

Reli ziko chache mno, usafiri wa treni bado uko nyuma, nadhani tuna reli nne tu na tatu ni MGR bado. Ya kati, Tazara na ya Kaskazini. Halafu treni za MGR zenyewe zimechakaa sana, zipo kama treni za 1900s
Hii SGR ni hatua nzuri, natarajia tutaongeza treni nyingine miaka ya usoni, kama tuko serious

Tanzania barabara zetu zimejaa michanga, mitaro mingi iko open matokeo yake watu wanatupia taka humo ndani. Ukijumlisha na mchanga unaoingia mitaroni, unakuta hadi mitaro inaota nyasi.
Na hapo barabara zina mashimo kibao

Drainage system nayo ni very poor. Msimu wa mvua ukifika ni mafuriko kuanzia Dar, Mwanza, Arusha, Morogoro yani Tanzania nzima

Hakuna pavements kwenye business districts nyingi, ni mchanga tu ndio maana michanga inajaa barabarani na kuziba mitaro

Neighborhood za Tanzania nyingi zina completely ZERO infrastructure. Yani unakuta tu ni ardhi na nyumba za watu basi, hakuna lami, hakuna pavements, hakuna drainage system za maana, hata zilizopo zimeachwa tu wazi, hazifunikwi, uggh

Mpaka leo miji kama Dodoma, Dar, Arusha na Mwanza haina metro railways licha ya kuwa na wakazi laki 6 hadi mamilioni 😏

Miji mingi Tanzania ni michafu. Hakuna dustbin mitaani, watu wanatupa tu taka hovyo, yani hii nchi imejaa takataka za plastiki everywhere. Mazingira machafu ndio maana kuna kipindipindu cha mara kwa mara kama cha Mbeya kilivyofyeka watu 2024/2025 kwa miezi 5 mfululizo

Neighborhood za Tanzania hazina streetlights, usiku barabara ni giza tu

Our development is slow na tuna zero commitment kwenye kuendeleza miundombinu kwenye makazi ya watu.

Kila siku unasikia uchumi unakua na bado mitaani barabara za vumbi, mitaro imejengwa tu kienyeji na ipo open, mitaa michafu, hakuna street lights....

Hapo ni mjini tu, ukiingia vijijini ndio kabisa utakata tamaa

Miundombinu Tanzania bado sana. Moja ya vitu vinafanya Watanzania kuwaza kukimbilia nchi za watu ni pamoja na miundombinu mibovu ambayo hakuna anayejali.
Especially miundombinu inayohusu makazi ya wananchi.
Achana na hiyo inayoenda kujengwa maporini huko
 
Nashukuru mitaa yangu huko ilipigwa mkeka
Kwengine walipiga zege
Serikali haijaamua hawako serious hayo mambo wakiamua wakiweka ubinafsi pembeni,inawezekana

Ova
 
Watu wasio na weledi wa kuongoza nchi wanang'ang'ania madaraka sasa unategemea nini?
 
500km² city area, 1.5 million people
Of course ni mji mkubwa
Top 10 ya mikoa mikubwa au miji mikubwa Mwanza haipo

1. Tabora
2. Morogoro
3. Rukwa
4. Mbeya
5. Lindi
6. Ruvuma
7. Kigoma
8. Singida
9. Shinyanga
10. Dodoma

Nionyeshee Mwanza hapo
 
Nimekwambia nionyeshee Mwanza kwenye hio top 10 kwani hio niliyotaja sio miji?
Mji wa Tabora sio mkubwa kuliko Mwanza
Wewe umetaja list ya mikoa mikubwa. Mkoa unahusisha miji, majiji, vijiji, vitongoji, mapori na kila kitu
Kwa mfano licha ya Dar kuwa mkoa mdogo sana ila ndio mji mkubwa zaidi East Africa. (Eneo la mjini pekee lina cover 1500km²)
Mji wa pili kwa ukubwa Tanzania ni Mwanza. Mkoa wa Mwanza una 25000km² lakini mji wa Mwanza una 500km² ambayo inakaribia Nairobi kwa ukubwa, Nairobi City ina 650km²
Kwa hiyo tofautisha kati ya mikoa na miji

Lindi ni mkoa mkubwa kuliko Dar, lakini Dar ni mji mkubwa kuliko Lindi town (size and population)
 
Back
Top Bottom