Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,855
- 110,961
Kwenye ukristo na katika Uyahudi huko agano la kalii nabii alichukuliwa kama ni mtu muonaji/seer wa mambo ya yajayo mbeleni, pia katika agano la kale na Uyahudi hakuna mtume au mitume. Katika agano jipya ndio kumekuwepo na cheo cha mtume(apostle) ambapo kinahusu wale wafuasi 12 waliokuwa wakiandamana na Yesu na ni cheo cha kawaida katika baadhi ya makanisa pia.
Tukija upande mwingine wa Uislamu naona karibia watu wote maarufu wa zamani waliopo katika Biblia na historia ya Wayahudi wanaitwa mtume au Nabii! Mfano Adamu, Mfalme Daudi, Yakabo(Israel), Ibrahimu, mfalme Suleiman, Ishmael mpaka Yesu n.k wote ni wanaitwa mitume au manabii! Ni kigezo gani katika uislamu cha mtu kuwa nabii au mtume? Kuna tofauti gani ya nabii na mtume?