Mitego ya mke wa Mchungaji nimeichoka!

Mr mgeni

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
1,222
804
Habari zenu wakuu,

Namheshimu sana mke wa mchungaji huyu ni jirani yangu tumepanga nyumba moja lakini mambo anayonifanyia hadi naona aibu, ndani ya nyumba hii ina public toilet ndani, anapenda mno kushinda na kanga moja nyumbani hata chupi ni shida kuvaa.

Siku moja tupo sebleni wawili tu tunaangalia movie mara movie ile imeisha akaweka part 2, mara kanga imeanguka Haaa! Kama alivyozaliwa aisee cha ajabu hakusema hata samahani, ndio kwanza kainama kaokota kaishikilia kwenye maziwa huku akisema movie hii ni nzuri sana Shemeji.

Bila hiyana nikajibu ndio ila nitaimalizia nikirudi kuna sehemu naenda...aka x, siku nyingine kanivamia bafuni nikiwa naoga na anajua kabisa kuna mtu bafuni, yote hayo na mengine mengi sijayasimulia.

Tunaheshimiana sana na huyu brother mchungaji kama vile familia moja. Kuhama natamani ila nimelipia pango mwaka mzima ndo kwanza na miezi 2 kwenye hii nyumba.

Nipeni ushauri ila usinishauri kuhusu kufanya nae mapenzi.
 
Mimi najiuliza unatoka wapi kuangalia movies na mke wa Mchungaji tena wakati mwenyewe hayupo???
Kwanza inavyo onekana wewe ndiye unajipeleka kwake kwani umesema hapo...ukaaga ukaenda kutembea??
Acha hizo kama unataka movies azima ukaangalilie kwako. Wanaume hawaangalii Movies/TV kwa wake za watu wakati wenyewe hawapo...shauri yako!!!
Isije kuwa wewe ndiye unampa vishawishi halafu unamlaumu mama wa watu....
Jichunguze kwanza!!!!
 
Kama wote wapangaji si kila mmoja ana chumba chake sasa TV mnakwenda angalia pamoja wapi kwake au kwako. Acha kwenda kwao baki kwako la utajikuta unakuja kuomba ushauri baada ya kuzini
mm ni mpenzi wa mpira na ninapenda kuangalia na marafiki zangu so nikaamua kununua flat screen kubwa na Dstv nikaweka seating room tukawa tunaangalia wote kama familia
 
Mimi najiuliza unatoka wapi kuangalia movies na mke wa Mchungaji tena wakati mwenyewe hayupo???
Kwanza inavyo onekana wewe ndiye unajipeleka kwake kwani umesema hapo...ukaaga ukaenda kutembea??
Acha hizo kama unataka movies azima ukaangalilie kwako. Wanaume hawaangalii Movies/TV kwa wake za watu wakati wenyewe hawapo...shauri yako!!!
Isije kuwa wewe ndiye unampa vishawishi halafu unamlaumu mama wa watu....
Jichunguze kwanza!!!!
kama huna video vumilia hadi ununue ya kwako.
 
Mimi najiuliza unatoka wapi kuangalia movies na mke wa Mchungaji tena wakati mwenyewe hayupo???
Kwanza inavyo onekana wewe ndiye unajipeleka kwake kwani umesema hapo...ukaaga ukaenda kutembea??
Acha hizo kama unataka movies azima ukaangalilie kwako. Wanaume hawaangalii Movies/TV kwa wake za watu wakati wenyewe hawapo...shauri yako!!!
Isije kuwa wewe ndiye unampa vishawishi halafu unamlaumu mama wa watu....
Jichunguze kwanza!!!!
Nyumba tunayokaa ni Nyumba kubwa ina room 3 sebule,choo na jiko mimi na room moja na mchungaji moja nyingine tukafanya kama stoo tv ya sebleni ni ya kwangu napenda
Hiyo flat screen uliiweka seating room kwako au kwa mchungaji
ipo seating room nao wanapenda kuangalia
 
Nyumba tunayokaa ni Nyumba kubwa ina room 3 sebule,choo na jiko mimi na room moja na mchungaji moja nyingine tukafanya kama stoo tv ya sebleni ni ya kwangu napenda

ipo seating room nao wanapenda kuangalia
Sipendi kupanga nyumba ya hivyo kushare no big no hayo ndio madhara. Sasa kodi mnalipaje kama vipi waambie wakulipe uwaachie nyumba ukapange kwingine
 
Yaani we jamaa post zako karibia zote unaongelea mada hizi tu. Acha ushamba. Mara mke wa boss ananitaka, mara mchepuko umekuja kidai pesa. Acha kutufanya wote maboya bwana
 
Mmmhhh! Haiwezekani mtu akufanyie mitego yote uvumilie pasi kumwambia kwamba anachokifanya hujapendezwa nacho nionavyo nawewe umeyapenda sio bure.

Laiti kwa mara ungeonyesha kutofurahishwa nayo sidhani kama angerudia. Ila ndio sifa yenu hiyoo.
 
Sasa nyumba gani hiyo umepanga mnashea sitting room na wapangaji wengine? Ushauri wangu ni kwamba kodi ikiisha utafute dalali mwenye akili akutafutie room nzuri au nyumba nzuri yakwako peke yako
 
Kwa faida tu ya wale ambao wanatamani wake za watu. Acheni hizo tabia. Unatamani kuuhalalisha ujinga huu kwa kusema kuwa mama mchungaji anakutega. Jua hili na joto hili wataka mama wa watu achubuke?? Avae atakavyo, HAKUTEGI. Anakuheshimu saana kwani anatamani avue zoote abaki wazi ila anakuheshimu.
Pili. Kumbuka kwamba, ukimpanda tu, labda ufe bila kuoa. Ukioa tu, na wewe wako watampanda tuuu.
 
Njoo tubadilishane nyumba ya kupanga... Wewe uhamie hapa ninapokaa na mie nihamie hapo unapokaa...
nataka Nyumba yenye sifa hizi,iwe barabarani,maji yawepo,Ac,geti iwe maeneo ya Mbezi beach kama inavigezo hivyo ni pm tubadilishane
 
Back
Top Bottom