Mke wa baba mchungaji kapata watoto watatu nje ya ndoa. Baba mchungaji amekwazika anaomba waumini tumpe ushauri

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,976
Mkasa wa wanandoa.

MKE WANGU HAJUI, KWAMBA MIMI NAJUA.

Nimekuwa kwenye ndoa kwa miaka 14, na tuna watoto 3, wote wanaume, lakini hakuna ata mmoja ambaye ni damu yangu. Najua ili kwa uhakika kabisa, lakini mke wangu hajui kwamba Mimi najua.
NGOJA NIWASIMULIE.

Miaka 5 kabla yakukutana na mke wangu, nilipatwa na ajali ya gari nikiwa pamoja na rafiki zangu wawili. Gari yetu iliaribika vibaya sana, nilipona peke yangu katika iyo ajali, nilitumia miezi 11 katika hospital moja hapa Dar, na mwisho kabisa niliambiwa siwezi kupata Mtoto tena katika maisha yangu.

Niliamua kumpa YESU maisha yangu (kuokoka) na nikatubu dhambi zangu huku nkimshukuru MUNGU kwa kuniokoa na ile ajali ambayo imewachukua rafiki zangu wawili.

Baada muda nikawa mchungaji katika kanisa dogo la mtaani kwangu,miaka 5 baadaye ndio nikakutana na mke wangu tukiwa katika moja ya mikutano ya injili. Sikumweleza juu ya hali yangu, kwasababu nilikuwa na matumaini kwamba MUNGU ataniponya.

Mwaka wa 6 yani ndio tukiwa na mwaka 1 ndani ya ndoa yetu, mke wangu alishika mimba kisha tukapata Mtoto wa kwanza.

Ili nipate uhakika, kwa siri nikaenda kupima DNA ikaonyesha wazi kabisa kuwa sikuwa Baba wa yule Mtoto. Sikumwambie, ajabu alishika tena mimba, mpaka akafikisha watoti 3, na Mimi kazi yangu ilikuwa nikupima tu kimwa kimya. Nilimlilia MUNGU anipe majibu sahihi, ivyo nikarudia tena kupima vipimo vya watoto wote 3, na wote hawakuwa wangu.

Niliishi na hii hali kwa miaka 8 nikaanza kuathiriwa na wote yani mama na watoto. Kilichokuwa kikiniathiri zaidi ni pale ambapo mkewangu anaigiza kwa kujifanya mke mzuri na mwaminifu hapo ndio niliumia zaidi. Alikuwa akifanya makongamano kanisani nakuwashauri mabinti jinsi yakuishi maisha matakatifu yakumpendeza MUNGU na waume zao huku yeye ana watoto watatu na mwanaume au wanaume wangine ata sijui.

Nilitaka kumthibishia, lakini nilijiuliza itakuwaje baada ya hapo na Mimi ni Mtumishi wa MUNGU naye tazamwa na wengi.

Basi nikawa mwenye hasira na nisiyevutiwa na yoyote ndani ya nyumba yangu. Ni nikawa nahisi kama wote ni wageni tu ambao wameletwa na Shetani katika nyumba yangu.

Nifanye nini Mimi!? Naomba unipe jibu lenye hekima ya MUNGU, maana kwa sasa siwezi ata kuomba wala kusimama mazabauni kuhubiri. Ajabu mke wangu yeye hajashtuka, ndio anazidi kujifanya anaupendo wa dhati kwangu.

KAMA MAJARIBU NI MTAJI BASI MUNGU ANISAIDIE NILISHINDE ILI JARIBU.
Share, uenda mkewangu akaiona nione atashauri nini.
 
comte,
Kama ni tukio la kweli, Basi ndugu yangu ulokole wako si sahihi haupaswi kuwa MWONGO .

Lengo la ndoa ni Nini? Hakuna lengo jingine zaidi ya kujamiiana na kupata watoto .

Kama huna uwezo wa kujamiiana na kupata watoto hiyo siyo ndoa ni uzinifu.

Ww ulitambua wazi matatizo uliyonayo Sasa kwa nn hukumjulisha mpenzi wako / mke wako ili akubali au akatae kuolewa na ww.

Umemficha Jambo kubwa Sana na yy amefanya heshima kukuficha Jambo hilo, ww unaamini hajui matatizo yako kwa taarifa yako anatambua fika ambacho hajui ni kwamba ww unajua matatizo yako .

Yy anajua ww hujui Kama huna uwezo wa kuzaa, yawezekana ndugu zako wanakusaidia kuendeleza kizazi.

Mpende mkeo na wapende watoto zako.
 
Mkuu naona msingi mbaya ulianza nao mwenyewe.
Hukuwa msema kweli kwa mwenzio ili ajipime kama ataweza kubeba msalaba wa kukusubiria wewe wakati unasubiria majibu ya Mungu kuhusu uponyaji wa tatizo lako.

Kuna wakati kuna mambo inabidi uweke ubinafsi pembeni useme ukweli hata kama kwa kufanya hivyo unaweza kumpoteza mtu unaehisi anafaa kuwa mwenza wako.
Unakuwa una okoa mengi sana yasitokee na mengine yangekuja kuwa maumivu kwako, ona sasa mfano umemuingiza mwenza wako ktk mitihani ya kukusaliti.

Itabidi tu uamini hao watoto mkeo kashika mimba kwa miujiza ya maombi mliyokuwa mnafanya na mkeo, si uliamini Mungu atakupa watoto?
Basi kakupa watoto kwa njia hiyo sio ya uponyaji bali ya miujiza kama ya Maria wa Nazareti. Kuwa na imani kama Joseph wa Maria.

Hiyo vijana wanaita alie uza cheni ya bandia kapewa fedha bandia.
 
Kwanza naamini hiyo ndoa ni batili kwa kuficha tatizo lako la kukosa uwezo wa kumzalisha mkeo.
Hii stori yenyewe imekaa kama ghahawa bila kashata.
 
Roho mtakatifu kafanya yake, wewe unaanza kulialia kama wale wasioamini.... ulishaambiwa hutoweza kuzalisha ni nini kulikuwa kinakutuma uwapime watoto..?
 
Kwanza shukuru amekufichia aibu na dharau, pili watoto ni wako kwani wamezaliwa na mkeo uliyemlipia mahari.
Tatu waheahimi na kiwapenda watoto huku ukiikibali hali yako.
Ukisanua hili timbili itateseka zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta baba halisi wa watoto kisha fahamu kama wanaendeleza mapenzi yao au la

Chagua moja samehe songa mbele

Piga talaka ubaki na majuto
 
Dah haya Mambo omba uyasikie kwa jirani yasikukute Sija ona la maana mchungaji akiamua kutalaka kwa maana ya kuto kumuharifu mapema
 
Siku hizi wanasema wanaume wote baba yenu ni mmoja, anakuacha na kusepa ila sasa ilitokea kama hivi unaambiwa mwanaume uwe mvumilivu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom