Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Duh!
Natumai airtel hawatabadilisha nao vifurushi vyao ndani ya siku kadhaa maana huu uzi wa nne tofauti nauona ndani ya muda si mrefu kuhusiana na voda.
Usiende tigo, nako majanga!

Lazima mitandao yote wapandishe na kubadili maana tatizo ni sera ya kodi ya mawasiliano..kuna mabadiliko ya kodi kwa hiyo lazima gharama zipande..muwalaumu TCRA siyo mitandao!
 
Mimi nilijua kuna ishu kumbe wanaolalamika ni wale wanaonunua vifurushi vya kisengesenge vya sh 500, lipa monthly 30,000 unakula maisha.

Wanalenga pale penye mapato mengi, watu wengi Tz tunanunua hivyo vifurushi.
 
Lazima mitandao yote wapandishe na kubadili maana tatizo ni sera ya kodi ya mawasiliano..kuna mabadiliko ya kodi kwa hiyo lazima gharama zipande..muwalaumu TCRA siyo mitandao!

TCRA hawahusiki na kodi, ni sera mbovu za ccm, raising money for campaign. Endelea kuwashobokea.
 
airtel walipunguza mb kwenye OMG huku kwengne mambo yale yale
ila voda ni muhumu kwa Mpesa tuu mambo mengine yote madudu airtel wakiboresha airtel money iwe na mawakala zaidi basi voda bye bye
 
Mwenye hisa sio Jambazi aliyejiuzulu uwaziri mkuu?
 
Nakumbuka kuna siku Chief-Mkwawa alisema haya yote yanafanywa na TCRA kwasababu mabadiliko hasa kwenye menu za mitandao yote yanaratibiwa na TCRA na yanatokea ndani ya siku moja kwa pamoja. Sasa kwa mb 8 utafanyia nin nazo?? Hawa TCRA wanataka nin kwa watanzania??

Wanatuamsha waTZ lakini sisi bado tumelala tu!!
 
kazi mnayo watumiaji wa mitandao hiyo...
 
Ushamba tu wa Internet Bongo..maana kwetu inafanywa ni anasa!Malaysia walikua na mpango wa kuifanya Kuala lumpur yote iwe Wif free..!na kuna mji wa viwanda tyr walishaunga mipango ilikua mbioni kwa pale mjini.
ila ktk public buses ni free internet..na bus lenyewe haulipi hata nauli!
 
Bongo bado sana,Wizi ndio Cv yetu mpaka makampuni sasa...wanaiba...internet yenyeewe ipo very slow..yaani we acha tu
 
maisha bora kwa kila mtz. Wameona tunachat saaana. mmmm pagumu kuna mapromoshen ya kijinga hushinda wanatangaza redioni, mbona hili kimya?
 
HUO MPANGO MZIMA UNARATIBIWA NA CCM... VODA na TIGO hawawezi wakakurupuka kupandisha mabei au kushusha vifurushi bila baraka za hawa Majambazi ya CCM..

Hiyo maana yake kile kilichoondolewa kinaingizwa kwenye Kampeni za MACCM... Kipindi cha UCHAGUZI hawa jamaa watamwaga hela nyingi sana... Nawaomba chondechonde hizi hela tusiziache, chukua bila woga ni za kwetu.. Lakini kumbuka kura kwa UKAWA..

Chukua fedha inayotoka CCM bila woga hiyo ni mali yetu watanzania..
 
Vifulushi vya masaa 24 mb 8 Sasa za niniii kama sio ushenziiii....hii nataka iwafikie vodaa Leo napasuaa laini yao rasmiii.haaaaa???
 

Attachments

  • 1423794006207.jpg
    1423794006207.jpg
    99.5 KB · Views: 262
Voda wezi sana hao bando ikiisha wanatafuna airtime moja kwa moja bila kukutaarifu.
 
Mmmh! Mb 8 hadi kwenye vocha ya buku kweli hawa kwao mteja ni zero kabisa ndio maana mi natumia airtel vocha ya mia sita ina Mb 150 na dk 25 za kupiga mitandao yote,, sasa ndugu zangu voda najua mna kiburi mna wateja wengi ila kuweni serious
 
G O O D B Y E E E
VODACOM
KAZI IMEWASHINDAAAAA
Vifushi vya masaa 24 voda kwenda voda
Tsh 150=10 sms
Tsh 500= dk 15+250sms+8mb
Tsh 650= dk 30+300sms+8mb
Tsh 1000= dk 50+300sms+8mb
vodacom kwenda mitandao mingine
Tsh 150= sms 10
Tsh 499= dk 7+300sms+8mb
Tsh 649= dk13 +450sms+8mb
Tsh 999= dk 20+1000sms+8mb
vifurushi vya wiki voda kwenda voda
Tsh 1050= sms 70
Tsh 2000= dk 60+150sms+60mb
Tsh 2800= dk 85+700sms+60mb
Tsh 4000= dk 140+1750 sms+60mb
Tsh 7000= dk 250+2100sms+60mb
Tsh 10000= dk 360+2500sms+60mb
vodacom mitandao yote kwa wiki
Tsh 1050= sms 70
Tsh 1999= dk 29+500sms+6omb
Tsh 3999= dk 49+500sms+60mb
Tsh 4999= dk 91+1000sms+60mb
Tsh 9999= dk 190+1000sms+60mb
WEWE UNAEJIITA MARKETING MANAGER......HUU
SIO UBUNIFU ILA NI UMBUMBUMBU
YOUR FIRED!!!!.......... 👹 📌 🔧
MB 8 ............NAZIPELEKA WAPIIIIIIIII HATA
MUKTASARI WA GAZETI LA MWANASPORT SIPATI......sambaza had ifke voda😡

Copy & Paste from WhatsApp friend!
 
Wakati mitandao mingine inazidi kuwajali wateja wake hawa Voda ndio kwanza wanazidi kuwakandamiza wateja wao.Kwanza mtandao umekua mbovu unatuma sms leo inafika kesho.Ngoja tuhamie kwingine
 
Back
Top Bottom