Mitandao isitumike kumchafua Rais

Mitandao isitumike kumchafua Rais

wapendwa,

kusema ukweli, nilikuwa nataka kuanzisha thread kulaumu hili la kumhusisha binti mwanaasha na kazi ya baba yake. kwa kweli si haki na tuache tabia hii mara moja! jakaya ni jakaya na mwanaasha ni mwanaasha. mimi baba yangu aliishia darasa la pili na mimi sasa nasomea shahada ya uzamivu (PhD) ulaya, na tena sio kwa kubebwa na mtu, bali kwa kushindania na kupata moja ya scholarship adimu kabisa hapa duniani!

tujiulize, kama performance ya baba ingekuwa ina uhusiano na performance ya mtoto, kwangu ingekuwaje?

nimelazimika kulisema hili kwa sababu sioni mantiki ya kumlaumu baba mwanasha kwa matokeo yasiyo mazuri ya binti yake na ambayo naamini yamemsikitikisha pia baba yake (jakaya) tena sana. hebu tujiepushe na siasa kila wakati. tukiendelea na hii tabia, tutakuwa si tu hatumtedei haki baba yake (mzee jakaya kikwete), bali pia mwanaasha mwenyewe.

yeye si wa kwanza kupata matokeo yasiyoridhisha na wala sio wa mwisho. amepata matokeo kama mtoto mwingine yoyote na kama jamii ya wastaarabu, tulipaswa kumtia moyo mdogo wangu mwanaasha ili asikatishwe tamaa na matokeo yake na ikiwezekana tuwashauri wazazi wake kumtafutia fursa nyingine nzuri zaidi za kujiendeleza zaidi.

binafsi namjua kijana mmoja (sasa ni mwanamume wa makamo), alipata div IV form 4 na baada ya kuhangaika ku-reseat, alipata div III form 6 na sasa ninavyoandika hapa ni mmoja wa wahasibu bora kabisa duniani, akiwa amekwishafanya kazi barani ulaya, afrika na arabuni akishinda usaili shindanishi na anazo tuzo kadhaa za utendaji kazi uliotukuka.

hivyo basi wapendwa, bado mwanaasha anazo fursa za kujiendeleza na nawashauri wazazi wake wasikatishwe tamaa na matokeo hayo ya mwana wao ambayo hawakuyatarajia.

nimalizie klwa kumwambia mwanaasha (kama atanisoma hapa), asikatishwe tamaa na maneno ya watu, azungumze na wazazi wake kuona namna gani watamsaidia na asonge mbele.

pole sana baba na mama mwanaasha,

pole sana mwanaasha,

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!
 
Mtu kusema kuwa Mwaansha Jakaya Kikwete kapata div IV amemchafua.
Kabla hajachafuliwa ameshajichafua mwenyewe mbona!!

Yeye kama baba si alitoa requirement zote na mwanaasha duty yake ilikuwa kusoma so jk hana kosa hapo
 
Tutamjadili, tutamkosoa na tutasemakweli, kama hataki tumjadili aachie ofisi.Mbona watu hawanijadili mimi, yeye kautaka urais basi akubali kuwa yeye ni kioo cha jamii akicheka anajadilwa,akikohoa anajadilwa akiumwa anajadiliwa, hakuna jinsi lazima tumchane live lakini bila kumkashifu wala kumtukana. UKWELI LAZIMA USEMWE.

Hapa naona hicho chombo cha habari kilichoripoti nacho kilidhani kinajipindekeza kwake kumbe ndo kimefungua mwanya wa kuanzia upya kumjadili pia na chenyewe kimeshiriki kumjadili
 
Wazazi busy na kutafuta sitting allowances hawana time na dogos zao nini kinaendelea shuleni, walai majuto ni mjukuu, vya ikulu vitamu sana, raha mstarehe, hamu ya kitabu huisha. kwani nisome nisisome baba ana nafasi sitakosa pa kwenda.
 
Kwa hiyo mnataka TUMSIFU RAIS WETU...............MILELE DAIMA?

Kama gadafe mwenyewe alikuwa akiwapa wananchi wake kila kitu ila bado tu walimkataa na kumtenda vibaya je huyu anaetoa majibu yanayochefua na ukimya kwa mambo nyeti ktk nchi huku utendaji wa timu yake ukiwa dhaifu na wezi wa mchana peupe pasipokuwajibishwa its so sad
 
kama kweli wote tulipitia posts baada ya tukio matokeo ya mwanaasha tunakubaliana kwamba mjadala ulihama kutoka kwa mtoto kwenda kwa baba.

Huyu binti Mwanaisha is l ni mdogo wala hawezi kupiga kura hence she is the responsibility of her parents who were duty bound to make sure that she performed well especially taking into account that mama Salma is a former teacher!! Rais na familia yake wanatakiwa kuwa role models in all walks of life na ndio maana wanatunzwa kwa kutumia kodi zetu; hivyo watoto wa Rais wanapofanya jambo lolote kinyume na matarajio ya jamii ,jamii hiyo hiyo inareact in different unbelieving ways!! Anybody who chooses public life must stand up to scrutiny, including their immediate family.
 
Sisi tuonacho mbele yetu ni matope tu yaliyomzunguka, na sisi tutamsiliba na hayo matope tu vinginevyo tuone mafuta yamemzunguka
 
vhelehele vyao toka kwa jk, treni imerudi nyuma nae ayameze zamu kwa zamu hapana wa kumlaumu.
 
Back
Top Bottom