Mitandao isitumike kumchafua Rais

Mitandao isitumike kumchafua Rais

Nadhani si Kumchafua, kumtukana wala kumdhalilisha. Hapa nilazima ieleweke kwamba anayajadiliwa si JK bali ni Rais wa Nchi. Nina maana gani kusema hivi, Raisi wa Nchi ni Kama Mungu wa Nchi hiyo, tunategemea Rais kuwa ni Kiongozi wa mfano, kuanzia ktk maisha yake binafsi, ya kifamilia na hata ya kinchi. ndiyo maana kila anachokifanya jamii lazima ikifahamu na inategemea kiwe ni kizuri cha mfano wa kuigwa. Nitatoa mifano michache,

1. Huko nchi zilizoendelea, bila shaka mnaona mchakato wa kumpata Rais unavyokuwa na upekenyeku, yaana ukikutwa hata na kashfa kidogo tu ya kibinafsi kabisa, unaweza usiwe Rais kwa sababu wanachokipigania watu wa huko ni hadhi ya hiyo nafasi ya Urais na wala si JK,

2. Mwalimu Nyerere ktk moja ya hotuba zake aliwahi kusema, akimtandika kibao mama Maria, ingawa ni jambo dogo kabisa la kibinafsi na kifamilia, lakini wakiipata vyombo vya habari , hiyo itakuwa ni story cover ya magazeti siku hiyo, na akasema story si kumpiga Maria kibao ila ni Rais wa Nchi kumpiga Maria kibao, kwa hiyo suala hapo ni Nafasi ya Urais,

3. Unapokuwa kiongozi wa Nyumba kwa familia zetu za kawaida kabisa, tunategemea uwe kiongozi mwenye busara na wa mfano, sembuse Rais wa nchi? Kwa hiyo mtoto wa Rais akifanya jambo tayari hiyo ni story kwa nchi, Rais mwenyewe akifanya jambo hata kama ni dogo vipi, tayari ni story ya nchi. Suala hapo ni Nafasi na hadhi ya kiti kile cha Uraisi na wala si mtu aliyepo hapo.

Kwa mantiki hiyo basi, Rais ni lazima awe msafi asiwe na dosari inayoweza kuleta picha mbaya ktk jamii ya nchi husika. Ni kweli kabisa ukisikia Rais anawake 7, ni jambo la kushtusha kwa nchi kama yetu, au mtoto wa Rais ni changudoa, tayari inamdharirisha rais, kwa hiyo nadhani, hata watu wanaotaka urais inabidi wajipime kwanza, na waelewe kuwa nafasi hiyo ni ya Public na si ya familia yake.

Kwa hiyo mitandao hii haimchafui Rais, bali nafasi yenyewe inahitaji kuchambuliwa kwa kila upande.
 
Suala hili liangaliwe zaidi ya kufikiri tu kuwa mambo ya mtoto hayahusu kazi ya baba

Sikubaliani na wale ambao pengine hawakujadili kwa hoja bali kashfa tu, lakini hiyo hainuzui kusema kuwa watoto wa viongozi kuwa katika ‘spot' ni kitu cha kawaida.

Kutokana na mahusiano na wazazi wao, wamekuwa wanafaidika na kazi za baba au mama zao pengine zaidi ya watu wengine.
Kwa vile tunakubaliana kuwa hakuna masika ya siyo na mbu, basi wanapojadiliwa zaidi ya hapo bila kashfa bado sioni kama ni tatizo bali upande wa pili wa shilingi.


Mtoto wa kiongozi anapopelekwa kutibiwa India kwa kodi zetu na kuacha mwingine Amana hospitali, hiyo ni advantage ya kazi ya baba yake. Disadvantage yake ni kuwa anakuwa sehemu ya kioo cha baba huyo huyo!!

Pili,kuna mtazamo wa kisaikolojia. Hao walioonyesha hasira na kashfa sidhani ni kwasababu hiyo tu. Pengine wanashadidia hoja kuwa mtoto huyo huyo ipo siku utamsikia ni balozi, mkurugenzi au mwenyekiti wa bodi bila juhudi ya ziada za kusafisha jina lake bali kupitia sabuni ya mzazi wake. Wanachotaka kuweka hapa ni kumbu kumbu

Hao walio na hasira na kashfa wanaweza kuwa wanasukumwa na hali ya utendaji wa mzazi wa mtoto na hivyo kuhamishia hasira zao pale wanapopata upenyo.Ni sawa na unapogombana na mtu akakutukania mama yako!

Yawezekana pia wanaonyesha hasira kwa tabaka fulani na familia zao dhidi ya tabaka jingine.

Muhimu hapa si kuangalia kashfa bila kufikiri chanzo kinaweza kuwa nini.
Mbona kuna watoto wa viongozi waliofanya vibaya na hawajadiliwi kiasi hicho?
Je, hii haiwezi kuwa frustration na kwamba inabidi iangaliwe inatokea wapi na kwanini kuliko kupapasa papasa tu kwa sentensi rahisi za kupendeza au kutetea.
 
wengine walimtukana Jk badala ya kujadili. kweli sio vizuri

Nakubaliana na mtoa hoja ingawa napenda kumfahamisha kuwa ktk viongozi wavumilivu JK NI No one na hii ndiyo sifa kubwa ya wanasiasa popote utakapokwenda, ndiyo maana mara kadhaa mh amekuwa haangaiki na wanaojadili ama kukosoa kwa kuwa anafahamu sifa ya kiongozi wa kisiasa. na kwa mpango wa hoja yako wewe unataka kumpotosha kikwete apige marufuku mitandao hii.
 
Hilo gazeti la tanzania daima ndio wamemchafua rais kijanja, kwa maana wao kutoa gazetini ndiyo wamefanya hata wale wasiosoma mitandao kuyajua hayo mambo.
 
Tutamjadili, tutamkosoa na tutasemakweli, kama hataki tumjadili aachie ofisi.Mbona watu hawanijadili mimi, yeye kautaka urais basi akubali kuwa yeye ni kioo cha jamii akicheka anajadilwa,akikohoa anajadilwa akiumwa anajadiliwa, hakuna jinsi lazima tumchane live lakini bila kumkashifu wala kumtukana. UKWELI LAZIMA USEMWE.

umeniacha hoi mkuu..
 
Du!Urais kaaaaaziiiii.....!Kweli kweli.Penye ukweli nilazima usemwe.Rais hajatendewa haki katika hili,Ukweli nikwamba ilikuwa ilitakiwa tumpongeze kwakusomesha mwanae hapa nchini!Zaidi kumkanya binti kwatomtendea haki mzazi wake kwakufeli masomo yake,zaidi tungeenda mbali kutoa ushauri nini mzazi afanye kwamatokeo kama hayo.Naamini mzazi ameumia sana kwamatokeo haya zaidi nimaneno/mijadala iliyojaa kebehi kwake kama Rais.Tenda kwawenzio unalopenda kutendewa nao!
 
Tukikijadili sana kichuguu, kinageuka kuwa kilima kidogo. Tukikijadili sana kilima kidogo, kinageuka kuwa jabali. Tukilijadili sana jabali, linageuka kuwa mlima.

Suala la Rais Kikwete kujadiliwa ni tofauti na kuchafuliwa. Mtandao wa Ze Utamu KWELI ULIMCHAFUA, na ulistahili kuondolewa. Lakini suala la kumjadili kwa matendo yake, tena wako wengi wanaomjadili kwa kumstahi (kwani wanaujua undani wake zaidi yangu mimi), si hoja nzito ya kuzuiwa kusomeka.

Rais huyu amefungua njia ya kujadiliwa kutokana na matendo yake. Kwa mfano, safari zake nyingi nje ya nchi, zinawachosha wananchi, wanashangaa, kwa nini safari nyingi huku nyumbani matatizo lukuki. Huku ni kumjadili, matendo yake.

Let us not censor our own actions and comments. Let us open doors for more dialogue. The Presidency is not the Holy Papalship! (Is this a word?)
 
at one hand ni ngumu kuhold such information katika era hii ya utandawazi....

lakini, all in all...naungana na mwandishi na muanzisha sredi hii.....


si haki hata kidogo kumfanananisha mtu na mwanae....kila mmoja ana hukumu zake kwa matendo yake.....na pia mtoto wa raisi si raisi.......

sidhani kama kuna mtu anapenda kufeli akiweka nia....hatujui kwanini mwanaasha alifeli...labda aliumwa


ukizoea kuwafanyia wenzio namna hii Mungu huwa anachukiai na kuirudisha ngoma kwa watoto wako...

lets disscuss issues!!!
 
wapendwa,

kusema ukweli, nilikuwa nataka kuanzisha thread kulaumu hili la kumhusisha binti mwanaasha na kazi ya baba yake. kwa kweli si haki na tuache tabia hii mara moja! jakaya ni jakaya na mwanaasha ni mwanaasha. mimi baba yangu aliishia darasa la pili na mimi sasa nasomea shahada ya uzamivu (PhD) ulaya, na tena sio kwa kubebwa na mtu, bali kwa kushindania na kupata moja ya scholarship adimu kabisa hapa duniani!

tujiulize, kama performance ya baba ingekuwa ina uhusiano na performance ya mtoto, kwangu ingekuwaje?

nimelazimika kulisema hili kwa sababu sioni mantiki ya kumlaumu baba mwanasha kwa matokeo yasiyo mazuri ya binti yake na ambayo naamini yamemsikitikisha pia baba yake (jakaya) tena sana. hebu tujiepushe na siasa kila wakati. tukiendelea na hii tabia, tutakuwa si tu hatumtedei haki baba yake (mzee jakaya kikwete), bali pia mwanaasha mwenyewe.

yeye si wa kwanza kupata matokeo yasiyoridhisha na wala sio wa mwisho. amepata matokeo kama mtoto mwingine yoyote na kama jamii ya wastaarabu, tulipaswa kumtia moyo mdogo wangu mwanaasha ili asikatishwe tamaa na matokeo yake na ikiwezekana tuwashauri wazazi wake kumtafutia fursa nyingine nzuri zaidi za kujiendeleza zaidi.

binafsi namjua kijana mmoja (sasa ni mwanamume wa makamo), alipata div IV form 4 na baada ya kuhangaika ku-reseat, alipata div III form 6 na sasa ninavyoandika hapa ni mmoja wa wahasibu bora kabisa duniani, akiwa amekwishafanya kazi barani ulaya, afrika na arabuni akishinda usaili shindanishi na anazo tuzo kadhaa za utendaji kazi uliotukuka.

hivyo basi wapendwa, bado mwanaasha anazo fursa za kujiendeleza na nawashauri wazazi wake wasikatishwe tamaa na matokeo hayo ya mwana wao ambayo hawakuyatarajia.

nimalizie klwa kumwambia mwanaasha (kama atanisoma hapa), asikatishwe tamaa na maneno ya watu, azungumze na wazazi wake kuona namna gani watamsaidia na asonge mbele.

pole sana baba na mama mwanaasha,

pole sana mwanaasha,

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!

Nakubaliana na maneno yako.
 
Kama gadafe mwenyewe alikuwa akiwapa wananchi wake kila kitu ila bado tu walimkataa na kumtenda vibaya je huyu anaetoa majibu yanayochefua na ukimya kwa mambo nyeti ktk nchi huku utendaji wa timu yake ukiwa dhaifu na wezi wa mchana peupe pasipokuwajibishwa its so sad

kama kuna maneno huwa yananichefua ni hii kusema Gadhafi alikua anawapatia wananchi wake kila kitu! ndugu lazima utambue kwamba chochote alikifanya Gadhafi huko Libya alitumia pesa za mafuta na gesi ya Walibya,haikua pesa yake na Libya haikua mali ya Gadhafi na familia yake! samahani nimetoka nje ya topic husika.
 
Kumjadili kikwete sioni tatizo, ni lazima ajadiliwe hata kwa mambo yake binafsi maana hiyo ni hulka ya binadamu. Kila mtu anajadiliwa inapofika wakati wa matokeo ya watoto. Katika mitaa tunayoishi watu wanasemwa kiasi kwamba kuna wazazi wanaficha matokeo ya watoto wao au wanadanganya matokeo na kuwasafirisha mbali watoto ili kuepuka adha wanayoipata mitaani. Kinachotofautisha hao wazazi na kikwete ni kuwa kikwete ni public figure kwa hiyo mambo yake hujadiliwa na watu wengi zaidi.

Na haya yanatokea duniani kote zaidi ktk nchi zilizoendelea; mfano ni tukio la waandishi wa habari kupiga picha paja la malikia Elizabeth wakati nguo yake ilipopeperushwa na upepo na hivyo kuonesha paja lake, watu walijadili paja la malikia usiku na mchana kiasi kwamba hata jambo alilokuwa anakwenda kulifanya likafunikwa. Lakini pia kumbuka ishu ya Bill Clinton na Monica Lewinsky watu walijadili suala hilo muda wote japo hilo lilikuwa la kibinafsi na halikuhusiana na urais wa Clinton.

Mwisho Kikwete kusomesha watoto wake hapa nchini ni jambo jema lakini haliwezi kutufanya tusijadili kufeli kwa Mwanaasha, kama watu wanataka tumsifu kikwete kwa kusomesha watoto hapa nchini basi waanzishe thread nyingine inayohusu hayo lakini thread iliyokuwa inajadiliwa inahusu kufeli mwanaasha.

Kumbukeni kuwa mwaka 2008 wakati Salama kikwete alipograduate Muhimbili baadhi ya magazeti yaliandika habari hiyo na kumsifu kuwa mtoto wa rais kikwete amefaulu vizuri masomo ya udaktari, lakini hakuna aliyesema maisha ya kikwete binafsi yameingiliwa au amedhalilishwa. Kwa hiyo nadhani hali hii inabidi tuikubali kuwa ni ya kawaida.
 
lakini ni kweli...tunazidi kulearn kuna element ya ULAIZAFAIRE katika familia ya JK.......wakati inajulikana kuwa ukiingia club na bastola unaikabidhi getini...rizuwani anaingia na bastola na kuiweka pembeni ya glass yake kaunta....

mie nadhani hapo TISS kuna shida kuruhusu watu dizaini hii kufika kwenye top posts....top posts zimejaa wahuni
 
Tutamjadili, tutamkosoa na tutasemakweli, kama hataki tumjadili aachie ofisi. Mbona watu hawanijadili mimi, yeye kautaka urais basi akubali kuwa yeye ni kioo cha jamii akicheka anajadiliwa, akikohoa anajadilwa akiumwa anajadiliwa, hakuna jinsi lazima tumchane live lakini bila kumkashifu wala kumtukana. UKWELI LAZIMA USEMWE.

Mkuu! - Duh! - hebu jitahidi kupunguza jazba / hasira kidogo!
 
Kwa muda mrefu mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kumchafua Rais JAKAYA KIKWETE kwa mambo ambayo hayahusiani kabisa na majukumu yake ya kuongoza serikali.

Yapo mambo mengi ambayo watu kupitia mitandao wamekuwa wakimchafua Rais na hapa nitatoa michango michache tu:-

1) Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mtoto wake aitwaye MWANAASHA KIKWETE yametumika sana kumchafua JK.
2) Thread iliyoletwa hapa JF na kichwa cha habari "Maswali mia moja kwa Rais KIKWETE" yakiwemo yaliyohoji ana wake wangapi na mengine mengi yalioonekana ni ya kumchafua Rais zaidi na hayakuwa ya kiutendaji.

Yapo mengine mengi ambayo kiukweli hata kurudia kuyaandika hapa hayafai.


Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 15/02/2012 katika ukurasa wake wa Tahariri (The Editorial page) mhariri ameandika kuhusu hili kwa kichwa cha habari "Mitandao isitumike kumchafua Rais". Amebainisha kwa uwazi na kuonya wanaomiliki mitandao hiyo wawe wanahariri na habari zinazotumwa kabla ya kuziandika katika mitandao yao.

Refference: Tanzania Daima la tarehe 15.02.2012



Wanaodhani wanamchafua JK ni wapiga blah blah tu most of them are natural born loosers; JK songa mbele mkuu
 
Kama mitandao isitumike kumchafau raisi, huyu mwandishi yeye kaamua kumvua nguo kabisa. Maana alichokifanya yeye ndio kile kile walichokifanya hao wa kwenye mitandao ya kijamii na zaidi ya hiyo yeye kahakikisha ujumbe unafikia kwa watu wengi zaidi kwa kutumia njia ya gazeti.

Labda sifa kwake ni kwa kutomtaja kwa jina mtoto wa Rais, vyenginevyo alichokifanya [na ninahisi kwa makusudi] ni kumvua nguo
 
Kwa muda mrefu mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kumchafua Rais JAKAYA KIKWETE kwa mambo ambayo hayahusiani kabisa na majukumu yake ya kuongoza serikali.

Yapo mambo mengi ambayo watu kupitia mitandao wamekuwa wakimchafua Rais na hapa nitatoa michango michache tu:-

1) Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mtoto wake aitwaye MWANAASHA KIKWETE yametumika sana kumchafua JK.
2) Thread iliyoletwa hapa JF na kichwa cha habari "Maswali mia moja kwa Rais KIKWETE" yakiwemo yaliyohoji ana wake wangapi na mengine mengi yalioonekana ni ya kumchafua Rais zaidi na hayakuwa ya kiutendaji.

Yapo mengine mengi ambayo kiukweli hata kurudia kuyaandika hapa hayafai.


Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 15/02/2012 katika ukurasa wake wa Tahariri (The Editorial page) mhariri ameandika kuhusu hili kwa kichwa cha habari "Mitandao isitumike kumchafua Rais". Amebainisha kwa uwazi na kuonya wanaomiliki mitandao hiyo wawe wanahariri na habari zinazotumwa kabla ya kuziandika katika mitandao yao.

Refference: Tanzania Daima la tarehe 15.02.2012



vijana ili tuheshimike tuachane na hili la kashfa binafsi tunaishusha JF hadhi yake...tunaonekana wote ni wahuni..nakubaliana na thread lazima tumkosoa kwa mantiki na kikazi zaidi au kimajukumu yake kama kiongozi mkuu wa kitataifa na mambo ya mtoto wake, wake zake kama hawatuhumiwi kwa lolote tuyaache mfano kama mtoto wake angekua amemaliza form sasa hivi na kapata alama hizo na amepewa scholarship hiyo ingekua ni critique ya Rais kikazi lakini siyo otherwise..sana sana haya matusi na personal attack zinamfany Rais kujihisi yuko sawa na anaonewa tu na section fulani ya wahuni...tuwe makini tumchambue Rais kikazi zaidi na kimaadili ya uongozi kutokana na desturi na tamaduni zetu za hapa ndani
 
Back
Top Bottom