Jamani jamani! chondechonde mkija Babati, si mchana wala usiku, si mwamamke wala mwanaume, si kijana wala mzee. Mtaa wa KITINTALE ni nouma, watu wote wana sura za kazi hata polisi hawathubutu pita huko.:smokin:
usimkosoe kama hujui, huyo jamaa (mwanza yote yangu) yuko sahihi, hiyo ni mitaa, kumbuka mjini hakuna vitongoji bali mitaa. Vitongoji viko huku Morogoro Vjijini, Mvomero, Mbalali, Chunya, Ileje; na maeneo hayao ni hatari tupu, ila Mkuyuni siyo pabaya sana
MWANZA ukiwa na gari usi-park ovyoovyo maeneo haya barabara ya Posta karibu na Pizzeria kuleana vinginevyo uweke ulinzi la sivyo utakuta milango iko wazi! Jamaa huwa wanajidai wanapiga story kumbe mwingine anabomoa mlango kwa mtambo maalum ambao uko design ya funguo! Mtaa Wa Karuta hapa kuna garage bubu karibia na maungano na barabara ya Kenyatta upande Wa kulia ukiwa unatokea huku msikitini wanatazamana na Busigasolwe hotel (Zamani) hawa jamaa nao huwa wanabandua nembo original za magari (mfano land cruiser Toyota, n.k), taa original za gari n.k
uwapo dar uwe makini sana ukifika manzese...kule kuna vibaka hatari, hata mchana kweupe mtu unakwapuliwa cheni au simu au kukwidwa na kunyanganywa hela. usipende kupita peke yako kwenye mitaa ya kiza na isiyoeleweka. watch out!