Miswambwanda na harufu kali ni pete na kidole

Miswambwanda na harufu kali ni pete na kidole

Mwanamke msafi, nadhifu anayenukia vizuri ndiyo mpango.... Japo usafi ni hulka ya mtu
 
Halafu mtoa mada haujafanya utafiti mtambuka, ndiyo maana comments nyingi zimekusuta kuwa unatukana.
Mada yako ni nzuri sana lakini umeitoa kihuni badala ya kuitoa kitafiti.
Tatizo hili lipo pande zote za jinsi.
Mwili wa binadamu yeyote awaye, ukiishatumika hunuka.
Kutumika kwa kazi yoyote, lazima utoe harufu.
Kitu cha kwanza kinachonukisha mwili ni bakteria wanaodakwa na mwili wa binadamu anapotoa fluid ya aina yoyote nje ya ngozi ya mwili wake.
Binadamu tuna miharufu ya ajabuajabu kila mtu jinsi alivyoumbwa.
Halafu tumeumbwa kwa kupumbazwa na harufu zetu wenyewe. Yaani pua lako halisikii harufu yako, bali harufu ya mwingine, yaani sawa na jicho lionalo taswira ya wengine, bali ya kwako halioni.
Sasa kuhusu muktadha wa mada hii ni kwamba binadamu yeyote yule, mwembamba kwa mnene, ameumbiwa harufu inayomridhisha mwenyewe lakini inayokwaza wengine.
Tukiishaelewa hivyo, basi kila mtu asijiamini pindi apangapo kujumuika na wengine, iwe kwenye mahusiano ama kukutana kwa kisogeleana.
Usafi wa hali ya juu sana unahitajika hasa unapojiandaa kwenda kufanya mapenzi.
Kuoga, kutawadha, kupiga mswaki, kupaka mafuta, lotion ama perfume.
Na maandalizi haya yafanyike mahsusi kwa ajili ya tendo.
Unaweza kujiswafi, lakini ukipita muda mrefu tayari bakteria watakuwa wamelitafuna tena jasho na harufu kurejelea.
Mtu yeyote anayefakamia kitanda bila kujiandaa kama nilivyoeleza kifupi, mtu huyo hajafundwa na hajitambui.
Kazi ya kusema kaoge, ama katawadhe si kazi ya mpenzi wako, bali ni ya kwako mwenyewe. Akiona haujiongezi, anakukwepa kimyakimya.
Tena jambo hili ni kubwa, laweza kuvuruga hadi ndoa. Maana kumwambia mshirika wako kwamba ananuka, ni jambo gumu sana kulitamka.
Hali ya uchafu ama harufu za ajabuajabu zitokeazo baada ya kuvuliana nguo ni uzembe wa makusudi ufanywao na mtu kwa kuwa muda wa kujiandaa, upo.
Tukizingatia misingi ya usafi, mapenzi kwa asili ni matamu na ndiyo faraja kuu iunganishiyo binadamu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naombeni niwanuse wote wenye misambwanda mmoja baada ya mwingine nikishamaliza nitawapa mrejesho kwa faida ya wote.
Pengine maneno ya mleta uzi yana mashiko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom