Miswada mitatu(3) ya kujadili masuala ya madini na maliasili yafikishwa Bungeni kwa hati ya dharura

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,782
5,204
Miswada mitatu ya Sheria ya Serikali imesomwa Bungeni na imepelekwa kwenye Kamati za kudumu za Bunge ili ikafanyiwe kazi ipasavyo

1. Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa 2017, utafanyiwa kazi na Kamati ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mh. Mohammed Omary Luchengerwa

2. Kwa mujibu wa Kanuni ya 7 Kanuni ndogo ya 3 ya nyongeza ya 8, imeundwa Kamati ya pamoja ambayo itafanya kazi ya kuchambua miswada ya sheria ifuatayo:

i) Muswada wa sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu masharti hasi ktk mikataba ya maliasili za nchi wa 2017

ii) Muswada wa sheria ya mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa maliasili wa 2017

Kamati hii itajumuisha Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi Maliasili na Mazingira, Kamati ya Sheria Ndogo, Kamati ya Katiba na Sheria.

Mwenyekiti wao atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Kamati itafanya kazi kuanzia 29/06/2017 hadi 03/07/2017 na kazi yake kuu itakuwa ni Kuchambua miswada hiyo miwili na kuandaa taarifa itakayowasilishwa Bungeni 04/07/2017

Kufuatia miswada hiyo, Bunge limeongeza siku 5 za kazi kutoka 30/06/2017 hadi 05/07/2017



=======

Anadokeza Mbunge John Heche wa CHADEMA akiwa Bungeni Dodoma.

"Tulisema CCM wanafanya sanaa na siasa kwenye masuala ya Madini baadhi ya watu wakashangilia upepo.

Leo tena wanaleta miswada (3) mitatu kwa "hati ya dharura" kujadili masuala ya madini na maliasili za nchi, wanataka miswada hii yote (3) mitatu ijadiliwe kwa siku (1) moja bila wananchi kupata nafasi ya kujua kilichomo hii ni aibu, na sasa CCM wanaonesha rangi zao halisi.

Haya yalifanyika kwenye Madini mwaka 1997, yalifanyika kwenye Gesi na Mafuta mwaka 2015 na yatatokea tena leo 29, June 2017, historia iandikwe!

Haya ndio chanzo cha makinikia na wizi wa rasilimali zetu, watanzania wakikubali haya ina maana tunakubali kuendelea kuibiwa"

Habari zaidi....

MBUNGE wa Kibamba John Mnyika (Chadema) amepinga kitendo cha rais Dk.John John Magufuli kupeleka hati ya Dharura ya kupitisha mswada wa sheria ya madini na mafuta na gesi.

Mnyika amecharuka muda mfupi baada ya spika wa Bunge Job Ndugai kueleza kuwa amepokea mswada wa sheria ya Madini, mafuta na gesi kutoka kwa rais ili uweze kufika bungeni kwa hati ya dharura.

Mnyika akiomba mwongozo wa Spika muda mfupi baada ya spika kutoa maelezo yake amesema ni kwanini miswada hiyo mitatu isijadiliwe katika bunge lijalo.

“Muda mfupi uliopita tumekabidhiwa ratiba ya bunge, serikali inaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura, mwaka 1997 mikataba ya madini ilipitishwa harakarahaka, mikataba ya ngesi hivyo hivyo, kazi ya bunge ni kutunga sheria, sisi ndio wawakilishi wa wananchi, kama sisi wawakilishi wa wananchi kwanini hii miswada mitatu kwa umuhimu wake na maslahi yake kwa ananchi, sisi wawakilishi tulitakiwa kukutana na wananchi, ni bora ikasomwa leo kwa mara ya kwanza na hati ya dhrarura ikaondolewa ikaletwa bunge lijalo”alihoji Mnyika.

“Kwa maelezo uliyotoa kwanini wadau wasiitwa kwa short notisi wafike Dodoma kujadili, sisi wabunge vile vile, miswada mitatu inaletwa tuichaambue, mheshimiwa spika huu ni mtego kwa kutufanya tushindwa kuishauri serikali kwa kutimiza kazi yetu ya kibunge.

“Mapendekezo haya yatenguliwe , miswada hiyo ijadiliwe katika bunge lijalo” alisema Mnyika.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama amesema Masharti ya kutunga sheria na masharti ya jumla yamewekwa katika fasihi ya nane ya kanuzi za bunge, masharti yameongezwa na kanuzi ya 80 na kanuni nyingine, miswada ambayo imeletwa imekuja katika hati ya dharura, ili bunge liridhie kama miswada hiyo inastahili kujadiliwa na bunge ama la.

“Kanuni 80(4) inasema mswada wowote wadharura haiutaingizwa katika shughuli za bunge bila kuwa na hati iliyowekwa sahihi na rais kuthibitisha kwamba muswada huo ni wa dharura.

“Kanuni zinaendelea kusema kuwa iwapo kamati inaona muswada wa sheria wa serikali uliowasilishwa kwa hati ya dharura haustahili kamati hiyo ya uongozi itaishauri serikali.

“Kanuni zinaendelea kusmea, muswada wowote uliokabidhiwa kwako spika utaonekana unastahili ama la, utatoa picha na baadaya kujadiliwa na kamati.

“Sisi kama serikali tumeshatimiza masharti yote ndani ya bunge lako tukufu, tumeshakamilisha hatua zote za kufikishwa muswada huo kwa hati ya dharura.

“Wanaoweza kulishauri bunge baada ya kuona uzito wa kazi iliyoletwa na serikali ni kamati husika itakayopewa kazi ya kujadili miswada hiyo.

“Haitakuwa busara sisi wabunge kabla hatujaona yaliyomo katika miswada hiyo tukajenga hoja ndani ya bunge ya kukataa maslahi mapana ya taifa letu bila kuangalia kilichomo ndani ya miswada, hata wabunge tulioko upande mwingine wa bunge pia tunawawakilisha wananchi” amesema Mhagama.

Awali Spika wa Bunge Jobu Ndugai alisema kwa niaba ya wabunge amepokea hati ya dharura kutoka kwa rais Dk.John Magufuli.

“Kanuni zinasema itakuja hati yenyewe yenye sahihi yake, hati ya dharura imekuja kuna haja ya kulifanyia jambo hili kazi, tulijadiliana na kamati ya uongozi tukakubaliana na suala hili ili lisonge mbele.

“Tumeunda makundi mawili, kamati moja ya kawaida na kamati ya pili ina kamati nne ndani nyake, watakaa katika ukumbi wa Pius Msekwa kuanzia leo mchana, kuanzia leo.

“Wakati rais akipokea ripotinya pili makinikia (mashapo), kwa niaba yenu nilikubali kama kuna mambo yenye maslahi kwa nchi tukayafanyia kazi, mambo yameletwa katika kamati husika, kamati itajadili kama miswada inastahili kuingia bungeni ama la hoja nitatokea huko.

“Bunge linatakia kuwa na nafasi fulani katika masuala yanayohusu maadini na gesi, liwe na nafasi fulani ili kuzuia nchi kuingia kutumbikia katika mikataba mibovu” alisema Ndugai.

Aidha amesema miswada iliyowasilishwa bungeni ataipaata katika tovuti.

Miswada mitatu mipya iliyowasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza ni muswada wa sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu masharti hasi katika mikataba ya maliasili za nchi wa mwaka 2017, muswada wa sheria ya mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa maliasili wa maka 2017 na muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali zenye upungufu uliojitokeza wa mwaka 2017.

“kamati ya uongozi ilikaa jana(juzi) kubadilisha ratiba kamba Bunge litaahirishwa Julai 5 badala ya Juni 30 kama ilivyokuwa , miswada mitatu mipya ya sheria imesomwa kwa mara ya kwwanza, itapelekwa katika kamati za Bunge.

Muswada wa kwanza wa muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali zenye upungufu uliojitokeza wa mwaka 2017 utafanyiwa kazi na Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mohammed Mchengelwa wakati mikataba mingine miwili itafanyiwa kazi na kamati ya pamoja itakayoongozwa na Dotto Biteko ambapo ndani yake kuna kamati nne.

Ngugai alizitaja kamati hizo nne kuwa ni Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Kamati ya Sheria ndogo ndogo na Kamati ya Katiba na Sheria.

Amesema kamati hizo zitafanya kazi kuanzia jana kisha taarifa itawasilishwa bungeni, Kamati itapanga jinsi ya kukutana na wadau mbalimbali na Bunge litaahirishwa Julai 5 mwaka huu.

“Kamati itapanga jinsi ya kukutana na wadau mbalimbali” alisema Spika.

======

Habari toka bungeni...

Bunge limeongeza siku za Mkutano wa Saba hadi tarehe 05 Julai 2017, ili kupitia Miswada mitatu ya sheria inayohusu marekebisho ya Sheria za Madini na ulinzi wa rasilimali za Taifa.

Akitoa maelezo Bungeni, Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alisema kuwa Kamati ya Uongozi ilikutana tarehe 28 Juni, 2017 Jioni, ili kufanya marekebisho ya Ratiba ya Mkutano wa saba Bunge ambao ulitarajiwa kuisha tarehe 30 Juni, 2017 na kukubaliana kuongeza siku tatu za kazi hadi tarehe 5 Julai, 2017 ili kuliwezesha Bunge kupitia Miswada hiyo.

Kufuatia uamuzi huo Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa ameunda Kamati ya pamoja itakayopitia Miswada miwili ambayo tayari imeshasomwa kwa mara ya kwanza Bungeni. Miswada hiyo ni;

Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-Negotiation of Unconscionable Terms)] Bill, 2017];

(iii)Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources (Permmanent Sovereignty)] Bill, 2017].

Mhe Spika alisema kuwa Kamati hiyo ya pamoja itakayochambua miswada hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Mhe Dotto Biteko na itajumuisha Wajumbe wa Kamati nne za Bunge ambazo ni Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Katiba na Sheria na Kamati ya Sheria Ndogo.

Aidha kwa upande mwingine Mhe Spika alilieleza Bunge kuwa Kamati ya Katiba na Sheria chini ya Uenyekiti wa Mhe Mohamed Omary Mchengerwa itauchambua Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2017]
 

Attachments

  • 1498723111-EXTRACTIVE INDUSTRY AND FINANCIAL LAWS-4 (1).pdf
    534.6 KB · Views: 102
  • 1498722623-PERMANENT SOVEREIGNTY (1).pdf
    330.1 KB · Views: 76
  • 1498722379-THE NATURAL RESOURCES CONTRACT (1).pdf
    245.3 KB · Views: 89
Tulisema ccm wanafanya sanaa na siasa kwenye masuala ya madini baadhi ya watu wakashangilia upepo, leo tena wanaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura kujadili masuala ya madini na maliasili za nchi, wanataka miswada hii mitatu ijadiliwe kwa siku moja bila wananchi mbalimbali kupata nafasi ya kujua kilichomo hii ni aibu na ccm wanaonesha rangi zao halisi. Yalifanyika kwenye madini 1997 ilifanyika kwenye gas na mafuta 2015 na yakatokea tena leo.haya ndio chanzo cha makinikinia na wizi, Watanzania wakikubali haya ina maana tunakubali kuendelea kuibiwa.
 
Anadokeza Mbunge John Heche wa CHADEMA akiwa Bungeni Dodoma.

"Tulisema CCM wanafanya sanaa na siasa kwenye masuala ya Madini baadhi ya watu wakashangilia upepo.

Leo tena wanaleta miswada (3) mitatu kwa "hati ya dharura" kujadili masuala ya madini na maliasili za nchi, wanataka miswada hii yote (3) mitatu ijadiliwe kwa siku (1) moja bila wananchi kupata nafasi ya kujua kilichomo hii ni aibu, na sasa CCM wanaonesha rangi zao halisi.

Haya yalifanyika kwenye Madini mwaka 1997, yalifanyika kwenye Gesi na Mafuta mwaka 2015 na yatatokea tena leo 29, June 2017, historia iandikwe!

Haya ndio chanzo cha makinikia na wizi wa rasrimali zetu, watanzania wakikubali haya ina maana tunakubali kuendelea kuibiwa".
Jamaa wanapenda posho hawa....!Hivi kweli kuna ambacho hatukijui kwenye kurekebisha sheria za madini, gesi, na mafuta??Sio kwamba inaletwa miswada mipya hapana, ni ile ya zamani ifanyiwe marekebisho ambayo tayari tumeshayapigia makelele sana!Mnataka kuendelea kutafuna kodi zetu mpk lini???Rekebisheni miswada acheni kulalama, kwanza Heche sijui kama atatoa hata mchango!
 
Jamaa wanapenda posho hawa....!Hivi kweli kuna ambacho hatukijui kwenye kurekebisha sheria za madini, gesi, na mafuta??Sio kwamba inaletwa miswada mipya hapana, ni ile ya zamani ifanyiwe marekebisho ambayo tayari tumeshayapigia makelele sana!Mnataka kuendelea kutafuna kodi zetu mpk lini???Rekebisheni miswada acheni kulalama, kwanza Heche sijui kama atatoa hata mchango!
sasa utafanyaje mabadiliko ya mswada bila kwanza kupewa nafasi ya kuusoma na kuuelewa. tusipende kurahisisha mambo kisa tu tunabana matumizi
 
Nilisikia bunge litaongezewa muda kama Mheshimiwa Rais alivyosema ili kujadili na kubadili sheria za madini, hati ya dharula ya nini tena?

Kwa nini wasipate muda wa kujadili ili wabunge wapitishe kitu wanachokielewa badala ya kusema ndiooo kwa kitu wasichokielewa.
 
Tulisema ccm wanafanya sanaa na siasa kwenye masuala ya madini baadhi ya watu wakashangilia upepo, leo tena wanaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura kujadili masuala ya madini na maliasili za nchi, wanataka miswada hii mitatu ijadiliwe kwa siku moja bila wananchi mbalimbali kupata nafasi ya kujua kilichomo hii ni aibu na ccm wanaonesha rangi zao halisi. Yalifanyika kwenye madini 1997 ilifanyika kwenye gas na mafuta 2015 na yakatokea tena leo.haya ndio chanzo cha makinikinia na wizi, Watanzania wakikubali haya ina maana tunakubali kuendelea kuibiwa.
Ngoja kwanza tumalize shunghuli za kumpongeza mwenyekiti ndo tutakuja shughulikia hii yako.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom