Mungo Park
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 2,112
- 1,831
Binafsi nafikiri kwa hapa ilipofikia hii miswada.. hamna namna.. Inabidi Wabunge wakakamae na kuipitia kwa uangalifu kila mmoja na kifungu chake kujaribu kuiboresha.
Kwa ujumla ni Sheria moja ya Marekebisho Mbalimbali yenye kurasa 86 na Sheria nyingine mbili mpya zenye kurasa 11 kila moja.
Hapa ndiyo weledi na maslahi ya Taifa yanapotakiwa kwani lazima kuna vipengele tata kwa makusudi au bahati mbaya..
1. The Written Laws(Miscellaneous Amendments) Act, 2017
2.The Natural Wealth and Resources(Permanent Sovereignty) Act, 2017
3.The Natural Wealth and Resources Contracts(Review and Re-negotiation of Unconscionable Terms) Act, 2017.

- Kwa haraka haraka Sheria ya No. 1 hapo juu katika Madhumuni na Sababu(Objects and Reasons) 'text' ya kiswahili na ya kiingereza zinapishana kwenye vipengele kadhaa
Mfano kipengele e. To eliminate all provisions... wakati 'text' ya kiswahili inasema e. Kuweka Utaratibu wa Bunge kufanya mapitio.. Yanaweza kuwa makosa ya kawaida au 'intentional' ukizingatia 'text' ya kiingereza ndiyo yenye uzito.
- Kwenye Sheria ya 2 (Permanent Sovereign.) Ibara ya 12:Review by the National Assembly : All Arrangements or Agreements entailing Extraction,Exploitation of Acquisition and use of Natural wealth and resources may be reviewed by the National Assembly.
Hii 'may be reviewed' kisheria maana yake ni kuwa hailazimishi Bunge kupitia mikataba.. inatoa 'discretion'
Ilitakiwa iwe 'shall be reviewed' ili kuweka ulazima wa Bunge kupitia mikataba.
Ilitakiwa iwe 'shall be reviewed' ili kuweka ulazima wa Bunge kupitia mikataba.
- Limetumika neno National Assembly bila kufafanuliwa mwanzoni kuwa maana yake ni Parliament of Tanzania vinginevyo inaweza kutumika vyovyote.
- Bado Bunge limenyanganywa Madaraka ya kutunga Sheria kwa Waziri kupewa uwezo wa kutunga Kanuni akiwa 'kajifungia'.. Hasa katika Sheria ya 3(Review and Re-neg.) : Ibara ya 8, Power to Make Regulations: The Minister may make regulations.. Hii inaweza kutumika vibaya..