Misungwi: Polisi wampiga mtu hadi kumuua

Misungwi: Polisi wampiga mtu hadi kumuua

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,505
Reaction score
8,256
Katika hali ya kusikitisha polisi wilayani Missungwi wamempiga hadi kufa kijana mmoja mtoto wa aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA wilaya hiyo kamanda Dickson, kosa la kijana huyo ni kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa za ugomvi uliokuwa umetokea kwenye guest house moja hapo Missungwi, cha kusikitisha na kushangaza polisi badala ya kupokea taarifa na kuzifanyia kazi walianza kumpiga kijana huyo na baadae kumpeleka hospitali ambapo ilibainika tayari keshafariki.

BABA WA MAREHEMU AKATAA KUZIKA MAITI
Katika hali nyingine baba wa marehemu bwana Dickson pamoja na ndugu wengine na Nzengo pia wamegoma kuichukua maiti hospitali na kwenda kuizika hatua ambayo ilisababisha RC Magesa Mulongo kwenda kushughulikia suala hilo kwa kuongea na ndugu pamoja na Nzengo hatua ambayo iligonga mwamba.

MTOTO MDOGO APATA ULEMAVU WA MAISHA

Katika hali nyingine ambayo mimi binafsi imenisikitisha zaidi, mtoto mmoja mwanafunzi wa shule ya msingi amesababishiwa ulemavu wa maisha na polisi hao wa Tanzania, baada ya Nzengo kujua kijana kafariki kwa kupigwa na polisi, Nzengo ilichachamaa na kuandamana kuelekea kituoni ndipo askari hao wakaitana na wenzao kutoka Mwanza Mjini na kuja kupiga mabomu hovyo hovyo kana kwamba hawana taaluma yoyote ya mambo hayo hapo ndipo kiliruka kitu kutoka kwenye mabomu hayo na kumpata mtoto huyo jichoni na kusababisha jicho la mtoto huyo kutoka, inasikitisha kwa kweli.

Hivi sasa mtoto huyo wa darasa la pili tena binti ndio tayari kawa na kilema cha kudumu maisha yake yote kisa polisi wapuuzi, huruma.
 
Mmh! Asee hii inatia uchungu sana asee. Tuko mikonon mwa wauwaji eemwenyezi tuokoe jaman
 
Duh!!!siku hz ukiwa na suala la polisi ni bora umuombee mwizi wako au mgomvi wako Mola ambadilishe kuliko kwenda polisi ambao wamegeuka kuwa ziraili mtoa mroho!!!kikwete maliza tu maana tumeshachoka mpk basi.
 
Hii habari ni ya kweli au ya kutunga?

Wasiwasi wako nini?! Hapa ni ukweli mtupu, hakuna mtu wa missungwi utamuuliza akasema hana habari hii make hadi sasa hakijaeleweka
 
Samahani mkuu ili twende pamoja "NZENGO" ndiyo nini?
 
Hakika hawa Form4 Failures na Advanced Stardard 7, ole wenu baada ya October 2015 mtatukoma.
Kaaeni mkao muda si mrefu mtalia na kusaga meno, ni lazima tufukuze Polisi wote mrudi darasani.
 
Kunahitajika mabadiliko ya sheria zinazotumika ktk jeshi la polisi.
 
Kwani hao raia hapo vipi, hawana kiberiti?

Mtani Bwana,sasa unataka WACHOME vituo au NYUMBA zao wanazoishi?Ila ninaiona hatari ya Polisi wengi either wao au familia zao kupoteza maisha.......
 
tatizo polisi wa tz hawana ethics kabisa...hapo utakuta wameweka maslahi Fulani mbele na kumpiga mtoto wa watu...yaani hii nchi tumekosa akili ya kutatua mambo kiaaluma na kibinadam...
 
Back
Top Bottom