Misungwi: Kanisa linaloendesha ibada tata labainika, takriban wagonjwa 200 wamekutwa wakihudumiwa katika mazingira duni

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Misungwi. Wakati mamlaka nchini Kenya kutambua makaburi waliozikwa waumini wa Mchungaji, Paul Mackenzie, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Paulo Chacha ameibaini kuwepo kwa kanisa linaloendesha ibada tata.

Chacha amebaini kuwepo kanisa hilo juzi Juni 8,2023 katika Kijiji cha Nyamayinza Kata ya Gulumungu wilayani humo ambapo alisema kanisa hilo linamilikiwa na William Masuma na mkewe, Kabula Lushika.

Alisema wamebaini kuwepo wagonjwa zaidi ya 200 waliolazwa na kupatiwa matibabu katika mazingira duni huku akiagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi ili kubaini iwapo kuna wagonjwa waliofariki na kuzikwa eneo hilo kinyemela.

Hata hivyo akizungumza chini ya ulinzi wa Polisi, William Masuma alisema pamoja na kuwa na kibali cha kutoa huduma ya Tiba Asili, katika eneo hilo anatoa huduma ya maombezi kwa wagonjwa pekee.

Ukifuatilia utakuta wahanga ni watoto na watu wazima wenye elimu duni na kipato kidogo.

Wazazi somesheni, Ujinga ni adui mkubwa sana. pia tutafute hela wakuu tuache kutegemea miujiza ya wagalatia
 
Sijui lini ujinga wa kuamini mafuta ya mzeituni na kokoto zinazo daiwa zinatoka Israel (wengine wanasema vinaokotwa Dodoma) vinatibu kila kitu kuanzia umasikini,ndoa, kazi na kila aina ya maradhi
 
Haya mambo ya ajabu ajabu yangekua yanatokea, kwa Islamu wengelowa matusi, wajinga ila huku huu ni weledi, watu wana muamini mchungaji, kuliko Mungu mwenyewe.
Kote kwa waislam na wakristo ujinga ujinga upo sana isipokuwa tofauti yenu ni kuwa hao wakristo wanamwachia Mungu mwenyewe awahukumu viumbe vyake ndo mana ujinga uko mwingi ila kwa waislam baadhi ya watu wanaogopa kuhukumiwa na binadamu wenzao ambao kimsingi hao watoa hukumu wanaweza kuwa waovu kuliko hata huyo wanayemhukumu.
 
Hivi sasa baada ya wateja wa Waganga wa jadi kupungua, Waganga nao wameamua kuvaa suit na kuanzisha makanisa ya mchongo Ili kurudisha uhai wa biashara Yao,

Mbingu hii imefanikiwa Kwa muda, bt tunaendelea kuwabaini, na kuwavua suit watoke ktk mwamvuli wa KANISA warudi kiringeni kuvaa ngozi kama zamani.

Kataa wahuni,

Watumishi wa Mungu wa Kweli wapo, na utawatambua Kwa matendo Yao ikiwa yanaendana na maandiko matakatifu.

Anayejiita Mtumishi yeyote anayewatamani waumini kingongo ni Mganga huyo.

Amen
 
Ukifuatilia utakuta wahanga ni watoto na watu wazima wenye elimu duni na kipato kidogo.

Wazazi somesheni, Ujinga ni adui mkubwa sana. pia tutafute hela wakuu tuache kutegemea miujiza ya wagalatia
Wakiristo wengi ni wasomi ila wanakwama kwa wachungaji na mapadire nenda kanisa la loma utakuta watu wasomi tena wamesoma mpaka ulaya likini wanaumgama kwa sanamu wakiambiwa huyo ndie mungu mkuuu
 
Ukifuatilia utakuta wahanga ni watoto na watu wazima wenye elimu duni na kipato kidogo.

Wazazi somesheni, Ujinga ni adui mkubwa sana. pia tutafute hela wakuu tuache kutegemea miujiza ya wagalatia
Hivi wakristo nchi hii si ndio kutwa kuchwa wanajinasibu wao ndio wasomi na hawajaanza kusoma leo.
 
Ni kweli kuna kundi la wajinga wa iman, wengi wanamuamini mtume, nabii, mtumishi na sio neno la mungu. Na ukienda kwenye mikutano mingi mingi ya maombi na maombezi, na upako. waislamu wanapatikana kwa wingi
 
Wakiristo wengi ni wasomi ila wanakwama kwa wachungaji na mapadire nenda kanisa la loma utakuta watu wasomi tena wamesoma mpaka ulaya likini wanaumgama kwa sanamu wakiambiwa huyo ndie mungu mkuuu
Nina uhakika kabisa wewe ni shehe.
 
Wakiristo wengi ni wasomi ila wanakwama kwa wachungaji na mapadire nenda kanisa la loma utakuta watu wasomi tena wamesoma mpaka ulaya likini wanaumgama kwa sanamu wakiambiwa huyo ndie mungu mkuuu
ELIMU ya Dunia haitoki majibu zinapokuja issues zinazohusu spirit.

Imagine unaumwa umepima Kila hospitali na unaambiwa huna UGONJWA wakati huo unahisi utaondoka anytime Kwa unavojisikia, ukifika hapo lazima atafute solution whether Kwa mganga au Kanisani.
 
#HABARI WAKATI sintofahamu ya Kanisa la Kenya lililowataka waumini wake kuishi kwa kufunga bila kula na kusababisha zaidi ya vifo 90 halijatoweka vichwani mwa watu, kanisa lingine limebainika wilayani Misungwi mkoani Mwanza, likikusanya wagonjwa na kuwazuia kwenda hospitali.

1686632056461.png
 
Back
Top Bottom