Mistari. . .

Mistari. . .

niwekeeni mistari ya vifuutundu humu jamani....lol
 
Usijigambee eti akupendaa,

Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako,

We wampenda,

Katu Usiusemee Moyo Wa Mwenzi Wakouwoo.

Verse zimetulia.
Kweli kuuusemea moyo wa mwenzio ni ngumu mno.
 
niwekeeni mistari ya vifuutundu humu jamani....lol

Vifuu tundu kwa maoni yangu ndo jisongi la mwaka!

Manake ni bonge la diss. Offside hata waje na diss 100, vifuu tundu bado itakuwa iko juu.

AT ni msanii aliye witty sana. Hata ukimsikia akiongea kwenye mahojiano unaona kweli fani ya kucheza na maneno anaiweza.

Kitu kingine kilichoipa mshiko vifuu tundu ni kumshirikisha Mwanne (mi namuita Mwafoo). Vibwagizo vyake vimeenda vidato. Mdada namzimia sana.
 
Nimeamini moyo, nificho la siri jama eee
Ningejua nisingempa penzi langu loote
Nikapoteza wapenzi wangu wootee
Nimehadaika eeee sababu yako ...............................
 
Wengi wafika chuo kwa njia za magumashi, ukiitwa mwaka wa pili haimaanishi uko peke yako wenzako wanakufa njaa mtaani na vyeti vyao sijui ni ujinga au ujana boys wanapaka poda tu hawathamini kusoma wanachowaza wao kung'oa tu
 
Nimeenda kwenye njenje kidogo: Sauti ya Nyota waziri

Gereee mama x4 wananionea gereeee....
Watausaga mtama na kuula wenyeweeee....
We mtu wa mia untaka elfu nne..x2
Kitenge umeunguza mwenyewe anakitaka..x2
Fahari eeeh ndio dawa ya mjinga...

Wa rhumba cheeee! wa rhumba henyaaaa! Leta vitu.....

mkuu mbona unanizodoa bule jamani? mi ni mtu wa mia lakini buk4 naitaka pia. hahahaaa...mia
 
Mie wanikumbusha zamani Lizzy, enzi hizo

Chura nakuulizia, unipe jibu makini
kwa kila ijapo mvua, wakimbilia bwawani
Mwanzo nilikudhania, umlinzi kisimani
mtu utamzuia, maji akishatamani
akaja dada Rukia, na ndooye mkononi
chura ukajing'atua, ukajitosa pembeni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom