Missed call ya shemeji

Missed call ya shemeji

MH! MISSED CALL YA SHEMEJI!-22

Aisha alihisi mwili kuishiwa nguvu, kila mahali alipahisi hajiwezi, akainama kuangalia chini kwa mawazo…
"Hivi huyu mwanamke nimfanye nini lakini? Yaani Ummy huyuhuyu ninayemjua mimi anaweza kunipora bwana na kunitamkia kwa kujiamini?

"Eti umeyataka mwenyewe Aisha. Ungekuwa mpole ukapewa ushirikiano, lakini meseji yako moja umenitumia kali sana. Mume wako nampenda sana na siwezi kumwacha kwa sababu wewe ni mburula…
"Hivi ana akili kweli, niwe mpole kwa mume wangu? Haitawezekana na haitatokea kwanza."
* * *
Kule kijijini dada wa Aisha alishaanza kuchakaa kwa maisha ya kijijini, siku moja alimpigia simu Beka na kumwomba shilingi elfu kumi tu apate kununua hata mafuta ya kujipaka mwilini maana alikuwa amepauka sana.
Beka kwa ubinadamu maana alijieleza sana, alimtumia shilingi elfu hamsini huku akimwambia amemmisi sana…"Hata mimi nimekumisi sana baby wangu, daa! Lakini vipi nyumbani kwako, ni amani tu au?"
"Hakuna cha amani, mdogo wako eti sana ndiyo ameyajua makosa yake, siku zote hakuwa anajua."
"Mvumilie tu. Sasa mimi nakuja lini huko baby?"
"Nitakwambia, lakini je, wazazi watakuruhusu kuja Dar?"
"Sitasema nakuja Dar."
"Utasema unakwenda wapi?"
"Moshi kwa rafiki yangu anaitwa Bitte."
"Oke, basi wikiendi hii nitakutumia pesa uje, lakini utafikia wapi?"
"Si gesti jamani! We unadhani nitafikia wapi kama si gesti?"
"Sawa."
* * *
Aisha alianza kuwa mpole kwa mumewe, hata alipochelewa kurudi hakumuuliza aliko wala atarudi saa ngapi! Na mumewe aliporejea alikutana na uso wa tabasamu kutoka kwa mkewe tofauti na zamani.
Na kila siku, Aisha alimsihi mumewe kuachana na tabia yake ya nyuma ya kumnyima unyumba kwani amebadilika sasa na anajitambua.
* * *
Wikiendi ilifika, Beka alimtumia pesa shemeji yake kwani hata yeye kutoka moyoni alilimisi sana penzi la shemejiye huyo.
Baada ya kupokea mshiko huo wa nauli, dada wa Aisha alimwambia mama yake kwamba anakwenda Moshi kwa Bitte. "Muage baba yako si mimi," alisema mama mtu. Akamfuata baba'ke…
"Baba samahani, ninaomba ruhusa niende kwa Bitte, Moshi."
"Bitte gani?"
"Yule rafiki yangu, mtoto wa mzee Telekamalombi."
"Ameolewa yule au bado?"
Dada ake Aisha hakujua maana ya swali la baba yake, yeye akaamini kwamba akisema hajaolewa, baba yake atamsema anakwendaje kwa mtu asiye katika ndoa, akasema…
"Ameolewa baba, ana familia yake kwa sasa."
"Basi hakuna kwenda."
Alishtuka dada ake Aisha, iweje akataliwe kwenda wakati mtu ameshamwambia ana familia…
"Wewe umeishi kwa mdogo wako, Dar yaliyotokea unayajua leo hii unataka kwenda kwenye ndoa nyingine ili ukaitibue siyo? Hakuna kwenda nimesema."
Aliingia chumbani na kuanza kulia sana akidai baba yake anamfuga kama mtoto. Alimtumia meseji Beka…
"Baby, baba amekataa mimi kusafiri. Sina cha kufanya."
"Pole sana, vuta subira iko siku atakubali tu, usiwe na haraka."
* * *
Siku hiyo, Aisha aliamka akiwa na hasira zilizopitiliza, aliamua kwenda kazini kwa Faidha ili kuzungumza naye kwa njia yoyote ile, iwe kwa ujeuri au busara pungufu lakini lengo akampe vidonge vyake…
"Angekuwa mwanamke mwenye busara kichwani angeamua kuachana na mume wangu maana amejua kwamba kumbe mimi ndiye mke wa Beka, lakini yeye bado anamng'ang'ania, kwa nini?" alisema moyoni Aisha akiwa anatoka kwake.
Alifika kazini hapo na kukutana na mlinzi yuleyule wa siku ya kwanza…
"Samahani, naweza kuonana na Faidha?"
"We si ndiyo ulikuja siku zile?"
"Ndiyo mimi."
"Oke, ofisi yake si unaijua ilipo?"
"Ndiyo."
"Oke, basi pita."
Aisha alipita kwenda ofisini kwa Faidha huku akiziandaa hasira. Aliamua kumwadhiri mbele ya wafanyakazi wenzake wajue kwamba anaiba bwana wa mtu!
Ile anazama ndani tu, anakutana na mumewe Beka naye anainuka kutoka kwenye kiti, mezani kwa Faidha…
"Faidha, nimekufuata wewe, lakini bahati nzuri nimemkuta na mume wangu leo," alisema Aisha kwa sauti iliyotulia kama hana wasiwasi…
"Nimefanya nini? Hapa ni kazini kwangu ujue Aisha," alisema Faidha akiwa amemtumbulia macho Aisha. Mumewe, Beka alikosa nguvu, alishindwa kusimama sawasawa, akakaa.
"Unajua unafanya nini na mume wangu? We ni mtu wa kunichukulia bwana kweli Ummy. Unajifanya unaitwa Faidha, kumbe Ummy! Loo! Ukome naseema Ummy," alipayuka Aisha mbele ya wafanyakazi wenzake Ummy.
 
MH! MISSED CALL YA SHEMEJI!-22

Aisha alihisi mwili kuishiwa nguvu, kila mahali alipahisi hajiwezi, akainama kuangalia chini kwa mawazo…
“Hivi huyu mwanamke nimfanye nini lakini? Yaani Ummy huyuhuyu ninayemjua mimi anaweza kunipora bwana na kunitamkia kwa kujiamini?

“Eti umeyataka mwenyewe Aisha. Ungekuwa mpole ukapewa ushirikiano, lakini meseji yako moja umenitumia kali sana. Mume wako nampenda sana na siwezi kumwacha kwa sababu wewe ni mburula…
“Hivi ana akili kweli, niwe mpole kwa mume wangu? Haitawezekana na haitatokea kwanza.”
* * *
Kule kijijini dada wa Aisha alishaanza kuchakaa kwa maisha ya kijijini, siku moja alimpigia simu Beka na kumwomba shilingi elfu kumi tu apate kununua hata mafuta ya kujipaka mwilini maana alikuwa amepauka sana.
Beka kwa ubinadamu maana alijieleza sana, alimtumia shilingi elfu hamsini huku akimwambia amemmisi sana…“Hata mimi nimekumisi sana baby wangu, daa! Lakini vipi nyumbani kwako, ni amani tu au?”
“Hakuna cha amani, mdogo wako eti sana ndiyo ameyajua makosa yake, siku zote hakuwa anajua.”
“Mvumilie tu. Sasa mimi nakuja lini huko baby?”
“Nitakwambia, lakini je, wazazi watakuruhusu kuja Dar?”
“Sitasema nakuja Dar.”
“Utasema unakwenda wapi?”
“Moshi kwa rafiki yangu anaitwa Bitte.”
“Oke, basi wikiendi hii nitakutumia pesa uje, lakini utafikia wapi?”
“Si gesti jamani! We unadhani nitafikia wapi kama si gesti?”
“Sawa.”
* * *
Aisha alianza kuwa mpole kwa mumewe, hata alipochelewa kurudi hakumuuliza aliko wala atarudi saa ngapi! Na mumewe aliporejea alikutana na uso wa tabasamu kutoka kwa mkewe tofauti na zamani.
Na kila siku, Aisha alimsihi mumewe kuachana na tabia yake ya nyuma ya kumnyima unyumba kwani amebadilika sasa na anajitambua.
* * *
Wikiendi ilifika, Beka alimtumia pesa shemeji yake kwani hata yeye kutoka moyoni alilimisi sana penzi la shemejiye huyo.
Baada ya kupokea mshiko huo wa nauli, dada wa Aisha alimwambia mama yake kwamba anakwenda Moshi kwa Bitte. “Muage baba yako si mimi,” alisema mama mtu. Akamfuata baba’ke…
“Baba samahani, ninaomba ruhusa niende kwa Bitte, Moshi.”
“Bitte gani?”
“Yule rafiki yangu, mtoto wa mzee Telekamalombi.”
“Ameolewa yule au bado?”
Dada ake Aisha hakujua maana ya swali la baba yake, yeye akaamini kwamba akisema hajaolewa, baba yake atamsema anakwendaje kwa mtu asiye katika ndoa, akasema…
“Ameolewa baba, ana familia yake kwa sasa.”
“Basi hakuna kwenda.”
Alishtuka dada ake Aisha, iweje akataliwe kwenda wakati mtu ameshamwambia ana familia…
“Wewe umeishi kwa mdogo wako, Dar yaliyotokea unayajua leo hii unataka kwenda kwenye ndoa nyingine ili ukaitibue siyo? Hakuna kwenda nimesema.”
Aliingia chumbani na kuanza kulia sana akidai baba yake anamfuga kama mtoto. Alimtumia meseji Beka…
“Baby, baba amekataa mimi kusafiri. Sina cha kufanya.”
“Pole sana, vuta subira iko siku atakubali tu, usiwe na haraka.”
* * *
Siku hiyo, Aisha aliamka akiwa na hasira zilizopitiliza, aliamua kwenda kazini kwa Faidha ili kuzungumza naye kwa njia yoyote ile, iwe kwa ujeuri au busara pungufu lakini lengo akampe vidonge vyake…
“Angekuwa mwanamke mwenye busara kichwani angeamua kuachana na mume wangu maana amejua kwamba kumbe mimi ndiye mke wa Beka, lakini yeye bado anamng’ang’ania, kwa nini?” alisema moyoni Aisha akiwa anatoka kwake.
Alifika kazini hapo na kukutana na mlinzi yuleyule wa siku ya kwanza…
“Samahani, naweza kuonana na Faidha?”
“We si ndiyo ulikuja siku zile?”
“Ndiyo mimi.”
“Oke, ofisi yake si unaijua ilipo?”
“Ndiyo.”
“Oke, basi pita.”
Aisha alipita kwenda ofisini kwa Faidha huku akiziandaa hasira. Aliamua kumwadhiri mbele ya wafanyakazi wenzake wajue kwamba anaiba bwana wa mtu!
Ile anazama ndani tu, anakutana na mumewe Beka naye anainuka kutoka kwenye kiti, mezani kwa Faidha…
“Faidha, nimekufuata wewe, lakini bahati nzuri nimemkuta na mume wangu leo,” alisema Aisha kwa sauti iliyotulia kama hana wasiwasi…
“Nimefanya nini? Hapa ni kazini kwangu ujue Aisha,” alisema Faidha akiwa amemtumbulia macho Aisha. Mumewe, Beka alikosa nguvu, alishindwa kusimama sawasawa, akakaa.
“Unajua unafanya nini na mume wangu? We ni mtu wa kunichukulia bwana kweli Ummy. Unajifanya unaitwa Faidha, kumbe Ummy! Loo! Ukome naseema Ummy,” alipayuka Aisha mbele ya wafanyakazi wenzake Ummy.

Shikamoo daudi
 
MH! MISSED CALL YA SHEMEJI!-23

ILIPOISHIA
We ni mtu wa kunichukulia bwana kweli Ummy. Unajifanya unaitwa Feidha, kumbe Ummy! Loo! Ukome naseema Ummy," alipayuka Aisha mbele ya wafanyakazi wenzake Ummy.
CHOMOKA NAYO MWENYEWE SASA…


asa ofisi ilikuwa kama sokoni, mzozo ulianzia hapo kwani Feidha naye hakuwa tayari kudhalilisha mbele ya wafanyakazi wenzake, tena wadogo kwake kicheo.
Aliamua kujibizana na Aisha…
"Kwani kosa langu mimi ni nini? Mumeo mwenyewe kaja kwangu na kusema unampimia unyumba kama mafuta ya kula, sasa je?"
"Lini alikwambia kama si umbeya wako?"
"Muulize mwenyewe."
"Si huyu hapa, lini alikwambia?"
Watu waliokuwemo kwenye ofisi hiyo walijitoa kuweka hali sawa lakini mzozo uliendelea…
"Kama ungekuwa mwanaume kweli si ungetafuta mume wako?" alisema Aisha kwa sauti iliyojaa kebehi…
"Na wewe ungekuwa mke kweli si ungekuwa unammwagia unyumba mumeo, angehangaika nje kufanya nini? Loo! Hata sijui kama ulifanyiwa kitchen party wewe na kama ulifanyiwa ulikula fedha za shughuli tu," alitema cheche Feidha.
Meneja mkuu wa benki alitokea akiwa mbogo baada ya kunyetishiwa kuwa, ofisini kwa Feidha kuna timbwili zito…
"Ni nini hapa?" aliuliza meneja huyo. Alipoona hajibiwi na Feidha wala Aisha, achilia mbali Beka ambaye ilibidi arudi kukaa kwenye kiti, aliwauliza akina Salma…
"Eti kuna nini?"
"Huyu dada kaja anasema eti Feidha kampora mume wake."
Meneja alihisi ni kitu kikubwa, mfanyakazi wake kudaiwa mambo kama hayo ni kuichafua taasisi, akatuliza hali ya hewa, akataka watu wengine watoke nje, akabaki yeye, Beka, Feidha na Aisha tu, akakaa…
"Feidha, niambie ukweli. Huyu ni mume wa huyu dada?"
"Ni kweli bosi."
"Kaka, ni kweli wewe mkeo ni huyu dada?"
"Wote wake zangu."
"Ah! Sasa kama wote wake zako kwa nini huyu anamshutumu huyu kuwa amekupora wewe."
"Huyu ni wivu wake tu."
"Eti dada, unamtambua Feidha kama ni mke mwenzio?" alimuuliza Aisha sasa…
"Mi nadhani dada jibu la mfanyakazi wako limetatua kila kitu, maana mwenyewe amekubali huyu ni mume wangu na hakusema yeye ni mke mwenzangu. Aliyeleta hayo mambo ni huyu mume wangu. Mimi nadhani nisimulie kidogo."
"Hebu simulia kidogo," alisema maneja huyo ambaye ni mwanamke.
Aisha aliweka wazi uhusiano wake na mume wake, alikoangukia ni wapi na anakotaka kwenda ni wapi.
"Kwa hiyo ni kweli ulikuwa unamnyima unyumba mume wako?" aliuliza meneja.
"Ni kweli."
"Mh! ulipata wapi hayo mawazo?"
"Ya?"
"Ya kumnyima unyumba mume wako!"
Aisha alinyamaza hapo, hakuwa na jibu.
"Kwa hiyo hata wewe unakubali kwamba ulifanya makosa?"
"Nakubali dada."
"Oke, enhe? Feidha! Wewe ulipokutana na huyu bwana alikusimulia matatizo ya ndoa yake?"
"Ndiyo, ndiyo maana nikampokea. Kwani hata mimi kama mwanamke nikiolewa siwezi kumnyima unyumba mume wangu," alisema Feidha kwa sauti iliyoonesha kupata tumaini jipya!
"Sasa licha ya hayo yote Feidha, je ilikuwa halali wewe umchukue mume wa mwenzako kisa amekusimulia kwamba ananyimwa unyumba?"
"Si sahihi," alijibu kwa kudakia Feidha.
"Lakini anti, mbona mimi hunipi muda wa kuzungumza?" alihoji Beka akionesha kuwa na shauku ya kutaka kusema…
"Sema."
"Ni hivi, mimi nimeamua kwa imani yangu kuwa na wake wawili, Feidha na Aisha. Hilo hata Aisha analijua, nilimwambia. Kama kosa ni mimi kusema kuhusu matatizo ya mke wangu ni kawaida. Kila ndoa duniani ukiuliza wanandoa, wana asili ya kukutana.
"Kwa hiyo mimi nilikutana na Feidha nikamsimulia matatizo ya mke wangu. Lakini ikawa ndiyo asili au chanzo cha mimi kujuana na Feidha hadi kufikia hatua ya kuwa mke wangu."
Wakati Beka anazungumza hayo, kutoka moyoni, Feidha hakuwa anapenda kusikia neno uke wenza. Hilo alikuwa halipendi toka anasoma shule ya msingi, aliweka ahadi kwamba hatapenda kuwa mke mwenza. Iwe kuanza yeye au kukuta mke mwenzake.
"Sasa kaka, kama kweli ulimwambia mkeo kuhusu uke wenza huoni kama hataki ndiyo maana amekuja juu?"
"Atataka tu."
"Feidha," aliita bosi huyo."
"Abee bosi."
"Unalijua suala la wewe kuwa mke wa pili?"
"Kusema ukweli bosi ndiyo nalisikia, niliambiwa ataachana na mkewe, mimi nitachukua nafasi, lakini kama ni uke wenza, siko tayari."
Mjadala ulikuwa mzito, alichotaka meneja huyo ni kutuliza ule mzozo wa awali…
"Sasa sikieni, wewe Aisha na mume wako nendeni zenu. Mkifika nyumbani jadilianeni kuhusu hilo la uke wenza, mkikubaliana sawa, mje mniambie mimi, niko tayari kumsimamia ndoa Feidha," alisema meneja.
Aisha na Beka walikubaliana, wakaondoka wote kwa wakati huohuo huku Beka akichukua business card ya mwanamke huyo kwa ajili ya mawasiliano.
Baada ya wawili hao kuondoka, meneja akamgeukia Feidha…
"Feidha."
"Ndiyo bosi wangu."
 
MH! MISSED CALL YA SHEMEJI!-24

ILIPOISHIA

Baada ya wawili hao kuondoka, meneja akamgeukia Faidha…
“Faidha.”“Ndiyo bosi wangu.” RUKA NAYO SASA…“


Unajua ni jambo la ajabu sana limetokea?”
“Sijaelewa bosi.”“Mwanamke kuja kufanya fujo hapa kazini!”
Faidha aliposikia hivyo alibaki amejiinamia tu kwa aibu kwani hata dhamira yake ilimwambia kilichotokea si cha kawaida.
“Ni kweli bosi.”
“Kama ni kweli itabidi uandike barua ya kujieleza kwa nini uongozi usikuadhibu?”
“Samahani bosi.”“Mimi langu ni hilo tu,” alisema bosi huyo huku akitoka kwa hasira.
Faidha alikaa na kujiinamia. Mawazo kibao kichwani yalimpata. Alianza kukasirika na yeye akiamini bila Aisha yasingetokea yale yote…
“Dawa yake yule kumchukulia mume wake moja kwa moja sasa,” alisema moyoni Faidha akijiapisha kwa dhati.Akina Salma nao walirejea baada ya kumuona bosi wao ametoka…
“Kwani dada Faidha vipi? Yule mwanamke ana akili timamu kweli?” walimuuliza…
“Ah! Yule kachanganyikiwa, kabip akapigiwa sasa anatapatapa tu…yeye angedili na mumewe si kuja ofisini kwa watu.”
“Ni kweli dada Faidha, sisi wenyewe tumemshangaa sana. Halafu hata wewe huna kosa kwani ulimuita aje hapa?”“Si ndiyo hapo sasa!”
“Mh! Wanawake wengine bwana, ni wa ajabu sana,” alisema Salma…
“Wa ajabu wa ajabu,” alimalizia Faidha.
***
Beka na Aisha walifika nyumbani, kila mmoja alitaka kumsikia mwenzake anasema nini kuhusu lilitokea lakini Beka akaonekana kutosubiri, akaanza…
“Mwezi ujao nafunga ndoa na Faidha.”
“Si alisema pale hataki uke wenza, hukumsikia?”
“Hatakuwa mke wenza, wewe nakupa talaka yako sasa hivi, sitaki ujinga mimi!”
“Unipe talaka nimekukosea nini mimi?”
“Hujui ee?” Basi subiri utajua tu.
Haiwezekani uwe mwanamke wa fujo, hekima imekupitia pembeni wewe,” alifoka Beka, akaenda kununua karatasi dukani na kumwandikia talaka Aisha.
Siku ya pili, Aisha alirudi kwa wazazi wake na kusimulia yaliyompata akaambulia kupewa pole nyingi. Alikaa kwao kwa mwezi mmoja akarudi mjini kuanza maisha yake mwenyewe, Beka akafunga ndoa na Faidha.
**************************
MWISHO
Shukrani za dhati zije kwenu wasomaji wa hadithi hii tok mwanzo mpaka mwisho, ni matumaini yangu pamoja na kuburudika lakini kuna funzo mmepata maana kazi ya fasihi haiendi bure, wanawake mliomo kwenye ndoa yawapasa kutambua kuwa tendo la ndoa si adhabu bali ni sehemu ya mapenzi hata kama mume wako anataka kila siku yakupasa umuhudumie maana ulijua hilo toka mwanzo na ukaamua kuingia kwenye ndoa kwa malengo ya kukabiliana nalo, japo haimaanishi hiyo ndo sababu pekee ya kufanya mwanaume asichepuke ila tendo la ndoa husaidia kupunguza migogoro ndani ya nyumba, "waswahili wanasema ukipenda ua penda na boga lake", kama unahisi umechoka tafuta lugha ya kumwambia menzio ili akuelewe
 
Mm haijanifrahsha mwisho wake,,,,inaonesha hakuna room for improvement,,,,mm nltegmea aisha atapata second chance,,,,bt anyway ni hadith tu
 
Back
Top Bottom