Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na mama yake wahamia CHADEMA kutoka CCM

JF week hii yote inamzungumzia Wema Sepetu hakuna cha madawa wala nini!

Nimeamini Huyu dada ana nguvu sana katika jamii yetu. Hata sisi wana CCM tumeshangazwa sana kumbe Huyu siyo mtu wa sport sport.

Naamini kuna kundi kubwa ameondoka nao kuelekea CDM ingawa hatutaki kukubali ukweli.

Najiuliza nguvu hizi zote anazitoa wapi???
Kwani hujui JF 80% ni CHADEMA?
 
ha ha! huwezi kuijua thamani ya mke mpk siku akikuacha! ndo hii sasa..
hivi mtu kajitutumua toka 2006 unafikiri mchezo..? wasanii pia wanahadhi yao ktk jamii ndio maana hata wanasiasa huwatumia
wananguvu yakupendwa/kuwavutia watu kutokana na kile anachokifanya

Uko sawa kabisa, Mkuu.
 
Ndo nashindwa kuelewa akili za watanzania. Wema ni nani? Halafu eti jitu linaweza kuhama chama kumfuata Wema! Au kupigia kura mtu fulani sababu ya Wema. Wakati mwingine huwa namhurumia rais anayeongoza watanzania kama alkili zao ndo hizi za uwema wema!
Tukaneni sana Wema lakini uchaguzi wa 2015 aliwasaidia sana ccm kupata kura za nyongeza
 
Kuna watu wamezaliwa hivyo, wao wana nguvu ya ushawishi kiasili Wema ni miongoni mwao. Hata kama mtu haitaki aongelewe watu wataongea tu kumuhusu. Angalia ni wasanii wangapi waliitwa polisi lkn wote wamesahaulika, lkn Wema bado ana make headlines.
 
Binadamu ni binadamu tu. Msidharau watu. Kila moja apate haki yake.
Ulaya watumia bangi hupelekwa rehab. Hapa wanapelekwa jela. Je tunaheshimu sifa kuliko uhai wa mtu?
 
Ameshindwa kusoma alama za nyakati..waliohama wote wana haha!
 
Hata kipindi cha Lowasa, Sumayi na Kingunge pia mlisema mambo haya na bado ccm inadunda, lakini Mwl.Nyerere alitamani upinzani wa kweli na huo upinzani ni ccm kugawanyika mara2- lakini bado hakijfanyika hata robo yake- Wema ni mtu mdogo sana ndani ya ccm ila nimaarufu kwenye magazeti ya udaku.
lowassa kura mil.6 magufuli kura mil.8, bado huamini kwamba utabiri wa Nyerere ni sahihi na unatimia?
au kugawanyika kwako ni kwa mtindo gani?
 
Huyu ni "big drug dealer" ndio maana anaongelewa sana na duniani kote hawa watu huwa na nguvu sana, usishangae ndugu

Ukiambiwa katoe ushahidi utaweza?? Jamani Watanzania mwenzangu Tusipende Watanzania wenzetu sababu ya chuki na utawala basi tuwatafitie maovu ya kupambika.

Inamaana alipo kuwa anatemeba na mama Suluhu Hassan alikuwa anavuta ngada na mkamuacha afe tu??Hapo ndipo shaka yangu ilipo.Acheni upumbavu huu UVCCM.

Chuki ya nini kwanza hata kesho yako huijui
 
Hahahaha. Tatizo mkiambiwa ukweli.
Si unaona! Haikukawia mmeshajibu, walahi! Na Mimi sioni noma kikubwa msiweke mitusi tu! Jana nilisafiri na Zitto Kabwe, tukapiga story hamna noma! Hekima na busara muhimu sana ndugu yangu!
 
Si unaona! Haikukawia mmeshajibu, walahi! Na Mimi sioni noma kikubwa msiweke mitusi tu! Jana nilisafiri na Zitto Kabwe, tukapiga story hamna noma! Hekima na busara muhimu sana ndugu yangu!

Ungejua mie na matusi ni sawa na Chuo Ba mpaka.Sina muda wa kukutukana maana napoteza Calories zangu bure.
 
Back
Top Bottom