Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na mama yake wahamia CHADEMA kutoka CCM

hahahah Mbowe akiamua kumpa Wema Sepetu hata ukatibu mkuu wa chama leo hakuna kamanda yoyote atafungua bakuli lake...CHADEMA ina wenyewe nyie wengine ni bendera fuata upepo tu
.....
.....vipi jomba vikao vimekwisha ...Wema Sukuma Moyo wangu
 
Mimi siwezi kutafakari faida ama hasara kwa chama alichokihama.
Maana tangu jana kuna clip ina"display" youtube kuonesha jinsi tangu mwaka juzi alivyotaka kuhongwa dolar 2k ili ahamie Chadema, nadhani sasa watakuwa wameongeza dau na kufikia kiasi alichokuwa anakihitaji.
Kwa hiyo hamahama hii ni biashara ya maslahi binafsi, hakuna jambo lolote lenye taswira ya tijara kwa umma hapo, hakuna.
Hizi ngebe zinazopigwa humu jf kiushabiki, hazioneshi jinsi gani mawazo ya waTz makini wanavyoona Cdm inavyozidi kuwa dodoki la kufyonza kila aina ya taka.
Kinazidi tu kupoteza umaarufu kwa watu wapenda mageuzi na kuonekana sasa ni chama cha wachumia tumbo, wavuta bangi na kila aina ya mawaa.
Tunakoelekea, muda utaongea , pia muda utakuwa ni hakimu wa hizi figisufigisu zinazoendelea sasa nchini.
Mambo yote haya yatafikia tamati chungu, mbichi na mbivu zitafahamika. Na tukae tusubiri.
kufanya tu uchambuzi juu ya wanachama, kwamba huyu yuko hivi na huyu yuko hivi ni dalili njema kwa chama, kwani, walipokuwa kule kwa nini hawakuchambuliwa? sasa walikohamia wanachambuliwa, we huoni kama hapo kuna kitu?
 
Wakuu:
Hii yote imesababishwa na mkuu wetu wa mkoa.
Cheo alicho nacho hakiendani na Umri/Hekima/Busara sambamba na wadhifa wa ukuu wa Mkoa.

Na hii ni ishara mbaya kwa CCM.
Wanachama ni kama wateja kwenye biashara yeyote ile yenye ushindani, haitakiwi kumpoteza hata mwanachama mmoja.

Hivyo mkuu wetu wakaya ni vyema angetafakari kwa kina na kuchukuwa uamuzi wa haraka.
"...........vinginevyo............."
Hivi wewe ccm??
 
Hakuna shida yoyote. Shida ni pale watu wa Chadema wanapoamini CCM itaathirika. Ndio maana Barbarosa akasema, viliishaondoka vingunge lakini CCM ikabaki imara!

Umekua msemaji wa Wanachadema? Au unaongelea Fikra zako na kuzipandikiza kwa CDM! Kwani Wema ni Wakwanza kuiacha ccm ?
 
Walishindwa nini? Kwani Hugo wema umeona chadema wamemshawishi au hasira zake? Chadema haina shida Na wema
 
isijekuwa anafanya usanii?? usimuamini msaniii tena wakike....

chadema angalia huyu mtu kwa makini
 
Kazi kweli kweli....inamaana huyu demu nae anadhani anaweza washawishi watu wenyefamilia zao wamuelewe...mi ningeskia wema amebeba mimba karibia anajifungua ningeona kitu cha maana...mziki wa huyu mzee ni shida ni wachache watauhimili...kwa hiyo chadema sisi kazi yetu ni kupokea waharifu eee
 
Hivi chadema hakuna wenye akili siku hizi?Au siku hizi ni Chadema-madawa ya Kulevya?
Mnafikiri mnamkomoa Magu?
Sio kwa siasa nyepesi kama hizi!
Yaani Wema mnamuandalia jukwaa?
Mnafikiri headline mtakazopata kwa Wema zitadumu kwa siku ngapi?
Nitafurahi sana siku Wema akiondoka huku akiwatukana matusi ya nguoni!
Itikadi hamna siku hizi?Wema anaifahamu?ataifuata?
Nyie kwenu ni bora tu kuwa na watu bila kujali kiwango cha ukichaa?
Ninasikitishwa sana na upuuzi huu
Kisokorokwinyo ña kiroho papo
 
Ni hiari ya mtu yeyote kujiunga na chama chochote, na wala hajakosea, ingawa kwa mtazamo wangu sioni kama CCM imepoteza lolote kwa kuhama kwa huyu Mwana dada, ambaye wala sikuwahi kuhisi uwepo wake ndani ya chama.
Sivutiwi Na maisha ya wema Lkn inabidi ujijaze UJINGA kichwani kukataa athari ambazo chama cha mapungufu kitapata kwa kuondokewa Na Huyu kiumbe. Na itabidi uwe chizi kukataa kuwa CCM haikutingishwa Na kuondoka Kwa Lowassa kutoka ushindi wa asilimia 80% mwaka 2005 mpaka asilimia 58% mwaka 2015 . Au mamba haipandi ndugu 80 -58=22 hii inamaana chama kimeshuka . Pia athari za kingunge Huwezi kufananisha Na wema wapiga kura wengi ni vijana Na wengi wao Ndio wale vilaza ambao Magufuli alisema. Lkn inapokuja kupiga kura uzito wa kura ya kilaza ni sawa Na ya mwenye PHD. Ni mfungwa Na chizi pekee ambae hapigi kura.
 
Mimi siwezi kutafakari faida ama hasara kwa chama alichokihama.
Maana tangu jana kuna clip ina"display" youtube kuonesha jinsi tangu mwaka juzi alivyotaka kuhongwa dolar 2k ili ahamie Chadema, nadhani sasa watakuwa wameongeza dau na kufikia kiasi alichokuwa anakihitaji.
Kwa hiyo hamahama hii ni biashara ya maslahi binafsi, hakuna jambo lolote lenye taswira ya tijara kwa umma hapo, hakuna.
Hizi ngebe zinazopigwa humu jf kiushabiki, hazioneshi jinsi gani mawazo ya waTz makini wanavyoona Cdm inavyozidi kuwa dodoki la kufyonza kila aina ya taka.
Kinazidi tu kupoteza umaarufu kwa watu wapenda mageuzi na kuonekana sasa ni chama cha wachumia tumbo, wavuta bangi na kila aina ya mawaa.
Tunakoelekea, muda utaongea , pia muda utakuwa ni hakimu wa hizi figisufigisu zinazoendelea sasa nchini.
Mambo yote haya yatafikia tamati chungu, mbichi na mbivu zitafahamika. Na tukae tusubiri.
Utakuwa na bahati mbaya sana kuendelea kuamini ktk kuuza, kununua na kununuliwa. Hakika Ccm wametuweza ktk hili. Maana yake wewe na kizazi chako-- kilichotangulia na kinachofuata mko kwenye mstari huo. Ni aibu kushindwa kuugrade ufahamu wako. Ninyi ndiyo wale mliamini Lowasa kujinyea jukwaani na kuinunua Chadema-- endelea kukomaaa ktk muktadha huo.....
 
45 Reactions
Reply
Back
Top Bottom