figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Habari: Miss Tz 2006, Wema Sepetu na familia yake watakuwa na Press Conference Saa 5 asubuhi nyumbani kwao Sinza-Meeda.
Waandishi wote wanakaribishwa.
Hiyo ndiyo meseji ya kutoka kwa akina Wema wenyewe kwenda kwa waandishi Asubuhi hii.
=======
Wema akidai hajalipwa fedha za kampeni na CCM
Update: 1337hrs: Bado anasubiriwa Wema Sepetu hajafika, wanafamilia wengine akiwemo Mama yake na Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ndo wapo.
1345hrs: Wema Amewasili na Kuanza Kuongea kama ifuatavyo:
Mama wema: Habari za mchana, nawakaribisha
Wema: Kwa jina naitwa Wema Sepeti Isack Abraham
Wema: Naomba mnisamehe kwa kufika kwa kuchelewa
Wema: Sitakuwa na mengi ya kuongea, nataka kutoa tamko moja kutoka kwa Wema mwenyewe
Wema: Nimewaiteni hapa kuja kutamka rasmi kwamba hivi sasa nmehamia CHADEMA kutoka CCM
Wema: Sio kwa tuhuma zinazonikabili bali nmefanya maamuzi kama mtu mwingine yoyote
Wema: Nyote mnajua nlikuwa kada wa CCM na nmepigania chama kwa uwezo wangu wote
Wema: 2015 niligombea ubunge viti maalum Singida na kura hazikutosha na sikufa moyo
Wema: Marehemu baba yangu alikuwa kada nguli wa CCM na alipata kuwa hadi mshauri wa rais Zanzibar, Waziri na Balozi wa Urusi. Amekufa akiwa CCM
Wema: Nimetuhumiwa hivi karibuni, wakati najitoa kwa hali na mali ndani ya CCM na niliamini hawatanitupa na haina maana kwamba nilitaka kubebwa hapana
Wema: Kilichotokea kwangu kilikuwa ni uonevu
Wema: Nimetafakari sana kwanini hili limetokea
Wema: Kama mwanachama kimenivunja moyo. Tenda wema uende zako usingoje shukurani
Wema: Mimi naamin katika demokrasia. Nimefanya reseach yangu na hata wakati wa kampeni CHADEMA ilitupa tabu
Wema: CHADEMA inapigania demokrasia na mimi nataka uhuru wa watu
Wema: Ningejua mapema ningenijiunga CHADEMA zamani. Najilaumu sana kuchelewa kujiunga CHADEMA
Wema: Bado sijachelewa kufanya maamuzi. Na hii najua nimeingia kwenye vita na naamini watu wengi wapo wananiunga mkono
Wema: Dola ifanye kazi zake na kifuata sheria kama dola. Ila wazingatie haki za binadamu
Wema: Naamini ndani ya CHADEMA tunaweza kuleta mabadiliko nchini
Wema: Kwa kupitia nguvu ya CHADEMA tunaweza pata ule uhuru tunaoupigania.
Tangu leo mimi sio mwanachama wa CCM. Mimi na mama tulikuwa wanachama hai wa CCM
Kwa upande wake mama Sepetu, alikuwa na haya ya kusema;
Mama Sepetu :Mmekuwa mnasema natoa mapovu,mimi sitoi mapovu
Mama Sepetu :Uchungu wa mwana aujuae mzazi
Mama Sepetu :Nmehangaika sana mwanangu alipowekwa ndani
Mama Sepetu :Ningejua mapema ningejiunga CHADEMA zamani.
Mama Sepetu :Najilaumu sana kuchelewa jiunga CHADEMA.
Mama Sepetu :Wema hakuzungumza sana mimi sasa ndo nguli nazungumza
Mama Sepetu :Ametuhumiwa sana. Amekaa sero hamjamuona mwanangu akiwa alosto. Anayetumia unga wiki moja tu akikosa unga anaishiwa nguvu, Mtumia madawa anakuwa hivi?
Mama Sepetu :Hamna kiongozi wa CCM alokuja kuniuliza kulikoni
Mama Sepetu :Mpaka usiku wakina wema walikuwa wanafuatwa mahabusu na Makonda
Mama Sepetu :Haki za binadamu hazikuzingatiwa, watu wanaua wanapewa dhamana.
Mama Sepetu :Lakini yeye(Wema) kahangaishwa sana
Mama Sepetu :Mimi ni mwenyekiti wa CCM tawi la Nzasa kata Kijitonyama tulikuwa na kura nyingi 2015
Mama Sepetu :Nchi hii Mambo hayaendi vizuri, Wengi hawataki kuzungumza wanauguliwa sana
Mama Sepetu :Sisi ni Watanzania tumebanwa tupo kwenye kitanzi
Mama Sepetu: Mimi kama mama nimesema siwezi kuteswa na mwanangu kudhalilishwa tukiwa chama cha mapinduzi
Mama Sepetu: Mwanangu amezunguka na CCM anainadi nchi nzima
Mama Sepetu :Tangu leo mimi sio CCM tena. Na nitatembea nchi nzima kukinadi chama cha demokrasia na maendeleo.
Mama Sepetu :Nashangaa CHADEMA hawatupi kadi zao.
Mimi ni mwenyeji wa Singida. Baba katuacha tupo 72. Naenda kupokea kadi za CCM Singida na wote wameahidi kuhamia CHADEMA
Wema: Naomba maswali matatu yanayohusiana na mimi kuhama
Swali: Unaidai CCM?
Majibu ya Wema: Wasanii wengi ikiwemo mimi nawadai, nikianza kuzungumzia madeni watasema ni kwa sababu tumehama. Mimi na wasanii wengine tunawadai CCM lakini wanatujibu tukamdai Kikwete rais mstaafu.
Mariam anauliza swali kuhusu voice note
Majibu ya Mama Wema: Mimi siku nyingi nimezima simu yangu, sijui wala sijaangalia kitu gani kimezungumzwa. Japokuwa nmesikia kwamba kuna sauti. Siijui kabisa
Mimi simu yangu ina matatizo, siwezi kuisikiliza hiyo sauti, mlioisikia ni nyinyi sio mimi
Steve ni mtoto wangu sasa hiyo sauti yangu na Steve siijui
Wala sijawahi kuisikia ila nina mpango wa kuisikiliza simu ikipona
Je huu uamuzi ni wa hasira?
Wema: Hapana sio wa hasira, nimepata hasira kura za viti maalum na ndo ningehama. Hadi hapo CCM ilipo ina jasho langu na nguvu zangu.
Nimeonewa na nimefanywa nijisikie mnyonge ndani ya chama
Nilijitoa ikibidi nife. Nilipoenda Zanzibar wanachama wa CUF walitaka kunimwagia tindikali kisa mimi ni wa CCM. Walinimwagia michanga. Hiyo yote ni katika harakati za kuitetea CCM
Leo chama ndo kimefanya nipitie yote Haya
Mapenzi ni nipe nikupe, mapenzi yakiwa ya upande mmoja sio mapenzi
Je chadema wamekununua?
Majibu: CHADEMA hawajanipa hata sh 10. Ni mapenzi yangu tu. Hayo mambo ya fedha tumezoweshwa kwa sababu chama cha mapinduzi ndo mtindo wao.
Huu ni uamzi mgumu sana, na mimi nikishasema basi ni basi. Sirudi nyuma.
CHADEMA wanapigania demokrasia. Tanzania yetu imeanza kupoteza demokrasia kwa kiasi kikubwa.
Sijaingia kwenye mitandao. Natamani niingie na kutoa kale kapicha ka CCM nilichokipost tatizo sijapata muda wa kuingi kwenye mitandao.
Kama ni vita nimeshavaa magwanda nipo tayari kupigana
CHADEMA wamenipokea kwa mikono miwili
Swali: Kuna mtu mkubwa una bifu naye, CCM unafanyiwa hivi, je CHADEMA si itazidi?
Kwanza kabisa sina bifu na mtu yoyote kutoka CCM
Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge
Kumbuka mimi nina kesi mahakamani, tunachopigania ni uhuru na demokrasia. Maswali yametosha. Asanteni sana

~MWISHO~