Misingi ya kuwa kinara wa ICT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misingi ya kuwa kinara wa ICT

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Mar 17, 2011.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Walenga wana usemi unaosema nabii hakubaliki kwao,hii ni kweli kwa mida fulani ila kuna wakati inabidi ujitahidi ili uweze kukubalika au kuaminika. Katika dunia ya leo,kila mtu anataka kufanya kazi au biasha ra na mtu anayemuamini na kumkubali. Hapa siwamaanishi wale wanaopenda ujanjaujanja.Hivyo ni jukumu letu kujijengea uaminifu.

  Jiulize,je umehudhuria mikutano mingapi ya wana ICT au wanajamii.Na ulipofika kule ni wangapi wametumia muda wao kubadilishana mawazo nawe yanayohusu ICT? Ni mara ngapi umekuwa ukipokea simu za kuomba msaada juu ya matatizo ya ICT toka kwa wanajamii? Hiyo itakupa jibu la ukubalikaji wakokatika jamii husika.

  Tumekuwa tukisika vinara(superstars) katika fani mbalimbali ikiwemo muziki,filamu nk,je sisi kama wana ICT tutawezaje kuwa vinara ? mfano mzuri chukulia watu kama Billgate,ni moja kati ya vinara ndani ya ICT,sio tu kwa nchini kwao,bali dunia nzima.Kama ilivyo kawaida yetu,leo hii tutaangalia ni vitu gani vinaweza kukusaidia ili kuibuka kinara ndani ya uwanja wa ICT?

  1.Pata uzoefu:

  Neno uzoefu si neno geni kwa wengi wetu,kwani mutakumbuka kipindi unahangaika kutafuta kazi kila sehemu ukienda wanataka mtu mwenye uzoefu,sasa swali linakuja,je huu uzoefu nitautoa wapi? Swali hili lina majibu mengi ambayo yanategemeana na muhusika,Kutokana na ukubwa na umuhimu wa ICT,basi ni sehemu nyingi bado wameweka milango wazi kwa wasio na uzoefu ila wana maarifa ya kutosha kuweza kujifunza tokea kwao.

  Kwa kuwa na uzoefu itakusaidia katika kuendesha mambo yako,sio tu kwa kuajiriwa bali hata kama utaamua kujiajiri mwenyewe.Uzoefu huohuo ndio utakao kusaidia kujenga jina na kuwa kinara kwakuwa utakuwa na mzunguko mkubwa(chanels).Vilevile zitakuwezesha kufanya kazi zako kwa umakini na kujiamini kitu kitakachokuongezea pointi kwenye soko la mavinara.

  2.Chagua muelekeo
  Si umewahi kusikia usemi wa watu wakisema mimi ni kilaka,ninaziba popote? Usemi huu huwapoteza wengi mno,kwani ICT yenyewe ni kubwa mno,hivyo kama utaendelea na ukilaka utajikuta siku ya mwisho kila unaziba ila ukiivaa hiyo nguo mtu anaona,pale pamewekwa kilaka.Kwani kila sehemu wewe unajua kwa asilimia ndogo mno na huwezi kufanya mambo kwa ukamilifu wake kama kilaka kilivyofanya,binafsi nimewahi kukutana na watu wengi wa karibu yangu,ambao yeye kila idara yumo,ukimuuliza kwanini anasema mimi ni mwana ICT,hii fani ni kubwa hivyo ninahitajika kujua mambo mengi.Sasa kukija kwenye utendaji,kazi inakuwa nzito.

  Labda niweke sawa hapa,kwakuwa vipengele vingi vya ICT vingi vina uhusiano,hivyo unaweza kujikuta kipindi unaenda kwenye muelekeop mmoja,umejifunza vingine vingi vya upande mwingine kwa uchache wake,kwa mfano chukulia wewe ni web designer au developer, ni dhahiri kuna wakati mwingi unatakiwa kujua mambo fulani ya mitambo endeshi(OS) kwani kila mtambo endeshi una matendo na tabia zake, hivyo siku ya mwisho unajikuta unafahamu jinsi ya kutatua matatizo ya mitambo hii,ila uelekeo wako(sehemu ambayo unaitilia mkazo) ni bado kwenye web design.
  Kwa kuchagua uelekeo mmoja,itakusaidia kutumia muda mwingi sehemu moja na kushika vitu kwa undani wake kitachokupelekea kukubalika na kuaminika.

  3.Toka kivyako

  Ndio inawezekana,kama umefuatilia historia ya makampuni makubwa yote ya ICT,kuna baadhi ya watu(mtu) aliamua kutoka kivyake na kisimamisha kitu,kwa mfano kaka wewe ni mtaalam wa kupiga code,basi unaweza kuamua kuja na project yako ya mtambo endeshi,au search engine. Ingawa vyote hivi si vitu vya kukurupukia, vinahitaji muda na uvumilivu wa kutosha hadi kufanikiwa.

  Kumbuka kwa kuamua kutoka kivyako itakusaidia mno kujifunza mambo mengi na kujuana na watu wengi ambao usingetegemea kukutana nao.Kwa mfano binafsi nimeweza kukutana na maelfu wa wataalam wa kitanzania na wasio watanzania toka maeneo mbalimbali kupitia AfroIT. Pia kwakuwa na kitu chako(chenu) itakusaidia kuwa makini na kufanya mambo kwa uthabiti zaidi.

  4.Anza mdogo

  Kuna methali nyingi mno ambazo zote zinaelezea na kutilia mkazo umuhimu wa kuanza polepole,kumbuka ICT kama fani nyingine inakuwa inahitaji hazina nyiingi mno,na nyingi zao huwa zinagharmu muda na pesa kitu ambacho kwa wanaoanza huwa ni ghali.

  Jaribu kuanza kwa kushirikiana na wenzako, kwa mfano kwenye makundi ya barua pepe(mfano yahoo group), nakumbuka binafsi kipindi nimeanza kuwa na moyo wa kuipenda ICT nilijiunga na kundi moja linaloitwa Tz E Think Tank ambalo linatumia yahoo group, nikawa mchangiaji mzuri tu,
  baada ya hapo nikajiunga tena na jamii Forums(Jambo Forums kipindi kile) na kujitahidi kuandika makala nyingi ambapo nikawa mchangiaji mzuri wa upande wa technology,baada ya hapo nikaja na Forums,ambayo ilikuwa ni uwanja wa kujadiliana na hadi leo tumekuwa na hii AfroIT na kesho kunakuja AfroIT Kisima na mengineyo.

  Sasa kama ukiangalia kuna mlolongo ambao una malengo na hautoleta utata wala ukinzani.Hivyo anza polepole.Usitake kuanza ghafla bin vuu na kila mtu akujue,utadonsoka kifo cha mende.

  5.Kuwa mwandishi

  Ukweli ni kuwa sio kila mtu anaweza kuwa mwandishi,ila kila mtu anaweza kujifunza kuwa mwandishi kwani elimu haina mwisho na kila hatua ya maisha ni mwendo wa kujifunza tu. Kwa kuwa mwandishi kwanza utajenga kujiamini, pia utaweza kukuza kipaji chako, pia utaweza kuongeza ujuzi kwani pindi unapoandika kitu chochote ni lazima utumie muda mwingi kujifunza na kuangalia kazi za wenzako hivyo unapata mididi vilevile utapokea maoni mengi kitu ambacho kitapelekea kujua watu wengi zaidi hata kama yalikuwa ni maonii ya kukosoa si unakumbuka wagombanao ndio wapatanao.

  Binafsi nilipoanza kuandika makala za kwanza enzi zile kwenye jambo forums,ilikuwa ni mchanganyiko wa kiswahili na kingereza,ila siku zilivyozidi kwenda mbele nimejifunza na ninaendelea kujifunza zaidi.Pia mmoja wa watu ambaye alikuwa anaandika maoni ya kukosoa mno kazi zetu leo hii ni moja ya watu wangu wa karibu na tumekuwa tukishirikiana kwenye mengi.

  Vilevile,kwa kuwa mwandishi utapata kujuana na wengi kwani baada ya kuandika utapenda kutuma makala zako sehemu mbalimbali na wengi wataweza kukuja kupitia huko.

  6.Jichanganye
  Wengi wanaamini kuwa wana ICT hawana muda,sio tu wa kufanya mambo ya jamii ,bali hata wa kula.Ingawa wengi wa wana ICT ni watu walio bize na mambo mengi,ila kumbuka kutafuta kamuda angalau kujichanganya na wanajamii.Hii itakusaidia sana,kwani wanajamii watapata wasaa wa kukuona na kubadilishana matatizo au kutaka msaada toka kwako.Hii itakujengea heshima na uaminifu kwa jamii kwani wao ndio wanaoona kazi zetu na kutukubali.

  Kwa leo ngoja niishie hapa,ila kama una lolote la kuongezea basi usisite kuchangia, mlango umefunguliwa.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Very nice.
  Thanks.
   
 3. Freelancer

  Freelancer JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 2,649
  Likes Received: 1,166
  Trophy Points: 280
  Nini maana ya kinara wa ICT? you mean kuwa mtaalamu wa ICT aliyebobea au kufanikiwa financially kwa kuanzisha biashara katika ICT bado sijakuelewa. Na hiyo Afro IT is it a a company generating money au ni forum tu.
   
 4. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Tafadhari hebu jaribu kuelezea kwa ufasaha nini maana ya ICT, maana hakuna mahali ulipo fafanua maana ya hicho unacho ongelea. Ingawa maelezo ni mazuri lakini fafanua tukuelewe vizuri.
   
 5. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2015
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,091
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  sipsndagi mimaneno mengiiiii
   
 6. MWANASIASA HURU

  MWANASIASA HURU Senior Member

  #6
  Jan 10, 2015
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nice contents. Appreciated
   
 7. Kaliro X

  Kaliro X JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2015
  Joined: Apr 18, 2013
  Messages: 635
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Useful info,, thanx
   
 8. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2015
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,354
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Kirefu cha ICT ni INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGY, kwa Kiswahili tunaita TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
   
 9. v

  vladtepes Member

  #9
  Jan 14, 2015
  Joined: Nov 26, 2014
  Messages: 48
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nice thread Kilongwe
  Hopefully some day we also will meet and do some work together. I appreciate this
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...