Misheni kubwa za taasisi ya upelelezi MOSSAD!

Kwa kifupi n kwamba tubalance shobo

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Nina vitabu viwili vya ROBIN SHARMA
1. THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI
2. DISCOVER YOUR DESTINY

Mungu akinipa nafasi nitaviweka kwenye jukwaa hili..
Naamini vitakuwa msaada sana kwa watu wengi...
Kuna mahali anazungumzia;
※ watu wenye mapungufu wasioyajua.
※watu wenye mapungufu wanayoyajua ila wasiojua namna ya kukabiliana nayo.
※watu wenye mapungufu wanayoyajua na wanajitahidi kukabiliana nayoa japo kwa njia zisizo na uhakika sana.
※watu wenye mapungufu na wanayafahamu na wanafahamu kwa hakika ni njia gani wazitumie kuyakabili na wanayakabili kwa umahiri mkubwa.

Nadhani sisi wote tuko kwenye moja ya hizo hatua.. tukipata muongozo mzuri tunaweza kuacha haya mambo ya kulipuka.
Kimsingi mtu anayewalipukia wengine kila wakati ana msongo mkubwa wa mawazo, hafurahii maisha yake kwasababu moja au nyingine... ameipoteza nafsi yake na hajitambui tena..

Ila akipata muongozo na akawa tayari kubadilisha matendo na tabia ili kurudia nafsi yaka safi na yenye amani na furaha aliyozaliwa nayo, basi mtu huyo atayafurahia maisha yake na itakuwa rahisi sana kuziona fursa na kutimiza ndoto za maisha yake.
 
Nina vitabu viwili vya ROBIN SHARMA
1. THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI
2. DISCOVER YOUR DESTINY

Mungu akinipa nafasi nitaviweka kwenye jukwaa hili..
Naamini vitakuwa msaada sana kwa watu wengi...
Kuna mahali anazungumzia;
※ watu wenye mapungufu wasioyajua.
※watu wenye mapungufu wanayoyajua ila wasiojua namna ya kukabiliana nayo.
※watu wenye mapungufu wanayoyajua na wanajitahidi kukabiliana nayoa japo kwa njia zisizo na uhakika sana.
※watu wenye mapungufu na wanayafahamu na wanafahamu kwa hakika ni njia gani wazitumie kuyakabili na wanayakabili kwa umahiri mkubwa.

Nadhani sisi wote tuko kwenye moja ya hizo hatua.. tukipata muongozo mzuri tunaweza kuacha haya mambo ya kulipuka.
Kimsingi mtu anayewalipukia wengine kila wakati ana msongo mkubwa wa mawazo, hafurahii maisha yake kwasababu moja au nyingine... ameipoteza nafsi yake na hajitambui tena..

Ila akipata muongozo na akawa tayari kubadilisha matendo na tabia ili kurudia nafsi yaka safi na yenye amani na furaha aliyozaliwa nayo, basi mtu huyo atayafurahia maisha yake na itakuwa rahisi sana kuziona fursa na kutimiza ndoto za maisha yake.
Poapoa

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ila walioanza kumshambulia Alex kwa kejeri haikuwa poa, kama mtu ameweka story kwa nia njema na ameomba (hakulazimisha mtu) mchango kidogo wa mb kwa aliyekuwa nayo shida ni nini hapo, kama hauna ni bora ukae tu kimya au usisome thread yake na usome hicho kitabu chako, kuliko kumshambulia mtu, mbona kuna watu wameanzisha story humu wakaziamishia Telegram kujiunga kwa pesa 'no one cares' au Alex kaja tofauti sana? Sio poa waungwana as long as hatujuani, itoshe tu kuheshimiana na kuthamini mchango wa kila mtu (ndio maisha ya great thinkers yanavyokuwa).
 
Tuendelee...

SHUSHUSHU WA KISOVIETI NA MWILI WA MTU BAHARINI

Sehemu ya Saba.

Kazi zake zilizofuata wakati wa vita ya uhuru zilitoa hakika ya umahiri wake na utashi wake ulio tayari. Wakati Isser akikusanya timu yake ya operesheni, alisajili watu wenye historia tofauti tofauti: wanusurika wa mauaji ya halaiki, maveterani wa Palmach na Haganah, wanachama wa zamani wa Irgun na kikundi cha Stern - wapiganaji wa mrengo wa kulia ambao aliwahi kuwawinda wakati wa mapambano kabla ya kuundwa kwa Israel. (Moja ya waliosajiliwa na Yitzhak Shamir, alikuwa kiongozi wa kikundi cha Stern na atakuja kuwa waziri mkuu baadae). Rafi aliteuliwa kama kiongozi wa timu ya operesheni. Alisafiri kwenda Rome, pamoja ma majasusi Taphael Medan na Emmanuel (Emma) Talmor. Majasusi wengine waliungana nao baadae kidogo.

Mara moja wakapangilia shambulio katika uwanja wa ndege wa Rome Fiumicino. Katika maelekezo yao ya mwisho kabla ya kuondoka, Isser aliwaamuru kumzuia Avner Israel katika uwanja wa ndege. "Hapaswi kabisa kuingia kwenye hiyo ndege. Tengenezeni ugomvi wa uongo, mzidini nguvu, muumizeni ikobidi. Na hizo njia zote zikishindwa - mpigeni risasi afe!"
Hiyo ni mara ya kwanza kabisa kwa kibali cha kuua kutolewa kwa majasusi wa Israel.

Ila shambulio katika uwanja wa ndege halikutokea. Taarifa za safari ya Misri zilikiwa na makosa; Israel aliendelea kukaa Rome kwa muda,na halafu, ghafla, akaomdoka na akaanza kusafiri kwenye nchi za Ulaya, na timu ya Eitan ikiwa miguuni mwake. Kama vile alijaribu kuwapoteza wale waliomfukuzia, alienda Zurich, Geneva, Genoa, Paris, Vienna...
Na mara, kwa ghafla, Kapteni Israel akapotea. Majasusi wa Mossad walimtafuta kila mahali, lakini wapii.. Ila baadae, bahati ya iliyozoeleka kwa Rafi Eitan ikajitokeza. Huko Vienna kulikuwa na muisrael, mjumbe wa taasisi ya siri, Nativ, ambaye misheni yake ilikuwa kutorosha wayahudi kwa ndege kutoka Urusi na kambi ya mashariki - na kuwaleta Israel. Huyu mjumbe wa Nativ alikuwa na uhusiano wa karibu na Mossad. Siku moja ya December, mke wake, aliyezaliwa Bulgaria alikuwa na "surprise" kwake.

"Hutaamini hili", alisema, huku akimkonyeza. "Hii asubuhi nikiwa natembea mtaani, nimekutana na rafiki yangu kutoka Sofia. Sikuwa nimemuona kwa miaka mingi. Tulisoma shule pamoja; kwenye darasa moja! Bahati iliyoje unadhani?". "Kweli? Anaitwa nani?" Mumewe akauliza. "Alexander Israel. Tunakutana kesho kwa chakula cha mchana". Huyu mjumbe wa Nativ alijua kuhusu msako wa Eitan kwa mtu ambaye alifanania kwa wajihi na maelezo ya mke wake na mara moja akamtahadharisha.
Siku iliyofuata majasusi wawili wa Mossad walienda kupata chakula cha mchana katika mgahawa uleule, na wakakaa karibu na ambako ,Alexander Israel na rafiki yake toka utoto, walitarajiwa kukaa.
Pindi Israel alipoachana na mke wa mjumbe wa Nativ, waligandana nae kama kivuli. Siku chache baadae, "Alexander Ivor" alipanda ndege ya shirika la ndege la Austria kuelekea Paris. Katika kiti kilichofuata alikaa msichana mrembo na anayevutia sana. Ivor, .....

Itaendelea...
 
Officially nakuachia kijiti, malizia mkuu!
Soon mimi nitaanza kitabu kingine na Richard Flanagan - Njia nyembamba kuelekea ndani kabisa ya Kaskazini " The narrow road to the deep North".

Hicho komaa nacho..
Mkuu achana nao maana kuna watu wana wivu kama mademu..anaweza kumuonea wivu dada yake kwa shemeji yake
 
Tuendelee...

SHUSHUSHU WA KISOVIETI NA MWILI WA MTU BAHARINI

Sehemu ya Nane.

...malaya aliyekubuhu, akaanza mazungumzo na yule mrembo, na akaitikia kwa upole. Wakakubaliana kukutana tena huko Paris angalau wabarizi kwa usiku mmoja. Kidogo kabla ya ndege kutua, yule mrembo akamgeukia afisaa: "Kuna marafiki zangu wananifuata hapa uwanja wa ndege. Ungependa kuungana na sisi? Nina uhakika kutakuwa na nafasi kwenye gari". Ivor alifurahi.

Hapo uwanjani, wanaume wawili waliovalia vizuri walikua wakimsubiri huyo mrembo. Wote wanne wakaingia ndani ya gari na kuelekea Paris. Ivor alikaa pembeni ya dereva. Usiku ulikuwa umeingia; dereva akamuona mtu aliyekuwa amesimama eneo lenye mwanga hafifu la makutano ya barabara akipunga mkono, akawa kama anayeomba lifti. "Acha tumchukue", alisema dereva. Akasimamisha gari, na ghafla 'muomba lifti' na wanaume wengine kadhaa, wakatokea kutoka kwenye giza, wakilifuata gari, wakati huohuo gari nyingine ilisimama nyuma yao.

"Tunatekwa!" Ivor alipaza sauti. Mara mtu aliyekuwa nyuma yake akampiga roba kwenye koo. Ivor akawa akipambana kujinasua kwenye ile roba. Mlango wa gari ukafunguliwa na mtu aliyekuwa amesimama nje ya gari akamrukia Ivor na kumzidi nguvu. Alitoa bastola na kufoka kwa Kiebrania: "Ukijigusa tena - hesabu umekufa!"
Mkono, ulioshikilia kitambaa chenye kemikali ya 'chloroform' kikabandikwa usoni mwake, na Ivor akatumbukia katika usingizi mzito.

Alifikishwa kwenye 'nyumba ya usalama' - 'safe house' huko Paris kwa siri, ambapo Rafi Eitan pamoja na watu wake walimuhoji. Alikiri kuwa ameuza nyaraka za siri sana kwa wamisri, na alifanya hivyo ili kujipatia fedha. Kutoka Israel, Isser alituma amri kwa telegraph kuwa Ivor arudishwe Israel. Hata msaliti aliyekosa maadili kabisa, aliamini, alipaswa kupelekwa mahakamani, na haki zake za kisheria kuheshimiwa. Eitan na watu wake wakamchoma Avner sindano za madawa, wakamuweka kwenye boksi kubwa la mbao, na wakampakia kwenye ndege ya jeshi la Israeli ya mizigo - Air Force Dakota, iliyokuwa ikiruka mara moja kwa wiki kutoka Paris kwenda Tel Aviv.

Safari ya kurudi nyumbani ilikuwa ndefu na yakuchosha. Ndege ilipaswa kuongeza mafuta Rome halafu tena Athens. Daktari maarufu - mtaalamu wa ganzi kwa jina la Yona Elian - alisafiri na hiki kikosi. Kabla ya kila kutua na kupaa, daktari alimchoma abiria wao sindano yenye dawa ya usingizi.
Ila baada ya kuruka kutoka Athens, balaa likatokea. Avner Israel, akiwa hajitambui, ghafla akaanza kupumua kwa nguvu; mapigo yake ya moyo yakaongezeka na kuwa sio ya kawaida. Dr. Elian alijitahidi sana kumrudisha kwenye hali ya kawaida ikiwa ni pamoja kujaribu kurudisha mapigo yake ya moyo kwa kumuongezea hewa kwa njia 'bandia', ila bila mafanikio. Muda mrefu tu kabla ya ndege kutua Israel, mfungwa alikuwa amefariki.

Mara tu baada ya kutua, majasusi wa Mossad walimpigia Isser simu na kumjulisha juu ya kifo cha Israel. Ramsad akawaelekeza kuuacha mwili kwenye ndege na kumwamuru rubani kurudi angani. Mbali kutoka ufukwe wa Israel, mwili ulirushwa kutoka kwenye ndege.

Itaendelea....
 
Tuendelee...

SHUSHUSHU WA KISOVIETI NA MWILI WA MTU BAHARINI

Sehemu ya Tisa.

Hii bahati mbaya isiyotegemewa ilileta msuguano mkali katika makao makuu ya Mossad. Isser akawahi ofisini kwa waziri mkuu, Moshe Sharett, na kumuomba ateue bodi ya uchunguzi kuchunguza kifo cha huyu afisa. Sharett akateua bodi ya watu wawili, ambayo iliwasafisha majasusi wa Mossad kutokuwa na kosa lolote. Yote waliyofanya, bodi iliamua, ilikuwa kumpeleka mtu huyo kwenye utaratibu wa sheria; na hawakupaswa kulaumiwa kwa kifo chake.

Sababu kuu ya kifo, walihitimisha, ilikuwa ni kuzidishiwa kwa dozi ya usingizi ambayo daktari alimchoma. Alipoulizwa miaka kadhaa baadae, Daktari alisema kuwa kifo kile kilisababishwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya mgandamizo wa hewa 'air pressure', ndani ya ndege. ( Mwaka 1960 alishiriki tena kama mtaalam wa ganzi, katika tukio la kukamatwa kwa Eichmann huko Argentina).

Watu wa Isser walizipitia karatasi za Israel na kugundua hati za viapo na barua za mapendekezo kutoka kwenye kanisa katoliki huko Jerusalem; baada ya kuuza siri zake kwa wamisri, alipanga kukimbilia America kusini. Kwenye begi lake, majasusi walipata tiketi ya meli kuelekea Brazil. Tatizo lililofuata kwa Isser kukabiliana nalo ilikuwa familia ya Israel. Alipaswa kuwa amemkaribisha Matilda kuja na kumwambia ukweli wote. Ila viongozi wa Mossad, wakiwa wameudhiwa na jinsi habari hii ilivyoishia, waliamua kuizika hii habari na wakapata baraka zote za waziri mkuu Sharett.

Mossad wakavujisha taarifa 'zilizopikwa' kuhusu kapteni Avner Israel kwenye vyombo vya habari. Walidokeza kuwa alitoroka kutoka Israel baada ya kuzidiwa na madeni binafsi na mahusiano ya kimapenzi. Hizi hadithi zikatengeneza vichwa vikubwa vya habari kwenye magazeti.
Kwa miaka mingi, Matilda, kaka wa mume wake, mtoto wake wa kiume, Moshe Israel - Ivor, hawakujua kilichotokea. Waliamini alikuwa akiishi sehemu fulani, labda America kusini. Huu uongo haukua wa kusamehewa.

Kosa la kwanza lililopelekea kushindwa kwa hii misheni ni jinsi walivyomtendea Israel, pamoja na kuwa alikuwa msaliti; kosa la pili ni njama za ukimya, kuondoa jina la Israel kutoka kwenye rekodi za jeshi, na Mossad kumpotosha mke na kaka zake. Rafi Eitan na maofisa kadhaa wa Mossad walipinga kwa nguvu maamuzi ya 'ramsad' kuutupa mwili baharini na kuidanganya familia, ila mikono yao ilikuwa imefungwa. "Dogo Isser alikua Mr. Usalama kipindi hicho", Eitan alituambia.
"Alikuwa mtawala pekee wa taasisi ya ujasusi na jumuia ya kijasusi haikuwahi kutofautiana na maamuzi yake".
Kuchapishwa kwa hii habari, miaka mingi baadae, kunaonyesha jinsi ilivyo ngumu kufuta uwepo wa mtu. Hata baada ya wao kufa, kuna wakati wanaongea na sisi kutoka ndani ya kaburi.

....MWISHO WA SURA YA NNE....

Ila ndio mwanzo wa sura ya tano..
..."AHH, HIYO? NI HOTUBA YA KHRUSHCHEV"...
 
Nawasubiri tuanze sura ya tano...
Kwa wanaoweza , changia MB..
Kama huwezi naomba usinitukane.. kausha tu.
 
Nazitafuta mb kiongozi, penye wengi pana mengi. Watoa miongozo yenye tija na kuleta hoja elekevu za kujadili na WAPUUZI pia wamo kikaoni. Vumilia
 
Officially nakuachia kijiti, malizia mkuu!
Soon mimi nitaanza kitabu kingine na Richard Flanagan - Njia nyembamba kuelekea ndani kabisa ya Kaskazini " The narrow road to the deep North".

Hicho komaa nacho..
Ahahahhaha...nazingua tu ila unatuua na Arosto tatizo. 😅😅😅 we tupiamo vitu tujifunze
 
5. "AHH, HIYO? HIYO NDIO HOTUBA YA KHRUSHCHEV..."

Sehemu ya Kwanza.

Yote yalianza na mahusiano ya kimapenzi.
Katika msimu wa kipupwe wa 1956, Lucia Baranovski alikuwa ameanguka kichwa chini miguu juu kwenye penzi na kijana, mwandishi wa habari, mwenye mvuto, Victor Grayevski. Ndoa yake na makamu wa waziri mkuu wa Poland iliyokuwa ya kijamaa ilikuwa juu ya mawe, na walionana kwa nadra sana ndani ya muda mrefu.

Lucia alifanya kazi kama katibu wa Edward Ochab, katibu mkuu wa chama cha kijamaa cha Poland. Wafanyakazi wake walishazoea ugeni wa huyu Victor mchangamfu kwa mpenzi wake. Kulikuwa hakuna siri juu ya hisia za Lucia kwa huyu kijana. Victor alikuwa mhariri kiongozi wa taasisi ya habari (PAP) huko Poland, iliyosimamia maswala ya Kisovieti na Ulaya ya mashariki. Kiuhalisia alikuwa myahudi, na jina lake la kweli aliitwa Victor Shpilman. Ila miaka kadhaa iliyopita, wakati alipojiunga na hichi chama cha kijamaa, marafiki zake walimtahadharisha kuwa, kwa kutumia jina kama Shpilman asingefika mbali. Hivyo akalibadili kuwa Grayevski, lililozoeleka Poland.

Wakati jeshi la Ujerumani lilipoivamia Poland kwenye vita kuu ya pili ya dunia - WW II, Victor alikuwa mtoto. Familia yake ilifanikiwa kuvuka kwenda Urusi na kidogo tu ikaepuka mauaji ya halaiki. Baada ya Vita, wakarudi Poland. Mwaka 1949, wazazi wa Victor na mdogo wake wa kike wakahamia Israel. Ila huyu Mjamaa mwenye shauku na bidii, alibaki nyuma; alikuwa mfuasi mkubwa wa Stalin, aliyetamaani kusaidia kutengeneza paradiso ya wafanyakazi.

Ila sio marafiki zake na wafanyakazi wenzake, wala hata mpenzi wake, aliyejua kuwa mkato wa tamaa ukianza kukua ndani ya moyo wa kijana huyu mjamaa. Mwaka 1955 alitembelea familia yake huko Israel, na kuona dunia nyingine - huru, yenye maendeleo, taifa la kidemokrasia la kiyahudi, kama ndoto hivi, tofauti kabisa na propaganda za kijamaa alizolishwa.

Aliporudi Poland, akiwa na miaka thelathini (30), Victor alianza kutafakari kuhamia Israel. Asubuhi moja mapema April 1956, Victor akaenda, kama kawaida, kumtembelea mpenzi wa moyo wake katika ofisi ya katibu wa chama. Kwenye kona ya dawati la mpenzi wake, Victor akaona kipeperushi kilichofunikwa na jalada jekundu, kikiwa na namba, na kupigwa mhuri wenye maneno 'Siri Muhimu'. "Hii ni nini?" Victor alimuuliza. "Oh, hiyo ni hotuba tu ya Khrushchev", alijibu kawaida. Victor aliganda kwa baridi. Alishasikia juu ya hotuba ya Khrushchev, ila hakuwahi ...

Itaendelea...
 
Tuendelee...

"AHH, HIYO? HIYO NDIYO HOTUBA YA KHRUSHCHEV.."

Sehemu ya pili.

.... kukutana na mtu yeyote ambaye alikuwa amesikia au kusoma sentensi moja kutoka kwenye hiyo hotuba. Ilikuwa moja kati ya siri zilizohifadhiwa vizuri na kambi ya kijamaa. Victor alikuwa akifahamu kuwa Nikita Khrushchev, katibu mkuu mwenye nguvu sana wa chama cha Kijamaa cha Sovieti, alikuwa ametoa hotuba katika mkutano wa ishirini wa chama ambao ulikuwa umefanyika mwezi wa pili wa mwaka ulioisha kule Kremlin.

February 25, muda kidogo kabla ya saa sita ya usiku, wageni wote wa nchi za nje na viongozi wa vyama vya kijamaa kutoka nchi za nje waliombwa kutoka ukumbini. Saa sita usiku, Khrushchev akapanda kwenye mimbari na akaongea na wajumbe 1,400 wasovieti. Hotuba yake ilisemekana kuwa ya kushtukiza na ya kushtua sana kwa kila aliyekuwepo.

Ila alikuwa amesema nini? Kutokana na mwanahabari mmoja wa Marekani ambaye alituma ripoti ya kwanza magharibi, hotuba ilidumu kwa masaa manne, na Khrushchev alielezea kwa undani jinai za kutisha za mtu aliyeabudiwa na mamilioni ya wajamaa kote ulimwenguni - Stalin.
Khrushchev, minong'ono ilisema, alimtuhumu Stalin kwa mauaji ya halaiki ya mamilioni ya watu. Kuna walionong'ona kuwa wakati wa kusikiliza hiyo hotuba wengi wa wajumbe walilia na kung'oa nywele zao kwa kukata tamaa; baadhi walizimia au walipatwa na shambulio la moyo; kwa uchache watu wawili walijiua baada ya usiku huo.

Ila hakuna hata neno moja juu ya ufunuo wa Khrushchev lililochapishwa kwenye vyombo vya kisovieti vya habari. Minong'ono ikaitawala Moscow, na baadhi ya kurasa za hotuba zilisomwa kwa usiri sana na vyombo vikuu vya chama. Ila maudhui ya hotuba nzima yalilindwa, kama vile ilikuwa siri ya serikali. Wanahabari wa nje walimwambia Victor kuwa taasisi za kijasusi za magharibi ninapangilia juhudi za pamoja kuipata hiyo hotuba. CIA walikuwa wametoa ofa ya dolla millioni moja kama zawadi. Ilikuwa inakisiwa kuwa kuchapishwa kwa hiyo hotuba, katikati ya vita baridi kati ya mataifa ya magharibi na kambi ya kisovieti, ungepelekea tetemeko la kisiasa katika nchi za kijamaa lisilofikirika na kuchochea migongano isiyomithilika.

Mamia ya mamilioni ya wajamaa, ndani na nje ya Urusi, walimwabudu Stalin kikipofu. Uanikwaji ya hizi jinai zake ungeangamiza imani zao na labda hata kusababisha kusambaratika kwa umoja wa kisovieti. Ila juhudi zote za kuipata hotuba zilishindwa. Likabaki kuwa fumbo, karibuni Victor aligundua kwamba Khrushchev aliamua kutuma nakala chache kwa viongozi wa vyama vya ujamaa huko mashariki ya Ulaya, na hivyo ndivyo jinsi hicho kipeperushi kilichofungwa jalada jekundu, kilivyofika kwenye dawati la Lucia.

Wakati Victor Grayevski alipoiona, alipata wazo la kikichaa. Alimuomba Lucia amuazime hiyo hotuba kwa masaa kadhaa, ili akaisome nyumbani, bila kusumbuliwa na purukushani za hapo ofisini. Kwa mshangao, Lucia akakubali. Alikuwa na furaha kumfurahisha Victor..." Unaweza kuichukua", alisema," ila uirudishe kabla ya saa kumi jioni, natakiwa niifungie kwenye 'safe' ". Alipofika nyumbani Victor akaisoma hiyo hotuba. Kiukweli ilikuwa ya kutisha. Khrushchev ali....

Itaendelea....
 
Tuendelee...

"AHH, HIYO? HIYO NDIYO HOTUBA YA KHRUSHCHEV.."

Sehemu ya tatu.

.....kuwa amepasuapasua, bila uoga na bila huruma, hadithi ya imani ya Yosif Vissarionovich Stalin. Khrushchev aliweka wazi kwamba Stalin, katika miaka yake kwenye uongozi, alikuwa ametenda jinai za kinyama na kuamuru mauaji ya mamillioni ya watu. Aliikumbusha hadhira yake kwamba Lenin, baba wa mapinduzi ya Bolshevuk, alishakionya chama dhidi ya Stalin.

Khrushchev alilaani imani kwa nafsi ya mtu ambaye alisifiwa kama, " Jua la mataifa".Akaelezea juu ya uhamisho wa nguvu wa vikundi vya kikabila ndani ya umoja wa kisovieti, uliopelekea vifo visivyo na idadi; juu ya mauaji makubwa ya watu waliodhaniwa kupingana na uongozi wa Stalin (1936 - 1937), ambapo wajamaa millioni 1.5 walikamatwa na laki sita na themanini (680,000) kati yao kuuawa. Kati ya wajumbe 1,966 wa mkutano wa kumi na saba (17) wa chama, kwa amri ya Stalin wajumbe 846 waliuawa, vivyo hivyo pia wagombea 98 kati ya 138 wa ujumbe wa kamati kuu waliuawa.

Khrushchev pia aliongelea njama dhidi ya madaktari, tuhuma zilizopikwa dhidi ya madaktari wa kiyahudi ambao walituhumiwa kula njama ya kumuua Stalin na viongozi wengine wa Kisovieti.
Maneno ya Khrushchev yalimuanika Stalin kama muuaji wa halaiki ya watu, aliyewaua mamilioni ya warusi na watu wa mataifa mengine, wengi wao wakiwa wajamaa watiifu. Ndani ya masaa manne, masiha alikuwa amebadilishwa kuwa shetani.

Hotuba ya Khrushchev iliondoa imani ya uongo aliyokuwa amebakiwa nayo Victor juu ya ujamaa. Na akagundua kwamba, mikononi mwake amekamata bomu ambalo lingeweza kutikisa kambi ya kisovieti mpaka kwenye msingi wake. Aliamua kukirudisha hiki kipeperushi chekundu kwa Lucia. Ila njiani kuelekea kwa Lucia, akapata mawazo mengine, na miguu yake ikampeleka sehemu nyingine - kwenye ubalozi wa Israel.

Akatembea kwa kujiamini, na ukuta wa polisi wa Poland na mawakala wa kijasusi wakampisha na kumuacha apite. Dakika chache baadae, alikuwa ndani ya ofisi ya Yaacov Barmor, kiofisi ni katibu wa kwanza wa ubalozi, ila kiuhalisia, ni mjumbe wa Shabak huko Poland.

Grayevski akampatia kile kipeperushi chekundu. Yule muisrael akakipitia na akapigwa na mshangao. Unaweza kusubiri dakika moja, akauliza, akakichukua kile kipeperushi na kutoka hapo ofisini. Akarudi lisaa limoja baadae. Grayevski aligundua kuwa Barmor alikuwa ametoa nakala za kile kipeperushi, ila hakuuliza swali. Akakichukua, akakificha kwenye koti lake na kuondoka.

Alifika ofisini kwa Lucia kwa wakati, na Lucia akakiweka kwenye 'safe'. Hakuna aliyemsumbua au kumuuliza juu ya safari ya ghafla kwenye ubalozi wa Israel.
Siku ya Ijumaa, April 13, 1956, mapema mchana, Zelig Katz aliingia ofisini kwa mkurugenzi wa Shabak, Amos Manor. Katz alikuwa msaidizi binafsi wa Manor. Makao makuu ya Shabak yaliwekwa katika jengo la kiarabu la kizamani huko Jaffa, karibu na soka la kuvutia la flea. Manor akamuuliza Katz swali la kawaida la kila Ijumaa : "Kuna habari yeyote kutokea mashariki ya Ulaya?"
Ijumaa ndiyo siku ambayo, kontena la kidiplomasia lisilo na ukaguzi, lilileta taarifa kutoka kwa mawakala wa Shabak nyuma ya pazia la chuma.

Itaendelea...
 
Back
Top Bottom