Sasa jamani mwili mmoja unawezaje kuwa na mishahara miwili? Si mwili mmoja macho mawili, sasa nazitolea macho ya kutoka wapi. Ina maana mwili huu una macho manne!
Unajua, wanawake walipoamua kuwasaidia waume zao kwa kufanya kazi na kutafuta pesa kwa ajili ya matumizi madogo madogo, wanaume ndio wakabweteka kabisaaaaaaaaaaaaa. Imefikia wanadai pesa za wake zao, wengine wanadiriki hata kulala tu majumbani na mke ndio atafute na kuhudumia familia, Ukiwaambia wanaaanza maneno ooo mwili mmoja, ooo kama ni hivyo usifanye kazi! nawashangaa sana wanaume.
Tafadhali waume simameni kidete katika wajibu wenu wa kutunza wake zenu na familia. Msiangalie pesa ya mke!lol mimi pesa ya mshahara wangu hamuipati ng'ooooooooooooooo
Unadhani mtu anapoanza kuita jinsia nyingine midudu kutakuwa na hoja hapo? Kila mtu ataanza kuwaka tu. Ila ni kweli inakera, inabidi kujadili hoja na sio kutetea jinsia.
NI KWELI,watu wanatumia lugha za kuumizwa,wanatendwa na wake au waume zao lakini wanajumlisha wanawake au wanaume wote!ni mbaya,hupelekea mijadala kutokuwa na muelekeo sahihi
Unajua, wanawake walipoamua kuwasaidia waume zao kwa kufanya kazi na kutafuta pesa kwa ajili ya matumizi madogo madogo, wanaume ndio wakabweteka kabisaaaaaaaaaaaaa. Imefikia wanadai pesa za wake zao, wengine wanadiriki hata kulala tu majumbani na mke ndio atafute na kuhudumia familia, Ukiwaambia wanaaanza maneno ooo mwili mmoja, ooo kama ni hivyo usifanye kazi! nawashangaa sana wanaume.
Tafadhali waume simameni kidete katika wajibu wenu wa kutunza wake zenu na familia. Msiangalie pesa ya mke!lol mimi pesa ya mshahara wangu hamuipati ng'ooooooooooooooo
mwili mmoja ni imani tu lakini akili tofautini, kusikia tofauti, kuona tofauti, hata kufa tofauti majukumu tofautiSasa jamani mwili mmoja unawezaje kuwa na mishahara miwili? Si mwili mmoja macho mawili, sasa nazitolea macho ya kutoka wapi. Ina maana mwili huu una macho manne!
MadameX,
Naomba ukasome vizuri sheria ya ndoa au omba wataalamu wakusaidie kutafsiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtoto wa nje ya ndoa hawezi kurithi mali ya ndoa labda kama baba kamwandikia urithi kwenye wosia.
Na pia ujue kuwa mali za ndoa ni za mume na mke 50 kwa 50%.
Kwa hiyo hoja zako hapa zimetoka nje kidogo!
Kidini kweli hawarithi, lakini sio sheria ya jamhuri ya muungano wa TZ, nimeshaliona hili watoto wa nje wamerithi.
leo nadhani nimeujua vema msemo wa kiswahili usemao ndoa ni ndoano (Satanic Idea), Nasema hivyo kwasababu moja, kwa wale wakristo na wanaoamini katika ndoa aliyoiunganisha mungu ndoa si ndoano, wala ndoa si pingu za maisha(mstari huo haupo katika maandiko ya biblia wala vitabu vitakatifu) ambavyohutumika kuwaunganisha watu (achilia mbali ndoa za kiserikali na kimila)
Ndoa ni taasisi nyeti iliyoanzishwa na mungu iwe mbaraka kwa wawili waunganao maisha yao yote, alifanya hivyo mungu katika ndoa ya kwanza ya adamu na Eva (mwanzo 2:23-24) Ndoa iliwekwa na Mungu kwa sababu kuwa si vema huyo mtu awe peke yake (Mwanzo 2:18).
sasa katika maisha ya leo, watu wanahisi ndoa ni taasisi za kijamii tu au ndoa ni nyumba ya disko unapolipia unacheza mziki, ukichoka unaondoka, tukiijua maana halisi ya ndoa kama ilivyoanzishwa na mungu mada hii inajibika, rejea tena maandiko hapa kabla sijatoa hitimisho la kuchangia mada
Mwanamume na mwanamke, wakati wameoana wanakuwa mwili mmoja. Huu umoja umedhihirishwa mara nyingi katika biblia. Agano Jipya inaongeza onyo kuhusu umoja huu. Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe (Mathayo 19:6). Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mana yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja (Waefeso 5:31).
Wakati mme Mkristo na mke Mkristo wanaitumia kanuni ya Mungu, ndoa ya Kibibilia hutokea. Ndoa ambayo imeanzishwa kwa misingi ya Bibilia ndio ile ambayo iko wastani, Kristo akiwa kichwa cha mwanamume pamoja na mkewe. Dhana ya kibibilia kuhusu ndoa ni umoja kwa wanandoa ambayo yaleta picha ya umoja kati ya Kristo na Kanisa.
sasa nihitimishe kwa kusema tukijua kuwa ndoa ni umoja na utaratibu na mmekuwa mwili mmoja, vipi mtashindwa kusaidiana majukumu? kwa tafsiri ya biblia alicho nacho mwanaume ni cha mke na kinyume chake ni halisia, si wawili tena, hamtendi katika migawanyiko tena, bali kikiwapo kitu mtafanya kwa uwazi na kama ni mishahara kila mmoja ataujuwa wa mwenzi wake na mtapeana majukumu kulingana na makubalianona kipato chenu na malengo, kwani mwajenga nyumba moja na mtafanya tena katika usawa. kinyume na hapo ndoa hiyo ni uadui tena si aliyoanzisha mungu bali idea ya kishetani, ya ndoa ni ndoano.na kwa mawazo ya ndoa ni ndoano leo ndoa hazidumu na hazina amani
Mishahara yenu! Basi mrudi kwenu mkale mishahara yenu!
Kidini kweli hawarithi, lakini sio sheria ya jamhuri ya muungano wa TZ, nimeshaliona hili watoto wa nje wamerithi.