Mishahara ya Wake Zetu

mishahara ya wake zenu
matumizi
kuosha nywele...3000@wiki
kufanya steaming na dawa20,000 KILA wiki 2
kusuka weaving-150,000@WIKI 2
kuosha miguu.....10,000 KILA WIKI
kutinda nyusi.....2500@KILA WIKI
kubandika kope....10,000@WIKI
kununua chupi mpya kila jmosi at least mbili...10,000
nguo mpya ya kichen party na hereni zake na viatu na mchango.....300,000
zawadi ya shost alojifungua....200,000
ndugu zake
vocha
manguo ,maviatu yalotoka mapya nk:lalala:
 
Last edited by a moderator:
Yake ni yetu, yangu ni yangu lol.....acheni kukimbia majukumu kiaina
 
thubutuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

kichwa cha nyumba kinachong'ang'ania ATM ya mkewe? ukichwa uko wapi hapo?



wewe mie nshajua unachotaka sema...

sasa mie nakwambieni nyote...mwanamke mwema ni yule ambaye wala hana shida na pato lake ...achilia ATM card lazima mwisho wa mwezi ibaki kwa mume.. mwanamke anabaki na kiasi cha mboga na saloon tu..
Ikumbukwe kuwa mme ndio kichwa cha nyumba....

tuacheni tujenge familia.
 
Hahahaha pesa za mkeo wewe mwanaume za nini?hizo ni dalili za kukwepa uwajibikaji..mambo ya kutunza mke na familia ni la kwako aisee acheni kukwepa majukumu nyie wanaume wa dot com

Naona ndoa inakaribia kuitwa ajira sasa. Vigezo na masharti kuzingatiwa..
 
Wakuu,
Hebu na tu shee Experience zenu especialy nyie wenye wake wanaofanya Kazi namna Pato linavyokuwa Distributed Home.
Nataka ku Draw Bonge moja la Conclusion hapa Kwangu

kazi nifanye mimi mshahara umdiskasi nyie akhu!mtuache na mishahara yetu!

ukijua mshara wake wewe ukusaidie nini? kama sio unaa uo, kama akipenda atakuambia mwenyeweeee

huyo mwanamke wewe umemuoa ili umtunze na kumpatia mahitaji yake yote hata kama anafanya kazi. Pesa yake including mshahara ni mali yake na huna mamlaka yoyote juu yake. Ukitaka uanze kujisikia inferior kwa mkeo anza kumtaka mkeo achangie matumizi/mahitaji ya kwenye nyumba yako. Halafu mwanaume kidume kweli haangaiki na pesa ya mke wake!!!!!

mimi kwangu ipo hivi.....pesa zake ni zetu wote.....zangu tunatumia mara moja moja.....

nahisi na mimi nitakuja kuwa kama wewe, now am single seacher


leo nadhani nimeujua vema msemo wa kiswahili usemao ndoa ni ndoano (Satanic Idea), Nasema hivyo kwasababu moja, kwa wale wakristo na wanaoamini katika ndoa aliyoiunganisha mungu ndoa si ndoano, wala ndoa si pingu za maisha(mstari huo haupo katika maandiko ya biblia wala vitabu vitakatifu) ambavyohutumika kuwaunganisha watu (achilia mbali ndoa za kiserikali na kimila)

Ndoa ni taasisi nyeti iliyoanzishwa na mungu iwe mbaraka kwa wawili waunganao maisha yao yote, alifanya hivyo mungu katika ndoa ya kwanza ya adamu na Eva (mwanzo 2:23-24) Ndoa "iliwekwa" na Mungu kwa sababu kuwa "si vema huyo mtu awe peke yake" (Mwanzo 2:18).

sasa katika maisha ya leo, watu wanahisi ndoa ni taasisi za kijamii tu au ndoa ni nyumba ya disko unapolipia unacheza mziki, ukichoka unaondoka, tukiijua maana halisi ya ndoa kama ilivyoanzishwa na mungu mada hii inajibika, rejea tena maandiko hapa kabla sijatoa hitimisho la kuchangia mada

Mwanamume na mwanamke, wakati wameoana wanakuwa "mwili mmoja." Huu umoja umedhihirishwa mara nyingi katika biblia. Agano Jipya inaongeza onyo kuhusu umoja huu. "Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe" (Mathayo 19:6). "Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mana yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja" (Waefeso 5:31).

Wakati mme Mkristo na mke Mkristo wanaitumia kanuni ya Mungu, ndoa ya Kibibilia hutokea. Ndoa ambayo imeanzishwa kwa misingi ya Bibilia ndio ile ambayo iko wastani, Kristo akiwa kichwa cha mwanamume pamoja na mkewe. Dhana ya kibibilia kuhusu ndoa ni umoja kwa wanandoa ambayo yaleta picha ya umoja kati ya Kristo na Kanisa.

sasa nihitimishe kwa kusema tukijua kuwa ndoa ni umoja na utaratibu na mmekuwa mwili mmoja, vipi mtashindwa kusaidiana majukumu? kwa tafsiri ya biblia alicho nacho mwanaume ni cha mke na kinyume chake ni halisia, si wawili tena, hamtendi katika migawanyiko tena, bali kikiwapo kitu mtafanya kwa uwazi na kama ni mishahara kila mmoja ataujuwa wa mwenzi wake na mtapeana majukumu kulingana na makubalianona kipato chenu na malengo, kwani mwajenga nyumba moja na mtafanya tena katika usawa. kinyume na hapo ndoa hiyo ni uadui tena si aliyoanzisha mungu bali idea ya kishetani, ya ndoa ni ndoano.na kwa mawazo ya ndoa ni ndoano leo ndoa hazidumu na hazina amani
 
thubutuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

kichwa cha nyumba kinachong'ang'ania ATM ya mkewe? ukichwa uko wapi hapo?


msome Smile hapo juu...siwezi nikaruhusu hela ya mke wangu ifanye huo upuuzi..
Ilhali mtoto ndo kwanza yupo nursery scholl na kiwanja ndo kwanza nipo hatua ya msingi.. NEVER..

Ikumbukwe kwamba ndoa ni uvumilivu na usistadoo wote unauacha huko ulikotoka...sasa nyie wadada wa kisasa hamkubaliani na hayo ndo maana kila siku mwafungashiwa virago.
 
Last edited by a moderator:
mishahara ya wake zenu
matumizi
kuosha nywele...3000@wiki
kufanya steaming na dawa20,000 KILA wiki 2
kusuka weaving-150,000@WIKI 2
kuosha miguu.....10,000 KILA WIKI
kutinda nyusi.....2500@KILA WIKI
kubandika kope....10,000@WIKI
kununua chupi mpya kila jmosi at least mbili...10,000
nguo mpya ya kichen party na hereni zake na viatu na mchango.....300,000
zawadi ya shost alojifungua....200,000
ndugu zake
vocha
manguo ,maviatu yalotoka mapya nk:lalala:

Ni zaidi ya 961,000/= kwa mwezi! Wangapi wana hata mshahara wa kulingana na hiyo!?
 
Last edited by a moderator:
Yaani mi nawaonea sana huruma walio kwenye ndoa,utakuta mamaa anafanya kazi ila mwanaume ndo anatoa mpaka michango ya kitchen party ambazo hata wahusika hawajui....halafu siku bange zako zikutume kuwa umechoka unataka kum-divorce huyo mwanamke ndo utajua kuwa hapa town kuna wadada wanasheria wanasubiri wavuta bange kama wewe ili na wenyewe waendeshe Spacio zao.

da!!!!!umenivunja mbavu mwenzio!!!!!!!
 
mjengo wa nini huko kwenu wa kaka zako sio but kumbuka wana wake zao na watoto wao...yaani unaacha kujengea wanao unamjengea wifi yako na wanae ...teh

At the end watoto ni warithi, sasa wasiwasi wa nini. Siwezi kwenda kijijini nifikie kwa kaka
 
Wakuu,
Hebu na tu shee Experience zenu especialy nyie wenye wake wanaofanya Kazi namna Pato linavyokuwa Distributed Home.
Nataka ku Draw Bonge moja la Conclusion hapa Kwangu

kila mtu na mshahara wake, lakini mie wake nina access nao, na wiki yote hii ni ATM yake, nikijua tu wamerusha salio fsta nazama, nachukua mkwanja, nachukua kidogo ya kutumia halafu nawasilisha kwa wife. kama nina matumizi ya kifamilia natumia halafu nawasilisha taarifa kwa wife. Yeye kwa upande wa mshahara wangu, wala hata hajawahi kuniuliza napata shilingi ngapi, lakini akiwa na shida akisema tu mgodi wangu unatema kwa M pesa au NMB Mobile. tuko simple. na hawezi niambia nimpe ATM yangu, kwa anajua hatokuta kitu kwa kuwa kila nikifanyacho anakijua. Na kutokana na kuwa busy kulea kijana wetu, wala yeye hataki kujisumbua kwenda benk, yote nimetupiwa mimi.
 
Pesa ya mama watoto inabaki kwake na kama kuna jambo muhimu tunataka kufanya basi tunazungumza na kuona ni namana gani tutalifanya na kama inaonekana kuna nguvu ya kuongeza na uwezo anao basi hapo inawezekana ila mambo ya kuangalia mshahara wa mama mwisho wa mwezi na kufanya kama pato la nyumba si jambo jema sana na linakiuka misingi ya ndoa.
 
mjengo wa nini huko kwenu wa kaka zako sio but kumbuka wana wake zao na watoto wao...yaani unaacha kujengea wanao unamjengea wifi yako na wanae ...teh

hata mimi nashangaa. amejibu hawezi kwenda kwao akafikia kwa kaka yake. Bila shaka ni mchaga huyo, wao nadhani mila zao kila mtu awe na nyumba yake. Sasa tatizo linakuja kwamba iwapo atakufa nyumba ile inakuwa ya familaa yake au inahamishiwa kwa watoto? Na watoto si ndugu wa pale, wana kwao, na wana ndugu zao wa damu. Kwa mama siwezi kwenda kuomba urith hata iweje, kwani undugu wetu ni kwa kupitia mama, sihesabiki kuwa mmoja wa wanafamila kule. labda our differences in cultures determine these issues
 
hata mimi nashangaa. amejibu hawezi kwenda kwao akafikia kwa kaka yake. Bila shaka ni mchaga huyo, wao nadhani mila zao kila mtu awe na nyumba yake. Sasa tatizo linakuja kwamba iwapo atakufa nyumba ile inakuwa ya familaa yake au inahamishiwa kwa watoto? Na watoto si ndugu wa pale, wana kwao, na wana ndugu zao wa damu. Kwa mama siwezi kwenda kuomba urith hata iweje, kwani undugu wetu ni kwa kupitia mama, sihesabiki kuwa mmoja wa wanafamila kule. labda our differences in cultures determine these issues
acha ukabila kila mtu na mawazo yake mimi mwenyewe mchaga
 
Back
Top Bottom