Mishahara ya Wabunge TZ, KE na UG | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara ya Wabunge TZ, KE na UG

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanza Madaso, Dec 7, 2011.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Uganda: 19,000,000 Million Ugsh (12,512,184.99 TZS),190 million shillings (125,552,859.19 TZS) per MP to purchase cars

  Kenya:
  Below is a Kenyan MPs total salary per month

  Basic salary = Sh. 395,000
  A minimum commuted mileage = Sh. 75,000

  Entertainment allowance = Sh. 60,000
  Extraneous allowance = Sh. 30,000

  House allowance = Sh. 70,000

  Monthly car maintenance allowance = Sh. 247,000.

  Gym membership allowance = Sh. 2,000.
  Vehicle fixed cost allowance = Sh. 336,000
  Committee meeting allowance = Sh. 40,000

  Constituency allowance = Sh. 50,000
  TOTAL TAX FREE = Sh. 1,305,000 (23,819,188.69 TZS)

  TANZANIA:
  7 million per Month, office of the legislator are stationeries, water, power and telecommunication and all this costs 735,000/- per month.90 MILLION Shilling per MP to purchase car.Daily sitting allowance of TSh70,000 and per diem of TSh55,000.


  My take:
  Kama tofauti ni kubwa kati ya wabunge wa Tanzania,Kenya na Uganda na ni Tanzania pekee wabunge wanapokea pesa kidogo sana kwa nini wasiongezewe zaidi.Ni halali yao kudai malipo zaidi na kazi zao majimboni ni zaidi ya tunavyofikiria.
   
 2. C

  Claxane Senior Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sio wabunge tu hata watumishi wa serikali punguza ubinafsi
   
 3. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  atuwekee mishahara ya madaktari na waalimu kwa nchi zote.tulinganishe
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii analysis haijakalimilika kwa upande wa Tanzania. Wabunge wa Kenya & Uganda inajulikana how much wanapata kwa mwezi (all inclusive). Hapa kwetu Tanzania mambo hayajanyooka. Yes, wabunge wana basic salary, lakini hizi seating allowances kwa mwizi zinafikia kiasi gani? Hapa ndio kuna wizi wa mchana kweupe. Tukumbuke wabunge wanalipwa hizi seating allowance kwa kila warsha/ mkutano wanayohudhuria. Yaani ni kama mwalimu kulipwa kwa kila kipindi anachofundisha (mbali za mshahara). Akiwa na vipindi vinne kwa siku analipwa kwa kila kipindi.

  Inabidi tukae chini na kujumlisha hizi number ili kupata picha halisi ya malipo wanayopata wabunge wetu. Itashtua wengi.
   
 5. majata

  majata JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  tatizo wewe upeo wako umeishia kuona wabunge tu na vipato vyao!, vp wafanyakazi wa kenya na uganda malipo yao yakoje! Rudi kafanye utafiti huo kisha tuletee tujadili.
   
 6. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Tuletee na mishahara ya watumishi wengine wa hizo nchi ndio tujadili,tatizo la Tanzania ni tofauti kubwa kati ya wabunge na watumishi wengine.
   
 7. M

  Masscom Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  serikalin unafanya kazi kama mtumwa kuanzia asbh hadi jioni. mshahara 250000 hakuna cha safari,launch allowance,transport wala cha house. eti leo mbunge kaongozewa posho kutoka 70000 had 200000. kwan wao tuu ndo maisha yamepanda au? HAKI SAWA KWA WOTE
   
 8. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Acha kuhalalisha wizi kwa simple logic. Tujaribu kuiga yale yaliyo mema. Sio kisa Kenya na Uganda wanawaibia wananchi, basi na kwetu ni ruksa, huo ni utahira.
   
 9. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Angalia na kipato cha nchi husika Kenya hawaishi kwa misaada wanategemea uchumi wao pekee, sio omba omba!!! Wewe uchumi wako ni omba omba unajipandisha mishahara fedha zitatoka wapi, mishahara ya wananchi wako ikoje????????
  Tuliza kichwa fikiri vizuri, acha ushabiki!!!!!!!!!!

   
 10. samito

  samito JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jipange upya. ha2japinga mshahara bali 2napinga alowance, tafuta alowance za ke,ug na tz ulinganishe, hapa wako juu siting laki 2 na vikao kwa siku mbunge anahudhuria zaid ya vitano, bado bahasha za kina jairo.
   
 11. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,773
  Likes Received: 6,105
  Trophy Points: 280
  Ubinafsi juu ya ubinafsi. Sio watumishi wa serikali tu! Serikali inawajibika kuboresha maisha ya wananchi wote bila upendeleo. Inapopandisha "posho" au mishahara ya kundi fulani ni lazima ihakikishe inaboresha pia mapato ya makundi yote au inaweka mazingira bora ya mapato ya makundi mengine kuboreka. Serikali ya aina hii ndio serikali inayojali na sikivu. Hii ni muhimu kwa sababu maisha yanapopanda yanaathiri wote na sio kakikundi fulani tu kama wabunge au "wafanyakazi wa serikali".

  Kwa mfano, nilitegemea kusikia mishahara ya wafanyakazi ikipanda, wakulima, wavuvi, wafugaji, n.k. wanaboreshewa bei za mazao yao, huduma za matibabu katika hospitali za serkali na hasa vijijini zipunguzwe, wazee na walemavu wapate bima za afya na watibiwe bure, na endapo, kwa mfano, mwaka ukiwa mbaya wakulima na wafugaji wawe subsidized na serikali. Kumbuka wafugaji walivyopoteza maelfu ya mifugo mwaka juzi kutokana na ukame lakini serikali ikawa kiziwi kana kwamba hayakuwa yakitokea Tz.

  Kama kweli serikali haina uwezo basi iwe kwa wote na sio kakikundi fulani tu kuneemeka kwa gharama na mateso ya walio wengi. Tena suala la mapato na matumizi ya nchi (keki ya taifa) ni lazima liwe suala la msingi katika katiba mpya badala ya ridhaa ya fulani.
   
 12. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa nini wabunge wa tz wasilipwe TZS 8,292,374.60 kwa siku?
   
 13. Jimbi

  Jimbi JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  we mbunge, acha kutuletea wizi wenu wa magamba hapa
   
 14. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hili suala halina utetezi.Hatuwezi kutetea wizi kwa kigezo cha kulinganisha malipo ya Kenya na Uganda.Katika nchi yenye matatizo lukuki kama yetu ni ushetani kushabikia dhulma inayofanywa na kakikundi ka watu wachache wakati mamilioni ya walipa kodi wanaishi katika lindi la umasikini.
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Umeongea ki layman sana mshahara unategemea uchumi wa nchi husika, uzalishaji, mapato na matumizi ya ndani, miradi ya maendeleo ya kipindi husika, inflation rate, vipaumbele ya kitaifa nk nk, sijui kama hivi vinafanana kwa nchi zote ulizozitaja, lakini sinta kulaum sana kama vipaumbele vyetu ni mishahara mizuri tena kwa wabunge tu.
   
 16. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kakurupuka jtulishalijadili hapa MM aliileta hii mada hapa, ukiangalia gap ya kipato cha watumishi wa umma hasa walimu na wabunge katika hizo nchi
   
 17. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Matokeo ya kupanda kwa mshahara wa wabunge ni haya hapa
  1. kuongezeka kwa ufisadi mdogo mdogo
  2. mgomo baridi; wafanyakazi kwenda kazini lakini kutumia muda mwingi kupiga stori baada ya kufanya kazi ofisini kwetu imeanza hiyo
  3. kuzidi kuchelewa kwa malipo muhimu ya miradi na mishahara kwa watumishi kama ilivyo sasa
  4. kukuza uhasama kati ya serikali na watumishi wake hivyo watumishi/watanzania wataichukia serkali
  5. kuiona hii serikali yetu ni ya kisenge (mod naombausilitoe hilo nenol iache kamalilivyo)
  6. ccm kujiwekakatika ma zingiramagumu zaidi
  7. kuzuga mchakato wa katiba ili wananchi waconcentrate katika posho za wabunge
   
 18. l

  laun Senior Member

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  A great thinker cant make such a poor analysis. You are not a great thinker.
  Umenikumbusha kale ka-msemo ka mwenzako akila m**vi na we utakula. Kwa hiyo tuige kila wanachofanya ke and ug hata kama ni cha kipumbavu,utakuwa ujingaaaa
   
 19. RR

  RR JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  mleta hoja angeweka na za burundi...kwa nini waongeze allowances na sio mishahara?
   
 20. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  So makinda ndo anaona hyo ndo solution! Anawaza nin kwa wale nao wanaopangsha hapo hapo Ddm? Wao wap watapata hyo nyongeza, it means maisha yamepanda kwa wabunge tu? Yan badala ya kutafuta njia ya kuta2a tatzo la m2 wa chin bado 2 wanazd ku2kandamiza, waltakiwa ku2nga sheria itakayomlinda mpangaj kutolpa kod kubwa! Ama kwel 2meingia mkenge! Hawa sio watetez we2 bal wameenda kudai chao!
   
Loading...