Mishahara ya wabunge itathminiwe upya

Princemwalejr

JF-Expert Member
Nov 9, 2017
496
488
Kwanza niseme mimi sina kadi ya chama chochote cha siasa. Ila ni mkereketwa wa bendera ya Tanzania.

Hakuna kitu kinanikera kama tabia ya wabunge kusimamia ya vyama vyao na kusahau ya taifa. Kuna wabunge wazuri sana wa kupinga ufisadi. Lakini hutawasikia wakimzogoa fisadi kama yuko kwenye chama chao.

Kwenye hili la mishahara ni kama wote kwa mpigo bila ya kujali vyama vyao wameamua kulikalia kimya. Katika nchi ambayo polisi mwenye shahada ya sheria analipwa laki sita kwa mwezi hesabu ya kuwalipa wabunge zaidi ya milioni nane kwa mwezi imetoka wapi?

Kuna watumishi wa serikali wako kazini zaidi ya miaka thelathini mishahara yao haijafifikia milioni. Na mafao yao wakistaafu yanaweza yasifikie huo mshahara wa mwaka wa mbunge mmoja.

Wengi wa watanzania wanateseka kwa kukosa bima. Nimeshuhudia waliorudi nyumbani kusubiri kufa kwa kukosa bima. Wabunge wao wana utaratibu wa kutibiwa nje kwa fedha za wavuja jasho.

Hivi kweli utaweza kuwakilisha wenye shida iwapo wewe hujui shida?

Wako wapi wale wabunge wasemaji wazuri hawaoni kuwa mishahara yao imekaa kifisadi? Na bado wanapewa posho za vikao. Hii haijatulia ni ya kukemewa vikali na wakereketwa wa bendera ya Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania
 
Wanahangaika kupunguza wage bills kwa kudhulumu wanyonge, ati ni darasa la saba hana sifa za kuajiri. Huu ni ubaguzi wa dhahiri mfagizi wa ofisi na fomu 4 inasaidiaje utendaji kazi wake. Msukule Msukuma na Mchawi Majimarefu wana zaidi ya daktari mwenye digrii ya Phd, huu ni ufisadi wa kiasi gani?. Tunapumua kwa kutukana maana uvumilivu umefika mwisho!
 
nchi muwape wenyeww sa hv mnaanza kuona mshahara ni mkubwa et.......afu mbona hapo naskia walipunguziwa....

[HASHTAG]#Atubu[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom