Hoja yako ni nzuri, ila tatizo ni sheria aliyoitunga Mkapa Mwaka 1999.
'Political Service Retirement Benefits Act, 1999'; inayohusu pensheni za viongozi wa kisiasa: Rais, Makamu wa Rais, Spika na Naibu wake, Waziri Mkuu.
Chini ya sheria hii mambo yafuatayo yalilifunga Bunge:
1. Ni lazima Bunge lipitie upya viwango vya Pensheni za wakubwa hao kila baada ya miaka mitano kwa lengo la KUZIONGEZA.
2. Kiwango cha pensheni ya Rais mstaafu ni 80% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.
3. Ili kukidhi matakwa ya 1. hapa juu lazima Bunge liongeze mshahara wa Rais aliyepo madarakani.
4. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977; Rais ni sehemu ya Bunge. Hivyo mshahara wake ukiongezwa; chini ya Sheria na 2. ya 1999 mishahara ya wengine waliotajwa hapo juu; pamoja na wabunge, ITAPANDISHWA.
Katika mazingira ya kikatiba na kisheria kama hayo hapo juu; mabadiliko kwenye maeneo kama haya haiwezekani bila kubadili Katiba.