Mishahara ya wabunge itathminiwe upya

Mishahara ya wabunge itathminiwe upya

Maisha hayafanani habadani. Wao hata kiinua mgongo ni kikubwa na wanapewa kwa wakati tofauti na mfanyakazi wa umma anayesota miaka nenda rudi na mafao kidogo tena yakusotea.
 
Kwanza niseme mimi sina kadi ya chama chochote cha siasa. Ila ni mkereketwa wa bendera ya Tanzania.

Hakuna kitu kinanikera kama tabia ya wabunge kusimamia ya vyama vyao na kusahau ya taifa. Kuna wabunge wazuri sana wa kupinga ufisadi. Lakini hutawasikia wakimzogoa fisadi kama yuko kwenye chama chao.

Kwenye hili la mishahara ni kama wote kwa mpigo bila ya kujali vyama vyao wameamua kulikalia kimya. Katika nchi ambayo polisi mwenye shahada ya sheria analipwa laki sita kwa mwezi hesabu ya kuwalipa wabunge zaidi ya milioni nane kwa mwezi imetoka wapi?

Kuna watumishi wa serikali wako kazini zaidi ya miaka thelathini mishahara yao haijafifikia milioni. Na mafao yao wakistaafu yanaweza yasifikie huo mshahara wa mwaka wa mbunge mmoja.

Wengi wa watanzania wanateseka kwa kukosa bima. Nimeshuhudia waliorudi nyumbani kusubiri kufa kwa kukosa bima. Wabunge wao wana utaratibu wa kutibiwa nje kwa fedha za wavuja jasho.

Hivi kweli utaweza kuwakilisha wenye shida iwapo wewe hujui shida?

Wako wapi wale wabunge wasemaji wazuri hawaoni kuwa mishahara yao imekaa kifisadi? Na bado wanapewa posho za vikao. Hii haijatulia ni ya kukemewa vikali na wakereketwa wa bendera ya Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania
Hoja yako ni nzuri, ila tatizo ni sheria aliyoitunga Mkapa Mwaka 1999.

'Political Service Retirement Benefits Act, 1999'; inayohusu pensheni za viongozi wa kisiasa: Rais, Makamu wa Rais, Spika na Naibu wake, Waziri Mkuu.

Chini ya sheria hii mambo yafuatayo yalilifunga Bunge:

1. Ni lazima Bunge lipitie upya viwango vya Pensheni za wakubwa hao kila baada ya miaka mitano kwa lengo la KUZIONGEZA.

2. Kiwango cha pensheni ya Rais mstaafu ni 80% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.

3. Ili kukidhi matakwa ya 1. hapa juu lazima Bunge liongeze mshahara wa Rais aliyepo madarakani.

4. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977; Rais ni sehemu ya Bunge. Hivyo mshahara wake ukiongezwa; chini ya Sheria na 2. ya 1999 mishahara ya wengine waliotajwa hapo juu; pamoja na wabunge, ITAPANDISHWA.

Katika mazingira ya kikatiba na kisheria kama hayo hapo juu; mabadiliko kwenye maeneo kama haya haiwezekani bila kubadili Katiba.
 
Ubunge iwe ni kazi ya kujitolea,ila wapewe posho stahiki wakati wa vikao vya bunge
Sifa ya mbunge iwe Mtanzania mwenye uwezo wa kujitegemea sio wasaka malupulupu kupitia ubunge.
 
Hoja yako ni nzuri, ila tatizo ni sheria aliyoitunga Mkapa Mwaka 1999.

'Political Service Retirement Benefits Act, 1999'; inayohusu pensheni za viongozi wa kisiasa: Rais, Makamu wa Rais, Spika na Naibu wake, Waziri Mkuu.

Chini ya sheria hii mambo yafuatayo yalilifunga Bunge:

1. Ni lazima Bunge lipitie upya viwango vya Pensheni za wakubwa hao kila baada ya miaka mitano kwa lengo la KUZIONGEZA.

2. Kiwango cha pensheni ya Rais mstaafu ni 80% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.

3. Ili kukidhi matakwa ya 1. hapa juu lazima Bunge liongeze mshahara wa Rais aliyepo madarakani.

4. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977; Rais ni sehemu ya Bunge. Hivyo mshahara wake ukiongezwa; chini ya Sheria na 2. ya 1999 mishahara ya wengine waliotajwa hapo juu; pamoja na wabunge, ITAPANDISHWA.

Katika mazingira ya kikatiba na kisheria kama hayo hapo juu; mabadiliko kwenye maeneo kama haya haiwezekani bila kubadili Katiba.
Point tupu
 
Kwani hili bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria bila ya kubadili katiba? Trump kapangua mfumo mzima wa kodi wa Marekani juzi kwa kutumia kura za wabunge, sisi tunashindwa vipi.
 
Watz kwa rohombaya hawajambo, yaani unataka aliye nacho apunguziwe
 
nchii wanasiasa hawapaswi kuchekewa hata kidogo...unakuta mbungeni hana tija yoyote ye kila kitu ndio tu halafu kodi za watanzania zinafujwa tu kweli napendekeza mishaara ya wabunge ingekuwa sawa na madiwani ili tuone wenye uchungu na nchi hii
 
Watz kwa rohombaya hawajambo, yaani unataka aliye nacho apunguziwe

Tuchukulie wabunge 265 kila mmoja akilipwa milioni nane kwa mwezi. Kwa hesabu za haraka haraka serikali inatumia milioni 2120 kila mwezi kuwalipa wabunge. Kwa mwaka serikali inatumia shilingi 25, 440, 000,000. Na bado wanapata posho.

Si bora wakatwe nusu yake itumike kuwaongezea mishahara watumishi wa serikali.
 
Mimi siku zote huwa nasema wanasiasa ni kikundi cha watu wajanja wajanja waliojikusanya sehemu moja kwa kutumia mbinu tofauti tofauti ili kutafuna kodi za wananchi!

Ukitaka kuthibitisha hilo hebu ajitokeze mtu mmojo aguse haya maslahi yao mapana uone jinsi watakavyoungana kumraruararua na kumchanachana bila kujali itikadi za vyama vyao!

Kwenye hili la mishahara mikubwa na maposho manene, hautowajua CCM ni wapi, CHADEMA, CUF, wala NCCR ni wapi.. Wataungana na kumchachafya kwelikweli yule mwenye kujaribu kugusa maslahi yao ya kifedha!

Uadilifu wa wanasiasa wetu, hasa wabunge una mashaka makubwa mno. Mnamkumbuka yule kiongozi aliyejaribu kutajataja wanaohusika na biashara haramu ya uuzaji wa madawa ya kulevya? Mliona tofauti yoyote kati ya wabunge wa CCM na wale wa upinzani?
 
Ukweli mtupu kwenye mishahara na posho wabunge wa CCM=CHADEMA
 
Wanahangaika kupunguza wage bills kwa kudhulumu wanyonge, ati ni darasa la saba hana sifa za kuajiri. Huu ni ubaguzi wa dhahiri mfagizi wa ofisi na fomu 4 inasaidiaje utendaji kazi wake. Msukule Msukuma na Mchawi Majimarefu wana zaidi ya daktari mwenye digrii ya Phd, huu ni ufisadi wa kiasi gani?. Tunapumua kwa kutukana maana uvumilivu umefika mwisho!
Au kama vipi wabunge pia walipwe kulingana na elimu zao. Maana kama Msukuma na Majimarefu anapokea mara tatu ya mtumishi aliye na PhD ya medicine, umuhimu wa elimu hapa haupo.

Ndiyo maana tutaendelea kukatana mapanga wakati wa chaguzi kwasabb siasa ni zaidi ya kila kitu hapa nchini.

Tuamue kama wataz, msianze kusema oooh duniani note wanafanya hivi.
 
Tuchukulie wabunge 265 kila mmoja akilipwa milioni nane kwa mwezi. Kwa hesabu za haraka haraka serikali inatumia milioni 2120 kila mwezi kuwalipa wabunge. Kwa mwaka serikali inatumia shilingi 25, 440, 000,000. Na bado wanapata posho.

Si bora wakatwe nusu yake itumike kuwaongezea mishahara watumishi wa serikali.
Wewe uko tayari kukatwa mashahara wako kwa nusu?
 
Wewe uko tayari kukatwa mashahara wako kwa nusu?

Nimeshawahi kwenda kazini nikaambiwa position yako imefutwa. Kampuni inabana matumizi kutokana na hali ya uchumi. Na haikuwa tabu vile vile. Mzungu anajiliza mimi nilicheka tu nikaishia.
 
Back
Top Bottom