inakupa hasira gani mishahara hiyo ?, most of these CEO's have perfomance based contracts and they negotiate their salaries, this is bcoz of the complexity of the job, magnitude and decision making @ that level,being contract based and renewed on perfomance, remuneration is commisurate(sp) to the risks taken to leave a healthy permanent job
Kama itasaidia wanaJF kulinganisha, mshahara wangu nilipoteuliwa Gavana wa BoT Januari 1966 ulikuwa Shs 60,000 kwa mwaka: yaani Shs 5000 per month.
Rais Mwalimu Nyerere alikuwa analipwa mshahara huo huo.
Lakini ikumbukwe kwamba wakati huo Dola moja ya Merikani ilikuwa sawa na Shs 7.00. Kwa hiyo mshahara wa Gavana ulikuwa US Dollars 712 per month ambao kwa kiwango cha sasa ungekuwa takriban Shs 1.1 milioni.
Rais Nyerere mnamo 1968 aliamua kupunguza mishahara ya viongozi Tanzania, na akapunguza mshahara wake kwa asilimia 10, kufikia Shs 54,000 kwa mwaka. Licha ya kwamba mkataba wangu wa Ugavana ulikuwa unatamka kwamba mshahara wangu hautapunguzwa, nilijitolea nikapunguzwa mshahara ili usizidi wa Mheshimiwa Rais. Kwa hiyo Mshahara wa Gavana kwa mwezi ulikuwa Shs 4'500.
Marupurupu mengine yalijazia mishahara hii, kama vile free housing, watumishi wawili nyumbani, gari pamoja na petroli na dereva.
Ingawa sikumbuki mishahara ya mawaziri wakati huo, ilikuwa chini ya ule wa Rais. Hata nilipoteuliwa Waziri wa Fedha 1977 mishahara ilikuwa midogo na tuliendelea hivyo hivyo hadi Mwalimu alipostaafu; ndipo milipuko hii inayatajwa na wachangiaji wa thread hii ilipoanza.
Kuna sheria iliyotungwa katika enzi za ukweli na uwazi inayokataza kuzungumzia mshahara wa rais, hivyo chukua tahadhari vinginevyo unaweza kupambana na mkono wa sheria.
serikali ina siri kali, never expect them to mention their salaries, only yours 'll b heard, not theirs. Leave it and work on ur biznez.
serikali ina siri kali, never expect them to mention their salaries, only yours 'll b heard, not theirs. Leave it and work on ur biznez.
Nina uhakika wameacha kuzila mkuu wangu.Basi kama unapokea na "zinatumika kuwakomboa Watanzania" kwa nini unalalamika?
Maana unawaambia wabunge wenzako na Watanzania kuwa hizohela zibakie huko, zikalipe walimu na kujenga zahanati lakini wewe mwenyewe unaziondoa huko, unapokea! Unasema unazitumia vizuri, basi endelea kupokea.
Unazitumia kusafiri around the country kuwaelimisha Watanzania, kuwakomboa Watanzania. Ina maana hela ambazo unadhani hutakiwi kuzila, kuzigusa, unazifanya hela zako za matumizi, ni nauli, ni chakula cha njiani, unazichanganya na hela zako zingine. Hicho kitu kinaitwa commingling. Una commingle funds zako na funds ambazo unatuambia huzili, hutakiwi kuzigusa!
Ukitaka kuonyesha a higher degree of ethic and rectitude hebu acha ku commingle hizo hela, mrudishie Sitta. Sasa hivi kina Sitta hawawezi kujisuta moyoni kwa sababu wanaona na wewe unazila! Ukimwambia za kwako unazila na CHADEMA Sitta anakuona kituko!
Na wakati tunaongelea ya Bunge, jana umeulizwa na waandishi kuhusu msimamo wa Mbunge mwenzako Mwakyembe ukajibu swali lakini ulipoulizwa kuhusu Mbunge unaetofautiana nae ukakwepa, ukidai kwamba Zitto anaongoza Kamati ya Bunge, unasubiri ripoti yake. Kwani Mwakyembe haongozi Kamati ya Bunge ya Madini (naibu Mwenyekiti)? Mwakyembe kwani katoa ripoti? Si uli sapoti ya Mwakyembe uliyoyasikia kwenye media na unofficial conversations may be, sasa Zitto ndio kusema hujasikia msimamo wake?
Dr. Slaa, kwa lugha za mtaani tunasema shukuru hao waandishi feki hawawezi kumbana mbavu mwanasiasa.
Heshima Mbele Wakuu,
Jana katika kikao cha wabunge kilichofanyika pale DIIC na kuhudhuliwa na baadhi ya wabunge,waliomba kuongezewa Posho na Mishahara,.
Spika wa bunge ak.a Mzee wa kukanususha 'Vilowassa' alitoa hoja kwa wabunge kwamba waongezee pesa katika bajeti ya bunge ili wao wapate maslahi zaidi,hoja hiyo iliungwa na Mhe. Masilingi na zitto ,ila zitto alissisitiza hilo liambatane na kurudishwa kwa pesa za EPA ili zifanye kazi ya kuendeleza Maendeleo ya Wananchi.
mhe. Massilingi alienda mbali zaidi na kusema inabidi posho iboreshwe ili wasifanye shughuli zingine na wawatumikie wananchi.
Je wakuu mnaona ni haki na bora kwa hawa waheshimiwa waongezee Mishahara??Je posho yao Haitoshi??
Kuna haja ya kuwa na wagombea ambao wanaojitosheleza kama Ndesamburo ili wawatumikie wananchi..sasa nimeanza kuyakumbuka maneno ya Ndesa Pesa wakati akichangia mjadala wa suala la RDC katika kiako nkilichopita cha bunge.
Wabunge wanastaili kuongezewa mishahara zaidi ya wafanyakazi wa Serikali.
Namnukuu Mzelohalisi hapa:
JF,
Mshahara na marupupupu ni milioni 7 kwa mwezi! Bado vikao vya kamati na maslahi mengine!
Kwa mwaka Mbunge hupata Shilingi milioni 84!
Na akimaliza mda wa miaka mitano hupata milioni 30 kama kifuta jasho!
Mwal Msingi hulipwa 150,000 kwa mwezi na kwa mwaka hupata 1,800,000! Hebu angalia tofauti ni shilingi 82,800,000 kwa mwaka!!!
Uwiii !!!!! Jamani hii tofauti kwa nchi maskini ni kubwa mno!!!
Ndo maana rushwa ktk uchaguzi haitaisha!
Hivi Jaji Mkuu, Spika, Raisi na PM kuna mtu ana data wanalipwa kiasi gani tz?
Source: Slaa akiongea Hedaru Bunge mradi wa ulaji
Pia hapa:
note:Villowassa=vimada=kashfa
Hata mimi nilishangazwa. Wenzetu hadi kodi wanazokatwa kwenye hiyo mishahara wanatangaza. Ukitaka kujuwa huu ni ummafia wenyewe.Ni 2011 na bado hakuna anayejua kwa uhakika mkuu wetu wa nchi analipwa mshahara kiasi gani! Hii ni aibu kubwa sana hususan ukizingatia kuwa walipa kodi hela zao ndiyo zinatumika.
Shameful!