1.
Sasa tuko nje ya topic kabisaa, lakini sio tatizo mkuu ndio maana tupo hapa JF ni pamoja na kuitaka serikali yetu ibadili katiba, kwa sababu katiba tuliyonayo imepitwa na wakati, kiongozi wa serikali hawezi kulazimishwa kujiuzulu na chama katika siasa za kisasa za maendeleo,
Halafu haiewezekani sheria iseme mstaafu anatakiwa kusaifiri na wasaidizi wawili, huku tunamuona akisafiri na wasiadizi zaidi ya kumi that is wrong, ndio maana nilisema leteni sheria tukate mzizi wa fitina!
Haya sasa, na katiba nayo imepitwa na wakati! Chama cha siasa kama chama kingine kina haki zote za kumuadhibu na hata kumlazimisha mwanachama wake ajiuzulu kutoka nafasi yeyote kama amepata nafasi hiyo kupitia mgongo wa chama hicho. Chama cha ANC kimemlazimisha Rais wa Afrika ya Kusini kujiuzulu. Nae amekubali kwa sabau hana support katika chama chake. Lakini barua ya kujiuzulu hakumuandikia Mwenyekiti wa Chama chake (Nzuma) bali Spika wa Bunge. Pamoja na kufanya hivyo, angeweza kukataa kujiuzulu na kuki'dare' chama kimfukuze uanachama kwani chama hakikuwa na mandate ya kumfukuza kwenye urais! Mbona Rais Bingu wa Mutharikai wa Malawialikataa kuwa disciplined na chama chake cha UDF na alijitoa na kuanzisha chama chake bila kujiuzulu urais?
Mpaka hapo utakapoweka ushahidi kuwa kweli hao watu zaidi ya kumi wote ni wasaidizi wake ndipo nitakapokubali hoja yako. Zaidi ya hapo ni speculation maana kuongozana na Mkapa si lazima uwe msaidizi wake![/SIZE][/FONT]
2.
Sheria ya mafao mliyoileta inaonyesha ime-expire siku nyingi sana kama haitumiki kabisa, hiyo ndiyo point yangu, kwa sababu haiwezekani wastaafu wote wawe na the same lifestyle, halafu ukasema eti wanai-abuse sheria no way! Haiwezekani ikawa wote toka enzi za Mwalimu!
Unataka kutuambia hata Nyerere alikuwa anaongozana na wapishi na wasaidizi kibao?
Leo unataka kusema Mkapa na Mwinyi na Jumbe na Mwalimu wana'life style' zinazofanana? Au maana ya lifestyle, siielewi? Unahakika gani wao wanategemea mafao yao kama wastaafu kulipia lifestyle yao? Una hakika gani kuwa wake zao ( wafanyabiashara wakubwa) hawalipii hiyo unayoiita lifastyle kama ilivyo kwa McCain?
Sijasema wana abuse sheria. Si lazima wote waliokatika msafara na mstaafu walipiwe na serikali kama sehemu ya stahili ya mstaafu. Sasa kama Mwinyi anaenda Umoja wa Mataifa kuwakilisha serikali katika kongamano ya ukimwi, ulitegemea aende peke yake? Ni lazima ataongozana na watu kutoka foreign, wizara ya Afya na Ofisi ya Waziri Mkuu (TACAIDS). Hawa si sehemu ya stahili yake inayozungumziwa hapa ingawa ukienda kumpokea mizigi airport utaona wote wako nae!
Mkapa yuko kwenye Foundation kadhaa ambazo zinamfanya asafiri kila wakati. Hizi foundation bila shaka zinamlipia gharama zake. Sasa kama huo mkutano anaoenda kuhudhuria kwa niaba ya Foundation yake una mslahi na Tanzania, basi asiongozane na watumishi wa serikali kwa kuhofia kuwa wako watu kama nyinyi mnaohesabu ukubwa wa ujumbe wake?
Mimi sijasema kuwa wana-abuse sheria. Nitasemaje wakati sikubaliani na wewe kuwa hiyo lifestyle unayodai inalipiwa yote kutokana na mafao yao ya ustaafu? Pamoja na hayo, unashangaa nini kuambia kiongozi ana abuse sheria? Mara hii umesahau Richmond na Buzwagi?
3.
Bwa! ha! ha! ha! haijawahi kutokea eti mstaafu kuwalipia wasaidizi wake nauli na kila kitu kwenda majuu na kurudi? Never! Wote hulipiwa na serikali bro!
Umeona wapi hilo? Wewe si unawaona tu wanapoingia na kutoka airport! Au unakuwa nao wanapoomba madurufu ya safari? Unahakika gani kwamba hawa wote wanalipiwa kutoka katika 'vote' ya wastaafu?Unajua lakini utaratibu wa kusafiri serikalini?
3.
Hawawezi kuwa wlaikuwa wanamuonea aibu Mwalimu, maana angewauliza pale pale, otherwise noana finally unakubali argument yangu kuwa sheria na ninachokiona ni tofauti, kabisaaa sasa either haipo, imekufa, au ilisha expire.
Ahsante.