Mishahara serikalini kulipwa dirishani

Ni issue ambayo ni ngumu kutimiza. Ni janja ya kuchelewesha mishahara ya watu. Mf. Watu wengi wana mikopo bank, unadhani wataikatia dirishani!
Kama wafanyakazi hawapo kwenye vituo vyao vya kazi, wanadhani ni vigumu kwa mfanyakazi kusafiri na kufuata mshahara wake popote?
 
Bongo kweli noma, watu wanaenda na technology, lakini bongo wanarudi nyuma zama za kale. gud luck guys
 
Ni issue ambayo ni ngumu kutimiza. Ni janja ya kuchelewesha mishahara ya watu. Mf. Watu wengi wana mikopo bank, unadhani wataikatia dirishani!
Kama wafanyakazi hawapo kwenye vituo vyao vya kazi, wanadhani ni vigumu kwa mfanyakazi kusafiri na kufuata mshahara wake popote?

Hii inaonyesha viongozi kwenye wizara/tume husikakuwa ama wameachwa na teknologia au wameachwa na uzalendo au vyote pamoja.
 
Huu ni upuuzi tena ujinga,ukosefu wa akili.maarifa,kutojiamini,kwani idara husika inafanya kazi gani?basi wameshindwa kazi
kuna wafanyakazi wengi wapo masomoni,sasa nani atawachukulia salary zao?
 
Ni issue ambayo ni ngumu kutimiza. Ni janja ya kuchelewesha mishahara ya watu. Mf. Watu wengi wana mikopo bank, unadhani wataikatia dirishani!
Kama wafanyakazi hawapo kwenye vituo vyao vya kazi, wanadhani ni vigumu kwa mfanyakazi kusafiri na kufuata mshahara wake popote?

mjiandae kununua bastola for self defence
 
Huu ni upuuzi tena ujinga,ukosefu wa akili.maarifa,kutojiamini,kwani idara husika inafanya kazi gani?basi wameshindwa kazi<br />
kuna wafanyakazi wengi wapo masomoni,sasa nani atawachukulia salary zao?
<br />
<br />

Vumilia kaka!!! Hawana njia ingine ya kuhakiki wapokea mishahara hewa!
 
hahahah
serikali ya CCM na mishahara dirishana,huko tulishasahau siku nyingi sana na haiwezekani iwe ndiyo njia ya kuwabaini ambao hawapo au marehemu

jamani wataaluma wa ICT toeni msaada kwa wizara husika maana hali ni mbaya kwao kuhusu utandawazi
 
Jamani wana JF,
Naombeni mnisaidie labda mimi ndio sijaelewa kauli ya waziri wa utumishi mhe.Hawa Ghasia alipokuwa kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria alipokuwa akijibu maswali/maoni ya baadhi ya wabunge;eti serikali inajiaandaa kuanza utaratibu wa kuwalipa wafanyakazi wa serikali mishahara kupitia dirishani

Soma hapa, angalia mistari ya mwisho hapo kwenye RED

Mbunge amwambia Waziri Mkurugenzi hafai

Imeandikwa na Shadrack Sagati;
Tarehe: 24th February, 2011


MBUNGE wa Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), amemshitaki Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke, Steven Kongwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, akidai ni mtu ambaye hana uwezo wa kiutendaji wa kuongoza manispaa hiyo.

Akichangia katika taarifa ya Waziri Ghasia wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala jana Dar es Salaam, Mtemvu alidai kutokana na uwezo mdogo wa mkurugenzi huyo, manispaa ya Temeke imerudi nyuma kimaendeleo.


Alisema, kuna miradi inayotekelezwa katika manispaa hiyo, lakini mkurugenzi huyo hajishughulishi kwenda kushuhudia, jambo ambalo alisema mfano huo unaonesha namna mkurugenzi huyo asivyo na sifa za kuongoza manispaa kubwa kama hiyo ya Temeke.


Kongwa aliteuliwa kushika wadhifa huo baada ya kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Iddi Nyundo. Mtemvu alisema wananchi wa Temeke wanamkumbuka Nyundo kwani chini ya uongozi wake, Temeke ilipiga hatua kubwa kimaendeleo.


Akijibu hoja hiyo, Ghasia alisema wabunge wanapokuwa na malalamiko yenye ushahidi juu ya utendaji mbovu wa watendaji kwenye halmashauri ni vyema wapeleke kwenye ofisi yake ili hatua zichukuliwe.


Kuhusu suala hilo la Mkurugenzi wa Temeke, Ghasia alisema wananchi wa Temeke wenyewe wana uwezo wa kumkataa mtendaji yeyote katika halmashauri hiyo kama wataona hawafai.


"Kwa mfumo wa sasa hivi wa utumishi wa umma, wananchi wenyewe wana mamlaka ya kumkataa mkurugenzi huyo sio lazima suala hilo lifikishwe utumishi," alisema Ghasia.


Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM) alilalamikia hatua ya baadhi ya halmashauri kuwanyima ruhusa walimu kwenda kujiendeleza, akidai uamuzi huo unawafanya walimu wasiwe na ari ya kufundisha.


Alisema ana mifano ya walimu ambao wameamua kwenda kujisomesha kwa gharama zao, lakini halmashauri zinawazuia hivyo akataka kupata mwongozo kutoka kwa waziri huyo.


Mbunge wa Manyoni Magharibi, Paul Lwanji (CCM), alitaka kufahamu Serikali inavyoshughulikia tatizo la watumishi hewa na kuhoji sababu ya kuwepo watumishi hao wakati tayari kuna sensa ilishafanywa miaka ya nyuma.


Akijibu hoja za wabunge hao, Ghasia alisema walimu kwenda kusoma, kwa sasa Serikali imeweka utaratibu kuwa wakajiendeleze kwa kufuata utaratibu uliopo na sio kila mtu kujigharamia na kwa muda anaotaka.


Alisema utaratibu uliopo ni walimu wanaruhusiwa kwenda kujiendeleza kufuatana na uzoefu kazini kwamba aliyetangulia kazini ndiye anapewa kipaumbele kwanza.


Alisema iwapo walimu wataruhusiwa kila mtu akajiendeleze shule zitaendelea kukumbwa na ukosefu wa walimu.


Kuhusu watumishi hewa, alisema kwa sasa kila taasisi ya Serikali inasafisha benki yake ya takwimu ili kujiridhisha kuwa fedha wanazoomba za mishahara ya bajeti ijayo ni kwa watumishi walioko kazini tu.


Alisema baada utaratibu huo kukamilika, Serikali itaandaa malipo ya mishahara ya watumishi kupitia dirishani, jambo ambalo linaweza kutekelezwa ndani ya miezi miwili ijayo.

"Kwa sasa tunaendelea na maandalizi kwani ni suala ambalo linahitaji fedha," alisema Ghasia.
 
Kitendo cha kuwalipa watumishi wa serikali mishahara dirishani ni kuwaongezea usumbufu tu. Si zani kama kuna mtumishi yeyote anayeunga mkono utaratibu huo. Labda Pa-diem ziwepo zakutosha.
 
Kurudi tena katika utaratibu wa zamani wa kulipa dirishani haitapunguza wafanyakazi hewa. Ukweli ni kwamba serikali kuu ie hazina inahaha kulipa mishahara ya civil servants. Sasa kwa kutumia utaratibu wa zamani wa kulipa dirishani wana-buy time na instead of tarehe 20 na kitu mishahara inalipwa wiki ya kwanza ya mwezi baada ya ukusanyaji wa kodi.
 
Mishahara dirishani ni njia za "Old Stone Age" za eti kuthibiti mishahara hewa!
 
Sasa kwanini watz turudi nyuma kwenye enzi za mwl.?wakati wenzetu katika nchi zilizoendelea/zinazoendelea watu hawatembei na cash kwenda sokoni/hotelini n.k. badala yake watu wanatembea na kati ya benki tu,hii si itakuwa tunaikana sc.&techno.?ikumbukwe kuwa hapo awali wakati watu wanalipwa dirishani mishahara ya watumishi ilikuwa inaibiwa kwenye vituo na sababu nyingine na ikaipelekea serikali kuamua kubadili utaratibu na watu wakaanza kulipwa kupitia benki.Hata hivyo tukumbuke kuwa kuna vibaka/wezi/majambazi ambao wakijua kuwa watumishi wa kituo X wanalipwa sasa hivi hawakawii kukaa barabarani na kuwateka.
 
Wanataka majambazi yaanze shughuli zao kwa kuvamia cashiers wanapotoka benki kuchukua hiyo mishahara na kwenye ofisi za kulipia. Amesahau kipindi kile walipochukua mamilioni ya mishahara ya Polisi pale Kituo cha Polisi Msimbazi?


Tatizo la Tanzania kila kiongozi anapoingia madarakani anakuja na wazo lake!!!!
 
Kama kawaida

Majibu rahisi kwa maswali magumu. Sawa nilivyowahi kumsikia mbunge mmoja akisema kwamba dawa kukomesha uchakachuaji wa mafuta ya petrol ni kuongeza kodi kwenye mafuta ya taa ili ilingane na petrol. Nikajiuliza bibi yangu kule kijijini amekosa nini hadi apandishiwe bei ya mafuta ya taa kwa kosa la wengine. Technology to answer that ipo ni kuyawekea marker ie rangi mafuta ya taa, petrol, diasel etc Migodi yote ya dhahabu wanafanya hivyo.

Wafanyakazi wengi wa serikali sasa hivi tunalipwa mishahara yetu moja kwa moja toka hazina. Kama ni wafanyakazi hewa basi pesa hizo zinaliwa hapohapo hazina.

Pili, sijui huyu Hawa Ghasia alikuwa na maana gani anaposema "kulipwa dirishani" Yaani wafanyakazi wote wa serikali Tanzania twende Dar Es Salaam kila mwisho wa mwezi kupanaga foleni ili tulipwe mishahara yetu? What is the cost items of time and money to achieve that?
 
Back
Top Bottom