Mishahara serikalini kulipwa dirishani

Jamani wana JF,
Naombeni mnisaidie labda mimi ndio sijaelewa kauli ya waziri wa utumishi mhe.Hawa Ghasia alipokuwa kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria alipokuwa akijibu maswali/maoni ya baadhi ya wabunge;eti serikali inajiaandaa kuanza utaratibu wa kuwalipa wafanyakazi wa serikali mishahara kupitia dirishani

Labda ni
1. Anatania tu,
2. Anatikisa kiberiti au
3. Ni mawazo yake binafsi.
Hao ndio vioo ngozi wetu!
 
anamanisha kwa muda wa mwezi mmoja fixed, ili kana kwamba wanafanya sensa ya watumishi kupitia malipo ya dirishani mmoja baada ya mwingine!!!!!!!!! Yaani yeye kama waziri na idara zake za umma hajajua idadi halisi ya watumishi wa umma-kwamba wapo na watumishi hewa!! sensa ya mwaka juzi ilikuwa ya bure kwa maana hiyo.
 
Wanataka majambazi yaanze shughuli zao kwa kuvamia cashiers wanapotoka benki kuchukua hiyo mishahara na kwenye ofisi za kulipia. Amesahau kipindi kile walipochukua mamilioni ya mishahara ya Polisi pale Kituo cha Polisi Msimbazi?


Tatizo la Tanzania kila kiongozi anapoingia madarakani anakuja na wazo lake!!!!

Hilo nalo neno! Maana tatizo kubwa la kulipwa cash money ni uporaji! Hata mfanyakazi anapoondoka dirishani na kurudi ofisini au nyumbani vibaka wanaweza kumvizia na kumpora mshahara wote! Uporaji huu unawezekana hata katika maeneo ya ATM lakini huwezi kuibiwa mshahara wote, labda kiasi kile ulichotoa kutoka mashine.
Kwa kweli tunazidi kutia aibu! Serikali hii inatufanya watanzania wote tunaonekana washamba!
 
Kwa kweli tunazidi kutia aibu! Serikali hii inatufanya watanzania wote tunaonekana washamba! mimi nazani kama habari za Tanzania huwa zinaonekana nje ya nchi wanaweza kufikiri tanzania ni kamkoa kako nchini kenya kwa jinsi viongozi wake wasivyo makini
 
Tatizo la wafanyakazi hewa ni madhara yakutokuwa na proper legal enforcement, yaani wezi wanaiba na wanahakika ya kuendelea kutesa kwani risk ya kufanya hilo kosa ni dogo...Ebu serikali iwaadhibu hao wahujumu uchumi kwa sampling tu ya haraka haraka katika idara na taasisi chache kama watu hawatawajibika! Tatizo la higher transaction costs ni tatizo la low social capital na dwa huwa ni heavy punishment kwa law offenders mpaka after a time inabadilika from practice na kuwa culture....Waziri anatibu symptoms na kuacha ungonjwa.
 
Tanzania ndio ina-collapse hivyo .....! Mnashangaa nini!

Ukweli ni kwamba serikali hii imefilisika na sasa inatafuta njia ya kuchelewesha malipo halali ya watu, hivi sasa hawana kitu hazina wanahaha hata kuwalipa watu kiinua mgongo chao baada ya kustaafu!! Mkwere nchi imemshinda anajikaza kiume tu kuogopa aibu!!
 
Mimi ninadhani serikali haipo makini katika hili, halina sababu ya kusumbua wafanyakazi kupokea mshahara dirishani kwa sababu kila ofisi ina toa mahudhurio kazini ya kila siku. Kwa namnahiyo basi tujue serikali yetu haina watendaji inaendeshwa kwa kubahatisha. Hapa bila kuadhiri usumbufu wa wafanyakazi kusumbuana na serikali wapitie madaftari yanayopelekwa manispaa na sehemu nyingine za mahudhurio. Hii hali ya kupokea mshahara dirishani ina madhara yake hasa walimu.
 
Kweli huyo waziri kichaa anataka kuturudisha henzi ya zamani pumbavu zake

Aliye karibu na Hawa Ghasia, amwambie aniajiri mimi kwa mkataba maalumu niwabaini watumishi hewa wote bila kutumia mtindo wa kizamani wa kulipa kupitishia dirishani. Hii ni kazi ndogo sana. Inakuwa ngumu kwao kwa sababu ya ufisadi wa viongozi katika idara yake ya utumishi.
 
sishangai waziri mwenyewe ni zilipendwa hata mawazo yake ni zilipendwa pia.
 
maendeleo ya kurudi nyuma nayo pia ni maendeleo vilevile!! Kaazi kwelikweli!
 
Kuna elimu anayokosa huyu dada Ghasia, maana wataalam wa mishahara wanasema kulipa mishahara dirishani ndio wizi mkubwa wa mishara ufayika, na pia uleta mishahara hewa; mshahara kwa njia ya benki haina mwanya wa mishahara hewa kama njia ya dirisha, mi nakataa katukatu, kumfungulia mtumishi akaunti na kuindesha inahusisha watu wengi kiasi kwamba kuwa na mtu hewa ni ngumu kuliko kulipia dirishani ambapo ni suala la mhasibu na huyo mtu hewa.
 
Baada ya kushindwa kuchukua hela yetu kupitia dowans sasa wanataka kuanzisha kikundi cha mafia ili kiwe na kazi ya kupora mishahara ya idara mbalimbali za serikali.
Haingii akilini waziri mzima na akili yake asione ubora wa mfumo uliopo na kuanza kuongea utumbo bungeni huu ni uhayawani.
Hatuhitaji mtaalam mwenye shahada yoyote kuweza kuuona ubora wa mfumo uliopo wa kuchukulia pesa benki na kulazimisha wafanyakazi wote siku ya mshahara waache kazi na kwenda kuanza kumsubiria cashier ili alipe mishahara, badala ya mfumo wa sasa ambapo benk kila mtu anakwenda kwa wakati wake hata baada ya saa za kazi.
Tunatakiwa tumfundishe waziri wetu huyu jinsi ya kufikiri na hasa kufikiri makini kabla ya kuropoka!
 
Wana JF,
Jana nimepata kusoma e-mail iliyosambazwa kwa wakuu wa vituo vya kaz kuwa waambie watumishi wao kuwa mshahara utalipwa kwa hundi na hivyo kila mtumishi awepo kituoni cku hiyo ya malipo.

1. LENGO- kuwahesabu watumishi halali na kuwaondoa watumishi hewa.

2. MAKOSA
-watu wanaenda likizo
-hawajasema lini watalipa
-walio masomoni wanadai warudi, hawajasema kama watalipiwa nauli.

NAWASILISHA
 
Katika kuhakikisha kuwa serilkali inaondokana na tatizo la watumishi hewa serikali imedhamiria kulipa mishahara ya watumishi
kupitia dirishani kuanzia mwezi huu.Je,ni njia sahihi ya kubaini watumishi hewa?
 
......hata sisi wafanyakazi feki tutaenda kuwachukulia mishahara wahasibu kwa kutumia vitambulisho feki......
 
Yah mimi binafsi naona kuwa hili linaweza kuwa jambo la msingi sana kwani litapunguza kulipa watu hewa lkn kama kawaida ya watanzania wengine wao wanawaza namna ya kuila hiyo hela itakayobaki, kwa hivyo watakachokifanya hapa ni kwamba wahasibu ndio watakaokula hiyo hela, wao wanajua watailaje watacheza dills na wakubwa wengine na watu watashangaa kusikia tena kuwa bado mishahara mingi imeliwa
 
Back
Top Bottom