Mishahara serikalini kulipwa dirishani

Mishahara serikalini kulipwa dirishani

Dowans nayo ilipwe dirishani. Kwani dirisha lina nini? Watanzania tu wajinga kabisa.

kweli mkuu. KAGODA,IPTL NA DOWANS nao ni watumishi hewa,walipwe dirishani vingnevo itakuwa ni discrimation among employees!
 
SERIKALI imetangaza kuwalipa watumishi wa umma mishahara yao kupitia madirishani kwa muda wa miezi miwili.

Katika kipindi hicho, itachukua hadhari zote ikiwamo ya kuhakikisha hakutokei uporaji mishahara hiyo ili kuwagundua watumishi hewa wanaotafuna fedha za umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, alisema hayo juzi mjini hapa kwenye mafunzo ya maboresho ya utumishi wa umma awamu ya pili.

“Utaratibu wa kuwalipa watumishi madirishani utakuwa wa muda tu, angalau miezi miwili tu. Nia ni tuwatambue, tusiowaona, tutawaondoa kabisa,” alisema Ghasia.

Alisema, ulipaji huo wa mishahara utawezesha kugundua watumishi hewa na kutolea mfano wa uhakiki uliofanywa katika shule za sekondari, ambako moja ilielezwa kuwa ina walimu 17, lakini ikakutwa na walimu wawili na nyingine walimu 70, lakini ukweli ilikuwa na walimu 20.

Kuhusu uboreshaji wa maslahi ya watumishi ikiwamo mishahara, alisema Serikali itaendelea kuiboresha kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.

Akiwa kwenye mafunzo hayo, Ghasia aliwataka watendaji wa halmashauri kusimamia vema fedha ili kuondoa mawazo kuwa halmashauri zimejaa wezi.

Kuhusu ajira, alisema kuanzia sasa mtu atakayefaulu usaili wa kazi katika utumishi wa umma na kupangiwa kituo cha kazi, hataitwa tena katika usaili wa kazi yoyote serikalini.

Alisema hiyo ina nia ya kukabiliana na watu ambao wanapewa kazi, lakini wanakwenda kuripoti vituoni na kuchukua fedha za kujikimu, kisha kutoweka.

Waziri Ghasia yuko katika ziara ya mafunzo kuhusu mabadiliko ya utumishi wa umma awamu ya pili na jana alitarajiwa kuwa Misenyi.

uMENEMA MAMA KAZA BUTI KUGUNDUA WAFANYAKAZI HEWA. ILA UNATAKIWA UWE MAKINI SANA NA KUCHUKULIANA MISHAHARA KWANI WANAOKULA KISOGO NI HAO HAO.
 
this still is "the removing of cobweb instead of killing the spider"pesa wanachukua wenyewe kwa ajili ya kampeni za ccm,..after all si vigumu kumjua anayekula heal za mishahara hewa,...
 
nimeiweka hii habari ili nijue je ni njia sahaha ya kubaini wafanyakazi hewa?kwasababu miaka kama 4 iliyopita wafanyakazi walikua wanachukulia dirishani na bado kulikua na wafanyakazi hewa kibao

Mkulu
Heshima mbele,nakubaliana na wewe kwa asilimia 100.Tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele, hivi kweli tumeshindwa kubuni njia mpya ya kubaini watumishi hewa kuliko kurudi kwenye njia za zamani ambazo ndizo zilikuwa chanzo kikubwa cha watumishi hewa.Unapofanya maamuzi kama yaha,you need to consider ukubwa wa serikali kwa sasa kwa maana ya number ya watumishi,serikali imeajiri watumishi wengi mno kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita ,kitu ambacho binafsi sina shida na hilo kwani ililenga kuboresha huduma kwa umma.

Kulipa dirishani ni ku-create mkanganyiko zaidi, my take ni kwamba zoezi zima halita-yield results wanazotegemea kwani ni watu wa zamani au wenye mawazo ya kizamani waliopendekeza njia hii ya kizamani.

KIPI KINGEFANYIKA:
Serikali ilianza vizuri kupitisha mishahara benki,controls zilizopo benki are much more stronger than those wanazopendekeza, ni suala la kutoa maagizo kwa wakuu wa idara na taasisi za serikali kuwasilisha physical stock ya watumishi waliopo kwenye vituo, then you compare payrol, stock list na account zinazotumika kulipia hiyo mishahara, zoezi hili likiwashirikisha branch managers wa mabenki husika, then you get the variance ambayo lazima ipo.

Utaratibu huu unakuwa unaufanya periodically.

Wakati mwingine ukiona watu wanafanya maamuzi kama haya unapata picha ni watu wa aina gani tulionao ...
 
Kwa hiyo mtu asipojihudhurisha dirishani ndio anageuka mfanyakazi hewa? ina maana kila bosi hajui watu wake?

Nchi hii kweli imejaa vituko na vilaza!
 
Huyu binti Hawa uwezo wake ni mdogo sana. yaani baada ya kuondoa tatizo ndo wanaongeza tatizo. Hili suaala lilikuwa ni la kukaa la wakurugenzi na maafisa utumishi kulimaliza kwa kuwa wanazorekodi zote. lakini tatizo serikali ya mkwere imejaa wizi kwa hiyo ni yale yale. Naona wahasibu wa halmashauri wanapiga vigeregere maana paja la kuku limerudi kinywani mwao baada ya muda kadhaa kuondolewa.
 
hili dili nyieee ngoja msikie ka mishahara haitaibiwa.....
 
mawazo ya huyu mama yapo miaka kumi kabla,amabayo ni hatari zaidi kwani hata majambazi yanaweza kukomba hela zote

Jamani walio karibu wamsaidie haiwezekani kulipa kwenye dirisha iwe ndiyo njia ya kubaini ambao hawapo

na hii inadhihirisha kuwa hata wizara haijui ina wafanyakazi wangapi kwa secta zote za serikali

Tumia hata huu ushauri wa Wayne
Serikali ilianza vizuri kupitisha mishahara benki,controls zilizopo benki are much more stronger than those wanazopendekeza, ni suala la kutoa maagizo kwa wakuu wa idara na taasisi za serikali kuwasilisha physical stock ya watumishi waliopo kwenye vituo, then you compare payrol, stock list na account zinazotumika kulipia hiyo mishahara, zoezi hili likiwashirikisha branch managers wa mabenki husika, then you get the variance ambayo lazima ipo.
 
mwenye cv yake atupe tafadhali. naona kama hamnazo vile na pia kaota usiku ndo kaamua kutangaza hili jambo nadhani IQ yake sawa na zero
 
hivi huyu mama ana akili timamu kweli? Wao ndo wezi wakubwa wa hizo hela za serikali wanazodai wanazilinda.
 
Kweli kuna watumishi hewa kuna ofisi kibao zinalipa watumishi tunazijua eg NIMR,BRELA,KILIMO,
 
mawazo ya huyu mama yapo miaka kumi kabla,amabayo ni hatari zaidi kwani hata majambazi yanaweza kukomba hela zote

Jamani walio karibu wamsaidie haiwezekani kulipa kwenye dirisha iwe ndiyo njia ya kubaini ambao hawapo

na hii inadhihirisha kuwa hata wizara haijui ina wafanyakazi wangapi kwa secta zote za serikali

Tumia hata huu ushauri wa Wayne
Serikali ilianza vizuri kupitisha mishahara benki,controls zilizopo benki are much more stronger than those wanazopendekeza, ni suala la kutoa maagizo kwa wakuu wa idara na taasisi za serikali kuwasilisha physical stock ya watumishi waliopo kwenye vituo, then you compare payrol, stock list na account zinazotumika kulipia hiyo mishahara, zoezi hili likiwashirikisha branch managers wa mabenki husika, then you get the variance ambayo lazima ipo.

Mkulu
Heshima mbele, sasa ndugu yangu hata kunibonyezea thanx muheshimiwa...ah ndugu yangu siyo mambo mkulu..LOL
 
Jamani Jamani ....... Hivi hii nchi ina wasomi ama ina MAJUHA.... kwelil mwl julius akifufuka ghafla atazimia na kufa kama nchi akiikuta imeharibika hivi.

kwanza hapo watalipwa wafanyakazi baada ya hapo change yote inapigwa mfukoni kwani ni mara ngapi signature bandia zinapigwa na cash inachukuliwa.
 
mwenye cv yake atupe tafadhali. naona kama hamnazo vile na pia kaota usiku ndo kaamua kutangaza hili jambo nadhani IQ yake sawa na zero

alisoma Masters ya SUA around mwaka 2000 i think
 
Mkulu
Heshima mbele,nakubaliana na wewe kwa asilimia 100.Tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele, hivi kweli tumeshindwa kubuni njia mpya ya kubaini watumishi hewa kuliko kurudi kwenye njia za zamani ambazo ndizo zilikuwa chanzo kikubwa cha watumishi hewa.Unapofanya maamuzi kama yaha,you need to consider ukubwa wa serikali kwa sasa kwa maana ya number ya watumishi,serikali imeajiri watumishi wengi mno kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita ,kitu ambacho binafsi sina shida na hilo kwani ililenga kuboresha huduma kwa umma.

Kulipa dirishani ni ku-create mkanganyiko zaidi, my take ni kwamba zoezi zima halita-yield results wanazotegemea kwani ni watu wa zamani au wenye mawazo ya kizamani waliopendekeza njia hii ya kizamani.

KIPI KINGEFANYIKA:
Serikali ilianza vizuri kupitisha mishahara benki,controls zilizopo benki are much more stronger than those wanazopendekeza, ni suala la kutoa maagizo kwa wakuu wa idara na taasisi za serikali kuwasilisha physical stock ya watumishi waliopo kwenye vituo, then you compare payrol, stock list na account zinazotumika kulipia hiyo mishahara, zoezi hili likiwashirikisha branch managers wa mabenki husika, then you get the variance ambayo lazima ipo.

Utaratibu huu unakuwa unaufanya periodically.

Wakati mwingine ukiona watu wanafanya maamuzi kama haya unapata picha ni watu wa aina gani tulionao ...

naunga mkono ushauri wako, ningekuwa na email yake ningemtumia
 
Kwani anaelipa hapo dirishani ni MALAIKA au ni wale wale? not a strong reason, wanaoiba salaries si wafanyakazi wa chini, ni wao wenyewe na hao hao ndio watakua wanatoa pesa hapo dirishani, sasa utegemee nini? je wale walimu watakaosafiri toka mbali kwenda halmashauri watarudishiwa nauli? na hili linafanyika lini? si waseme kua hawna pesa? no i strongly disagree with Ghasia, na sie tuone mishahara yao na marupurupu yao! pambaf
 
Yaani hii ndo solution ya Waziri na washauri wake wote Tanzania bwana raha sana unajiamria tu unachotaka
 
serikali ya awamu hii imeanza vibaya mikosi kibao na ukilaza
 
Wa ndg, nimesikia kuwa kuanzia mwezi huu wa Februari 2011, watumishi wa serikali watapokelea mishahara yao dirishani, kisha kutambua waajiriwa halali! Najiuliza maswali yafuatayo:
(1) Ukipokelea dirishani, inasaidiaje kujua nani hayupo? Kani kama mtu hajaja kuchukua mshahara wake, si anaweza kusainiwa tu na anayegawa pesa dirishani?
(2) Tumejiandaaje, kuwadhibiti wale wasiowaaminifu, au je, tunajuaje kuwa watakaowagawia mishahara watakuwa waaminifu, kwamba wasigushi shahihi?

Mimi nilishani kupitia benki, ni rahisi kujua nani mzima na nani kafariki au hayupo, (a) asipokuje mwenyewe, yaani anayestahiri kupata mshahara, mshahara utabaki benki. (b) ikitokea mtu mwingine akachukua kadi ya mtu aliyefariki, ni rahisi kumwona hata kwenye picha ya kwenye ATM, sasa hii ya kupokelea dirishani, mbona siielewi? Au ni janja tu?

Naomba kueleimishwa jamani!
 
Back
Top Bottom