Mishahara serikalini kulipwa dirishani

sasa ndio na-confirm kabisa hata kura zetu hazikuhesabiwa kisahihi... kama hata payroll kitu ambacho unamonitor every month unashindwa kukiamini, utawezaje kuamini a one-off electronic system ya kuhesabu kura?

Hivi kweli tumefikia hatua ya kutojua nani yuko wapi ndani ya nchi yetu, tutawezaje kutambua wairan walio hapa isivyo halali?

Kama walishindwa kulinda amari ya arusha iliyokua haivamiwi na kuua raia, tuna uhakika gani hawa polisi hawataua watu wengine kwa kisingizio cha kulina mali?

Hivi kama staff yupo nje ya nchi kimasomo au ana long leave ya zaidi ya miezi miwili, au hata yupo kwenye short course ya miezi mitatu wata-capture vipi?

Tanzania inadidimia...
 
Hii ni kuhatarisha usalama wa hizo pesa,ni rahisi kuziteka kama benki tu wanavamiwa na mjambazi wakati nje kuna askari na silaha masaa 24.hiyo sio njia sahihi ya kutatua tatizo bali ni kuongezaja tatizo
 
Alisema, ulipaji huo wa mishahara utawezesha kugundua watumishi hewa na kutolea mfano wa uhakiki uliofanywa katika shule za sekondari, ambako moja ilielezwa kuwa ina walimu 17, lakini ikakutwa na walimu wawili na nyingine walimu 70, lakini ukweli ilikuwa na walimu 20. .
Kulipia mishahara dirishani wala siyo suluhisho, ili mradi waliweza kufanya uhakiki katika baadhi ya maeneo. Nadhani hicho ndicho kilichotakiwa kufanywa kwa nchi nzima na hilo linawezekana. Kila mwajiri atakiwe kuhakiki idadi ya watumishi alionao then kuwe na utaratibu wa kila mkuu wa sehemu kutoa taarifa za wafanyakazi kwa mwajiri kila mwezi. Hii itasaidia walau kuwa na taarifa zinazokaribiana na ukweli.
 
Ndiko tulikiofika hapa, badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma.Hizi ndizo gharama za ukosefu wa maadili na uadilifu.Huko nyuma hatukuwa hivi.Kwa sasa yako mengi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wapya kama waalimu huko vijijini kukosa mishahara kwa mwaka au zaidiza.Tunajiuliza kwa teknolojia iliyopo ,iweje hali hiyo ijitokeze
 
Kazi ipo kweli, sasa tulioko mbali itakuwaje? Si ndo wataleta matatizo mengine ya kulaza familia za watu njaa! kwa kweli hili limenigusa mojakwa moja na limenifedhehesha sana. Yetu masikio na macho.
 
na kuna wafanyakazi wapo mashuleni ina maana waache shule warudi kuchukua mshahara then waende tena vyuoni?mie sielewi hii serikali yaani miaka mingi sana wamelipa watu kupitia madirishani na bado kulikua na wizi sana kuliko hata sasa sijui wanachotafuta nini naona kama wanachezea pesa tu maana mishahara inaweza kutekwa au wafanyakazi wanaweza kutekwa wakiwa na mishahara na kisha kunyanganywa

Asante maana kuna watu wako nje ya nchi kimasomo yaani wanataka watu wasafiri kuja kufata mishahara yao? Yaani nchi yetu bwana vichekesho kwakweli!!!
 
Inaweza kusahidia! unajua serikalini kuna wafanyakazi wanacheque No. mbili bila wao kujua?!! Aisee acha sasa hivi kila mtu Tanzania ni MWIZI!
 
Suluhisho la enzi za ujima hili na wala halitasaidia, wanipe mimi hiyo wizara mwezi mmoja tu waone kazi!
 
bila shaka huyo waziri ulimshuhudia wewe mwenyewe je alikuambia ni miezi ipi hiyo ya kufanya zoezi hilo?
 
Hilo ni wazo lake binafsi. Cdhan kama amepata maon kutoka kwa wenzake. Dirishani!? Kazi ipo
 
Mmmmmhh ndiyo maana nasema shule ya watanzania sijui ikoje... yaani hiyo mtu anaona ndiyo mbinu mbadala aliyoigundua. Ameshindwa kabisa kuhakiki kwa kutumia technologia. Nakumbuka wakati nafanya kazi Serikalini tuliambiwa eti hatuwezi kuchukulia mshahara benki kwa sababu tutatumia muda mwingi kufuata mshahara badala ya kufanya kazi.
 
Dowans nayo ilipwe dirishani. Kwani dirisha lina nini? Watanzania tu wajinga kabisa.
 
Mmmmmhh ndiyo maana nasema shule ya watanzania sijui ikoje... yaani hiyo mtu anaona ndiyo mbinu mbadala aliyoigundua. Ameshindwa kabisa kuhakiki kwa kutumia technologia. Nakumbuka wakati nafanya kazi Serikalini tuliambiwa eti hatuwezi kuchukulia mshahara benki kwa sababu tutatumia muda mwingi kufuata mshahara badala ya kufanya kazi.

mwanangu hayo yalikua mawazo dhaifu sana ya viongozi wetu sijui ujinga huu ulikua unatoka wapi!
 
sijui ujinga huu ulikua unatoka wapi!

haukuwa ujinga bwana mdogo, teknolojia ya bongo ilikuwa benki ni manual tu, kila kitu kinaandikwa na kusomwa kisha kupitishwa kwa mtu mmoja, minimum benki ilikuwa ni shughuli ya saa zima hasa ikiwa ulikuwa una draw, hata wafanya kazi by then ungewauliza wapewe chao dirishani au uwawekee benki wangekuambia tupe chetu.Kwa mliozaliwa wakati wa kompyuta hamuwezi kuelewa kabisa kama kunawakati mtu ilimbidi asubiri pesa zake benki kwa masaa matatu kwa kuwa kuna mtu ana balance akaunti yake.
 
Jamani msiongee mengi, huo mshahara tu wa January hadi ninavyoandika msg hii, haujawa deposited kwny deposit Ac ili bank waweze ku-disburse kwny AC za watumishi katika bank husika. Wamefanya mbwebwe za kuleta payroll na salary slip lakin hd sasa hawajatuma hyo mishahara. Nanivyofkri hy mbinu ya kulipa dirishani ni kufanya delay janja ili ionekane nature ya payment method ndo tatizo. Amini usiamini hzo fedha ztafika designation area late kwa visingzio kede ili kumbe wanasubri makusanyo kutoka vyanzo vya mapato ambvyo kimsingi vinatasilisha mapato kwa nyakati tofauti!
 
Jamani msiongee mengi, huo mshahara tu wa January hadi ninavyoandika msg hii, haujawa deposited kwny deposit Ac ili bank waweze ku-disburse kwny AC za watumishi katika bank husika. Wamefanya mbwebwe za kuleta payroll na salary slip lakin hd sasa hawajatuma hyo mishahara. Nanivyofkri hy mbinu ya kulipa dirishani ni kufanya delay janja ili ionekane nature ya payment method ndo tatizo. Amini usiamini hzo fedha ztafika designation area late kwa visingzio kede ili kumbe wanasubri makusanyo kutoka vyanzo vya mapato ambvyo kimsingi vinatasilisha mapato kwa nyakati tofauti!


Serikali imeanza maandalizi ya kulipa wafanyakazi wapya mishahara kupitia madirishani badala ya benki, ili kukabiliana na watumishi hewa.

Akikaririwa na chanzo chetu akifafanua ishu hiyo nzima Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, alisema malipo hayo kupitia dirishani yatafanywa kwa kipindi cha miezi miwili ya kwanza kwa mwajiriwa mpya.

“Sasa tunafanya maandalizi ya kulipa mishahara dirishani kwa watumishi wapya katika miezi miwili ya kwanza, ili kuepuka watumishi hewa, kwani tumeshaona mtu anaripoti akiona mshahara umekaa sawa anaondoka na anaendelea kupata mshahara,” alisema Ghasia.

Alisema katika uhakiki uliofanywa na Serikali, walibaini Sh bilioni 7.56 zililipwa kwa watumishi hewa katika kipindi cha miaka minne ambapo kiasi hicho cha fedha kililipa watumishi 2,950.
 
Ujinga mtupu. Kipindi kile tulikuwa tunachukua dirishani pale Magomeni mbona watumishi hewa walikuwa kibao! Alete tu aone tutakavyozipiga na hataamini macho yake. Yaani anashindwa kujua wafanyakazi hewa kati ya hawa 350,000 tu?
 
Kama si usanii basi ni Ulaji tu! Utasikia gari ya Nmb no.xxx imetekwa msituni Biharamulo na pesa ya mshahara imeibiwa yote mil.700. Ktk tukio hamna jambazi aliyekamatwa. Baadae utasikia papaxxx amewagawia wasanii wa twanga pale Diamond Jubilee!
 
Back
Top Bottom