Mishahara serikalini kulipwa dirishani

Katika kuhakikisha kuwa serilkali inaondokana na tatizo la watumishi hewa serikali imedhamiria kulipa mishahara ya watumishi
kupitia dirishani kuanzia mwezi huu.Je,ni njia sahihi ya kubaini watumishi hewa?[/QUOTE

Kikwete nae achukulie mshahara dirishani kwani na ni mtumishi hewa(NEC appointee)
 
Katika kuhakikisha kuwa serilkali inaondokana na tatizo la watumishi hewa serikali imedhamiria kulipa mishahara ya watumishi
kupitia dirishani kuanzia mwezi huu.Je,ni njia sahihi ya kubaini watumishi hewa?
Halfcaste, kwanza sio kweli kuwa serikali sasa ndio imeamua kulipia mishahara madirishani kuanzia mwezi huu, bali hili ni zoezi la kawaida ambalo hufanyika japo mara moja kwa mwaka/miaka 2 etc kwa serikali kulipia mishahara madirishani ili maofisa masuhuli, (accounting officers) wajiridhishe kwa kuwahakiki watumishi wao. Baada ya uhakiki, utaratibu wa kawaida huendelea!.

Hata hivyo watumishi walio katika extensions mbalimbali ambako ndiko hewa kubwa huwepo, wataendelea kupelekewa fedha huko walipo!.

Dawa ya watumishi hewa ndio hiyo iko jokoni ikimalizia kuchemka, ni vitambulisho vya taifa!.
 
Katika kuhakikisha kuwa serilkali inaondokana na tatizo la watumishi hewa serikali imedhamiria kulipa mishahara ya watumishi kupitia dirishani kuanzia mwezi huu.Je,ni njia sahihi ya kubaini watumishi hewa?

Huu ni upuuzi mtupu tena kuiba mshahara kwa dirishani ni rahisi kuliko benki, Pia hii njia italeta usumbufu mkubwa kwa watumishi kwa mfano mtumishi ambaye yuko likizo bukoba na anafanya kazi dar inabidi aache likizo afuate mshahara tu, mtumishi ambaye yuko masomoni anapataje huo mshahara? Mtumishi iliyelazwa hospitali mbali na kituo chake cha kazi inakuwaje?
 
Mimi ni Mhasibu Serikalini, kwa uamuzi huu serikali imekula kwao maana kama kawaida yetu malipo yoyote yanayobaki ambayo beneficiary wake hawajatokea huwa tunasaini sisi wenyewe kwa kutumia Mkono wa Kushoto! Unaangalia jina kwenye Pay List linasomekaje then unatafuta saini inayoendana na jina hilo kwa kutumia mkono wa kushoto!
 
maana ya watumishi hewa ni ipi?,mbona serikali inatia aibu?,inamaana hao watumishi hewa wako chini ya idara gani?,hawana mkuu wa idara na akajua taarifa zao?,mi nacho jua , wahasibu mara nyingi ndio huwa na majina yao feki wanayo yatumia kukwapua hela kila mwisho wa mwezi,hao ndo wa kubanwa na sio kutusumbua sisi wengine ambao tuko likizo,wengine masomoni na ni mbali sana na vituo vya kazi...
 
Nakumbuka kipindi serikali inabadili mfumo wa kuwatoa walimu wa sekondari kwa katibu mkuu moe na kuwaleta katika halmashauri,kulikuwa na majina mengi sana ambayo yalipo pelekwa katika halmashauri,hayakujulikana ni wakina nani,na wakaendele a kuyaandalia mishahara kila mwezi,hayo majina yalikuwa ni feki toka kwa wahasibu wa wizara ya elimu,waliyaandalia taarifa za uongo kwa kusingizia mikoa fulani na kujikwapulia mahela kila mwisho wa mwezi,lieni na wahasi na sio na watumishi...
 
nchi yetu nzuri, rais bomu,uongozi bomu,yani kila siku ni ngojera za serikali tu. Na bado mpaka 2014 tutaona mengi sana.
 
...sijui wafanyakazi hewa ni nani. Mbona kama ni mimi narudi huko wanakojua mi ni hewa kubeba mshahara wangu na kurudi.
 
Yah mimi binafsi naona kuwa hili linaweza kuwa jambo la msingi sana kwani litapunguza kulipa watu hewa lkn kama kawaida ya watanzania wengine wao wanawaza namna ya kuila hiyo hela itakayobaki, kwa hivyo watakachokifanya hapa ni kwamba wahasibu ndio watakaokula hiyo hela, wao wanajua watailaje watacheza dills na wakubwa wengine na watu watashangaa kusikia tena kuwa bado mishahara mingi imeliwa

Just look at the turth of the matter;
1) Nani atakayewalipa hao wafanyakazi dirishani?
2) Nani anayetengeneza pay roll hewa?

Is not it one and the same person?

This is wastage of time.
 
Nakumbuka kipindi serikali inabadili mfumo wa kuwatoa walimu wa sekondari kwa katibu mkuu moe na kuwaleta katika halmashauri,kulikuwa na majina mengi sana ambayo yalipo pelekwa katika halmashauri,hayakujulikana ni wakina nani,na wakaendele a kuyaandalia mishahara kila mwezi,hayo majina yalikuwa ni feki toka kwa wahasibu wa wizara ya elimu,waliyaandalia taarifa za uongo kwa kusingizia mikoa fulani na kujikwapulia mahela kila mwisho wa mwezi,lieni na wahasi na sio na watumishi...

This is very true. Ni kuleta usumbufu wa hali ya juu kwa wafanya kazi. Shida ni kwua systems is low and almost collapsed. A well functioning system will easily recognise bogus empoyee. There is no need of wasting time and resources.
 
Mimi ni Mhasibu Serikalini, kwa uamuzi huu serikali imekula kwao maana kama kawaida yetu malipo yoyote yanayobaki ambayo beneficiary wake hawajatokea huwa tunasaini sisi wenyewe kwa kutumia Mkono wa Kushoto! Unaangalia jina kwenye Pay List linasomekaje then unatafuta saini inayoendana na jina hilo kwa kutumia mkono wa kushoto!

Pamoja na hii tip, bado serikali imelala?
 
Huu ni upuuzi mtupu tena kuiba mshahara kwa dirishani ni rahisi kuliko benki, Pia hii njia italeta usumbufu mkubwa kwa watumishi kwa mfano mtumishi ambaye yuko likizo bukoba na anafanya kazi dar inabidi aache likizo afuate mshahara tu, mtumishi ambaye yuko masomoni anapataje huo mshahara? Mtumishi iliyelazwa hospitali mbali na kituo chake cha kazi inakuwaje?

Ndio maana nasema, the whiole system is callapsing.......
 
Katika kuhakikisha kuwa serilkali inaondokana na tatizo la watumishi hewa serikali imedhamiria kulipa mishahara ya watumishi
kupitia dirishani kuanzia mwezi huu.Je,ni njia sahihi ya kubaini watumishi hewa?

Yaani kulipia mishahara dirishani ndiyo umekuwa ukomo wa serikali kufikiria njisi ya kudhibiti watumishi hewa?!

Kwa fikiri hizi, serikali imewapa mtaji majambazi. Mishahara mingi itaporwa njiani wakati ikienda
madirishani kulipa wafanyakazi. Karne hii ya technology bado serikali inategemea physical means to
account of his employees. Kweli sisi ni zaidi ya Banana republic
 
wanakumbuka kubadili utaratibu baada ya kufulia,hata hivyo itakua ngumu kwani kuna watu wana pata pesa nyingi itakua risk
 
Watumishi hewa wanapatikanaje? Katika mfumo wa taasisi yeyote kuna kurugenzi, idara na vitengo vyote vikiwa na wakuu wake; kusema kwamba kuna wafanyakazi hewa inamaanisha wakuuu wa vitengo, idara na kurugenzi hawajui watumishi walio chini yao?

Naweza kusema jibu ni HAPANA; kila mkuu wa kitengo au idara ya taasisi ya umma anafahamu watumishi walio chini yao hivyo swala la kuwepo watumishi hewa ni "syndicate" pengine kuanzia huko mishahara inakotengenezewa yaani hazina mpaka inakokwenda kulipwa. Iweje kampuni binafsi zenye wafanyakazi zaidi ya 1000 wasiwe na wafanyakazi hewa iwe tuu serikalini?
 
I wish they could ask and work on it!
Ni uzembe tgu uliokithiri.
There is no excuse.
 
Back
Top Bottom