Mishahara juu, kupanda Julai kwenye bajeti

Mishahara juu, kupanda Julai kwenye bajeti

Mwaka jana ongezeko kwa watu walio kwenye tax band ya juu (zaidi ya Shs. 720,000) kwa mwezi ilikuwa Shs. 4,900 kwa mwezi! Tafakari!!!, ccifweero
Lengo la ongezeko hilo dogo kwa vigogo ni kuondoa gape kubw kati ya wafanyakazi wa ngaxi za juu, kati na wa chini..
 
Lengo la ongezeko hilo dogo kwa vigogo ni kuondoa gape kubw kati ya wafanyakazi wa ngaxi za juu, kati na wa chini..

Ifweero,
Ongezeko kwa July 2013 lilikuwa 1,900 na hiyo ya 4,900 lilikuwa la July 2012. Na kumbuka kiasi hicho ni kwa kila level ya mshahara! Uwe unakula 720,000 au 170,000 nyote unapata kinacho itwa unafuu wa Shilingi za kitanzania elfu moja mia tisa tu.
 
Ifweero,
Ongezeko kwa July 2013 lilikuwa 1,900 na hiyo ya 4,900 lilikuwa la July 2012. Na kumbuka kiasi hicho ni kwa kila level ya mshahara! Uwe unakula 720,000 au 170,000 nyote unapata kinacho itwa unafuu wa Shilingi za kitanzania elfu moja mia tisa tu.

angalia watu wakukaa b kupoteza muda wako kuwaelewesha
 
WATU WENGINE BWANA!? Hivi hamjaridhika na maneno na mbwembwe za Mh Rais JMK? Mbaya zaidi mnaanza kupamba magazeti yenu hata bila kuomba ufafanuzi wa ongezeko kwa tarakimu (asilimia ngapi) na uthibitisho wa maneno yake majukwaani!

Mnachekelea na kufurahia maneno tu ya kisanii??!

Mwaka 2010 PAYE ilipungua kwa Tzs 7,500
Mwaka 2011 PAYE hakubadilika
Mwaka 2012 alisema kwa madaha kuwa kodi itapungua PAYE ikashuka kwa Tzs 4,900 nikajiuliza hili ndilo lililo tangazwa kwa mbwembwe zote zile?

Mwaka 2013, kwa mbwembwe zile zile PAYE kwa MASIKITIKO MAKUBWA ikapungua kwa Tzs 1,900 TU bila kujali nani analipa kodi kiasi gani kulingana na mshahara wake??! Hivi Mfanyakazi kupunguzia Tshs 1,900 kwa mwezi kuna muongezea ahueni ganiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii????????????????????????????????????????????????????????????????

Kwa mtiririko huo wa kuendelea kupungua kwa kiwango kinacho tolewa na Serikali sikivu badala ya kupanda, mfano mwaka 2010 PAYE ilishuka kwa 7,500; ilitakiwa kiwango cha PAYE kipungue (kwa maana ya kuongezeka kwa mshahara wa mfanyakazi) tuseme 2012 kiwe Tsh 10,000 ; na mwaka 2013 kiwe mfn 15,000!

Sina hata wasiwasi record ya Mwaka 2014 PAYE itapungua kwa Tsh 900! Tuwe wa kweli punguzo la Tshs 7,500; 4,500; 1,900 lina weza kuonyesha unafuu wowote katika kuendesha maisha ya miaka hii?

Halafu pia, kwa nini Serikali sikivu isipunguze PAYE kwa kuzingatia asilimia badala ya viwango ambavyo ni constant kwa kila level ya PAYE formula??? Na kwa nini kama kweli Serikali ina nia ya (hata isiyofikia dhati)kumuondelea adha mfanyakazi kwa nini kiasi cha PAYE kisiongezeke kama nilivyo toa mfano hapo juu badala ya kupungua kila mara kwa maana ya kuwa PAYE ikipungua kwa kiasi kikubwa kiasi hicho hicho ndicho kinacho ongezeka kwenye mshahara wa mfanyakazi kwa kila mwezi?

Napendekeza UNAFUU WA KULIPA KODI (kupungua kwa kodi) PAYE uendane na viwango vya mishahara kama ilivyo formula yenyewe ya PAYE na kiwe ni kiasi ambacho kina uhalisia wa kuwa nafuu haswa!

Wakati wanashusha PAYE kisanii kuna dubwana linaloitwa mfumuko wa bei na gharama za maisha so the impact will virtually become zero.
 
Ndg mtukufu sorry Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete,

Unapopunguza kodi katika mishahara kwa wafanya kazi ili viwango vya mishara yao vipande, kisha unapandisha kodi katika vitu / bidhaa muhimu, hapo unadhani umetoa unafuu kwa huyo punda mlipa kodi au ni usanii?

PAYE yangu inaniuma ujue!!? Inazidi hata NSSF/PPPF?

Kuna report ilishawahi kutolewa ikionyesha kuwa kiasi cha fedha kinachotokana na kodi (PAYE) inayotolewa na wafanyakazi katika sekta ya madini ni kikubwa kuliko fedha inayokusanywa kutoka kodi inayotkana na shughuli za za uzalishaji na uendeshaji wa makampuni katika sekata ya madini. Hii maana yake ni kuwa wafanyakazi wa sekta husika wanachangia sana pato la taifa kuliko kodi inayokusanywa kutoka makampuni yanayofanya kazi katika sekta husika. Kwa mwendo huo kweli tutafika?

Walio wengi ama kwa kujua au kutokujua wanachekelea na kufurahia maneno ya majukwwani yanayotolewa kila mwaka!

Tafakuli #1
Mwaka 2010 PAYE ilipungua kwa Tzs 7,500; Mwaka 2011 PAYE hakubadilika
Mwaka 2012 alisema kwa madaha kuwa kodi itapungua PAYE ikashuka kwa Tzs 4,900 nikajiuliza hili ndilo lililo tangazwa kwa mbwembwe zote zile?

Mwaka 2013, kwa mbwembwe zile zile PAYE kwa MASIKITIKO MAKUBWA ikapungua kwa Tzs 1,900 TU bila kujali nani analipa kodi kiasi gani kulingana na mshahara wake??! Hivi Mfanyakazi kupunguzia Tshs 1,900 kwa mwezi kuna muongezea ahueni gani?

Kwa mtiririko huo wa kuendelea kupungua kwa kiwango kinacho tolewa na Serikali sikivu badala ya kupanda, mfano mwaka 2010 PAYE ilishuka kwa 7,500; ilitakiwa kiwango cha PAYE kipungue (kwa maana ya kuongezeka kwa mshahara wa mfanyakazi) tuseme 2012 kiwe Tsh 10,000 ; na mwaka 2013 kiwe mfn 15,000!

Sina hata wasiwasi record ya Mwaka 2014 PAYE itapungua kwa Tsh 900! Tuwe wa kweli punguzo la Tshs 7,500; 4,500; 1,900 lina weza kuonyesha unafuu wowote katika kuendesha maisha ya miaka hii?

(NOTE: Ongezeko au unafuu wa kiasi tajwa hapa juu hakijalishi mtu anapokea mshahara kiasi gani kiwe kima cha chini au cha juu wote wana pokea unafuu sawa)

Tafakuli #2
Kwa nini Serikali sikivu isipunguze PAYE kwa kuzingatia asilimia badala ya viwango ambavyo ni constant kwa kila level ya PAYE formula? Na kwa nini kama kweli Serikali ina nia ya (hata isiyofikia dhati)kumuondelea adha mfanyakazi kwa nini kiasi cha PAYE kisiongezeke kama nilivyo toa mfano hapo juu badala ya kupungua kila mara kwa maana ya kuwa PAYE ikipungua kwa kiasi kikubwa kiasi hicho hicho ndicho kinacho ongezeka kwenye mshahara wa mfanyakazi kwa kila mwezi?

Napendekeza UNAFUU WA KULIPA KODI (kupungua kwa kodi) PAYE uendane na viwango vya mishahara kama ilivyo formula yenyewe ya PAYE na kiwe ni kiasi ambacho kina uhalisia wa kuwa nafuu haswa!

Tafakuli #3
Serikali kuongeza kwa mshahara kwa kiasi cha Tshs 1,900 (PAYE imepungua kwa kiasi hicho) kwa mwezi na kuongeza kodi x dufu katika huduma muhimu mfano mafuta ya taa, petrol, diesel, soda (mwaka huu bei inapaa x3), na huduma nyingine, kuna leta unafuu gani kwa mfanyakazi au mkulima???? Akili kweli tunayo? Kama tunayo tuna dhamila hata isiyo ya kweli? Tuna amini katika maisha halisi ya Mtanzania wa kawaida? Tunalenga kumwezesha mtanzania kutoka hapo alipo kupiga hatua walau hata 1 mbele kiuchumi (nasikia @ anatakia kujiletea maendeleo yeye mwenyewe)?

JMK " akili ya kuambiwa changanya/ongezea na ya kwako" JMK bonge la Entertainer!!
 
Ifweero,
Ongezeko kwa July 2013 lilikuwa 1,900 na hiyo ya 4,900 lilikuwa la July 2012. Na kumbuka kiasi hicho ni kwa kila level ya mshahara! Uwe unakula 720,000 au 170,000 nyote unapata kinacho itwa unafuu wa Shilingi za kitanzania elfu moja mia tisa tu.
eeh,mkuu hiyo inaitwa kugawana kidogo kilichopo.
 
Hakuna cha neema wala nini. Ni nini kimeongezeka leo kwenye huu uchumi mpaka serikali iweze kuwapa neema wafanya kazi? Kuongeza mishahara na huku unapandisha kodi kwa bidhaa muhimu kama mafuta n.k unakuwa umefanya nini sasa? ni heri usingeongeza huo mshahara na kodi zikabaki palepale. Uchumi ukikua ndio uongeze mishahara. kama uchumu haujakua na ukaongeza mishahara ni kusababisha tu inflation, na kupunguza thamani ya shillingi. Km kweli wanataka watu wapate nafuu na neema km inavyoshadidiwa na hilo gazeti hebu waongeze mishahara halafu wasiongeze kodi kwenye bidhaa hasa mafuta ya petrol na bidhaa nyingine muhimu tuone kam kweli wamedhamiria. Otherwise hicho ni kiinimacho kingine kama hiki cha muungano.
 
Mi nashangaa watu wanamshangilia na mambo yake ya kisanii. Ina maana mpaka sasa rais hajui ni asilimia ngapi ya punguzo la PAYE na ongezeko la mshahara lililopo katika bajeti ya wizara ya utumishi? kazi? Ni wazi anajua ni asilimia ngapi lakini hakuzisema ili asije akaharibu mudi ya mazuzu yaliyokuwa yanashangilia usanii wake. Kimsingi ni peanut na haitakuwa nan nafuu yoyote kwa mfanyakazi. Kwani ni nin kilichoongezeka kwenye uchumi tofauti na mwaka jana hadi wafanyakazii wapate nafuu?
 
Badala ya kuongeza mishahara Serikali ingedhibiti bei ya bidhaa na huduma! Haina maana kuniongeza elfu 50 kwenye mshahara wakati ada ya mtoto inapandishwa kwa elfu 50, nauli ya daladala inapanda, na bidhaa zinapanda. Nikipiga hesabu ya maisha kwa mwezi mshahara umepanda kwa elfu 50 wakati gharama za maisha ziko juu kwa laki 1.5. Udanganyifu mtupu....
 
Eti nini? kodi single digit? Uzuri mmoja ahadi zake hazitekelezeki. Bado nasubiria maisha bota kwa kila mtanzania. Remmitence huko kwa extended family zinazidi kuongezeka.
 
Hivi ni lini kutakua na sikukuu kwa wasio na kazi???do we think abt this????
 
Watz tunatatzo la ubinafsi, kunakundi halitaki kusikia wafanyakaz wakiongezewa mishahara wala kupunguziwa kodi nyie kuletewa machine na TRA hamulali kwa vile mlizoea kupi
ga hela bila kodi.
 
Ifweero sijakuelewa,nisekta gani ambayo mwaka jana waliongezewa sh.1900 kama ongezeko la mshahara otherwise tutahtaj standing order
 
I av never seen fixed PAYE, coz PAYE is calculated as a percentage, now how do you come out with this fixed amount!?
 
Mimi siungi sana mishahara kuongezwa ila ningependa Serikali kuongeza uthibiti wa bei ili kile kidogo kinacholipwa, mfanyakazi aweze kununua vitu vingi zaidi, ada za shule ziwe nafuu, nauli zishuke n.k. Ikumbukwe kuwa wakati wanafikiria kuongeza mishahara tayari taasisi zote za Serikali zilishaagizwa kubuni mikakati ya kuongeza mapato; hii ndiyo inapelekea kurudishwa kwa ada ya leseni ya kila mwaka, halmashauri kudai Service levy kwa nguvu, taasisi zisizofanya biashara kutozwa SDL, ada za posta kupanda, nk. Ada na tozo mbalimbali serikalini zilipanda toka mwaka huu wa fedha.

Mabadiliko yote hayo yanapelekea gharama za kufanya biashara Tanzania kuwa kubwa sana na matokeo yake moja ya njia wa wenye viwanda na wafanya biashara kudhibiti matumizi ni kusitisha ajira mpya.

Hilo la kuongeza kima cha chini kama ongezeko hilo litafikia tarakimu 6, uwezekano wa kufungwa kwa viwanda au kupunguza wafanyakazi ni dhahiri. Chukulia kiwanda chenye wafanyakazi 4,000; ongezeko la TZS 100,000 maana yake Basic salary itaongezeka kwa TZS 400,000,000 kwa mwezi; Mchango wa akiba ya uzeeni utaongezeka kwa TZS 40,000,000 kwa mwezi SDL itaongezeka kwa TZS 20,000,000 kwa mwezi, Likizo zitaongezeka kwa TZS 400,000,000 kwa mwaka; kwa mwaka gharama zitaongezeka kwa TZS 5,920,000,000 ongezeko hili haliwezihamia kwa mlaaji (bei) kutokana na ushindani wa bidhaa toka nje. Ukichagiza na uvivu makazini na umeme usio na uhakika, hakika ongezeko la mishahara kama litafika tarakimu sita linakwenda kudidimiza uchumi badala ya kuukuza.

NB: mimi nami ni mwajiri mdogo, namaanisha ongezeko la mishahara litaenda sambamba na "down sizing" ya idadi ya wafanyakazi kwenye sekta binafsi ili kumudu ushindani wa bei "to be competitive in the market".
 
Ifweero sijakuelewa,nisekta gani ambayo mwaka jana waliongezewa sh.1900 kama ongezeko la mshahara otherwise tutahtaj standing order

Hiyo TZS 1900 ilitokana na kubadilika kwa viwango vya kodi ya mishahara
 
Hilo la wakala wa Ajira Mbona bado lipo? Kwenye Makampuni ya simu yote call Center zimekuwa Outsourced na malipo ni chini ya Kima cha chini sikuhizi.
 
Mishahara inatokana na kodi, matumiz yakiongezeka, TRA wanajitahidi kuongeza mapato, mfanyabiashara akikatwa kodi kubwa nae anapandisha bei bidhaaa, na ndio maana tokea wameanza kupandisha mishahara maisha yako vile vile hata hayabadiliki
 
Back
Top Bottom