Mishahara juu, kupanda Julai kwenye bajeti

Mishahara juu, kupanda Julai kwenye bajeti

Kupandisha mishahara na marupu rupu si suluhisho la kudumu la maisha magumu kwa wafanya kazi.......... inflation ikidhibitiwa, tukadhibiti uingizwaji wa bidhaa hafifu, tukazalisha zaidi......... maisha magumu ni ndoto... sasa unaongeza mshahara elfu 50..mhindi anaongeza bei ya pembejeo, mnyakyusa anaongeza bei ya mchele, muiraq anaongeza bei ya maharagwe, mchaga na mhaya wanaongeza bei ya ndizi na maparachichi,msambaa anaongeza bei ya mkaa na machungwa.... back to square Zero....! wafanyakazi wenzangu tutambue tunachokiomba!
 
akili yako ndogo km mjumbe wa bunge la katiba agrrrrr!

naona unamatatizo na UKAWA kweli umewajua kuwa ukawa wanamatatizo tumewatuma kujadili katiba yenyewe yanatoka yanawahi kwenda kudanganya watu nashukuru kuwa unawatambua kuwa wanamatatizo warudi bungeni au warudishe hela walizochukua
 
jk ni kiongozi hodari ambaye hajawahi kutokea kwenye jamii nyingi za kiafrika mungu ampe uzima atupeleke mbali zaidi.
 
Hz mbwembwe tulishazizoea maana kila mwaka huo ndio wimbo.

kila mwaka kivipi inawezekana wewe siyo mtumishi hata hujui kinachoendelea kwenye utumishi,mishahara imekuwa ikipanda kila mwaka na kushuka kwa kodi kila mwaka lakini wewe unaongea bila hata kulijua hilo.
 
sijajutia kuwa mtumishi wa umma katika nchi hii haswa kipindi hiki cha JK, nakumbuka naanza kazi na mshahara wa 308,500 mwaka 2009 leo baada ya miaka 4 tu nakaribia milion, kwa hili sina tabu naye ila kwa mambo ya kijamii hata chama chake kula yangu hawaipati ng'o.
 
kila mwaka kivipi inawezekana wewe siyo mtumishi hata hujui kinachoendelea kwenye utumishi,mishahara imekuwa ikipanda kila mwaka na kushuka kwa kodi kila mwaka lakini wewe unaongea bila hata kulijua hilo.
hata TGS ni nini hajui achana naye
 
jk ni kiongozi hodari ambaye hajawahi kutokea kwenye jamii nyingi za kiafrika mungu ampe uzima atupeleke mbali zaidi.

Hakika hajawahi kutokea kabisa, kiongozi anawasamehe wezi, kiongozi anawajua wauza madawa ya kulevya na bado anawachekea, kiongozi ambaye nata yeye hajui kwa nn nchi yake ni maskini, kiongozi ambaye anasema watoto zetu wanapata mimba za utotoni kwa sababu ya vihereher vyao tu,,,hakika hatujawahi kupata kiongozi kama huyu
 
changa la macho, maana tumezoea kusikia hayo maneno, wala hayanitishi maana ni ya kawaida mno.
 
Ni ujinga kuongeza mshahara kwa 10% halafu unakimbilia kuongeza bei za mafuta na umeme kwa 60%. Bora wasiongeze hata senti moja lakini wapunguze bei za mafuta na umeme. Pia waondoe baadhi ya kodi kwenye material ya ujenzi na uagizaji wa magari na vipuri vyake.

Vinginevyo serikali inawapumbaza wafanyakazi kwa mapesa yasiyokuwa na thamani. Tunafuata njia ya Zimbabwe, kuongeza ma-sifuri kila mwaka kwenye mishahara ni ujinga ulitukuka.
 
Mi naona ni changa la macho tu,mbona mwaka jan alisema hivyohivy mbon haikutekelezwa,ss hapo ndo wamefungulia wafanya biashara kupandisha bei za bidhaa kihorela,isije kua ni maneno tu ya kuweka watu saw

Mwaka jana walipandisha pia mbona mimi iliongezeka Net pay Tshs elfu sita (6,000)
 
Pesa zinazoibiwa nyingi sana na hii wanaongeza kama kuwa-petipeti tuuu japo ni pesa iyo 30 lakin dah aya bhana tutafanyaje sasa
 
Aseme hizo hera atapata wapi?vinginevyo ni usanii tu
 
Hz mbwembwe tulishazizoea maana kila mwaka huo ndio wimbo.

WATU WENGINE BWANA!? Hivi hamjaridhika na maneno na mbwembwe za Mh Rais JMK? Mbaya zaidi mnaanza kupamba magazeti yenu hata bila kuomba ufafanuzi wa ongezeko kwa tarakimu (asilimia ngapi) na uthibitisho wa maneno yake majukwaani!

Mnachekelea na kufurahia maneno tu ya kisanii??!

Mwaka 2010 PAYE ilipungua kwa Tzs 7,500
Mwaka 2011 PAYE hakubadilika
Mwaka 2012 alisema kwa madaha kuwa kodi itapungua PAYE ikashuka kwa Tzs 4,900 nikajiuliza hili ndilo lililo tangazwa kwa mbwembwe zote zile?

Mwaka 2013, kwa mbwembwe zile zile PAYE kwa MASIKITIKO MAKUBWA ikapungua kwa Tzs 1,900 TU bila kujali nani analipa kodi kiasi gani kulingana na mshahara wake??! Hivi Mfanyakazi kupunguzia Tshs 1,900 kwa mwezi kuna muongezea ahueni ganiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii????????????????????????????????????????????????????????????????

Kwa mtiririko huo wa kuendelea kupungua kwa kiwango kinacho tolewa na Serikali sikivu badala ya kupanda, mfano mwaka 2010 PAYE ilishuka kwa 7,500; ilitakiwa kiwango cha PAYE kipungue (kwa maana ya kuongezeka kwa mshahara wa mfanyakazi) tuseme 2012 kiwe Tsh 10,000 ; na mwaka 2013 kiwe mfn 15,000!

Sina hata wasiwasi record ya Mwaka 2014 PAYE itapungua kwa Tsh 900! Tuwe wa kweli punguzo la Tshs 7,500; 4,500; 1,900 lina weza kuonyesha unafuu wowote katika kuendesha maisha ya miaka hii?

Halafu pia, kwa nini Serikali sikivu isipunguze PAYE kwa kuzingatia asilimia badala ya viwango ambavyo ni constant kwa kila level ya PAYE formula??? Na kwa nini kama kweli Serikali ina nia ya (hata isiyofikia dhati)kumuondelea adha mfanyakazi kwa nini kiasi cha PAYE kisiongezeke kama nilivyo toa mfano hapo juu badala ya kupungua kila mara kwa maana ya kuwa PAYE ikipungua kwa kiasi kikubwa kiasi hicho hicho ndicho kinacho ongezeka kwenye mshahara wa mfanyakazi kwa kila mwezi?

Napendekeza UNAFUU WA KULIPA KODI (kupungua kwa kodi) PAYE uendane na viwango vya mishahara kama ilivyo formula yenyewe ya PAYE na kiwe ni kiasi ambacho kina uhalisia wa kuwa nafuu haswa!
 
Hii inaweza ikatekelezwa, maana 2014 na 2015 ni miaka ya mshikemshike kwa watawala wetu.
 
Jk hajui tofauti ya ABSOLUTE NUMBER AND PERCENTANGE (%)! This is real, mwaka jana alisema kwamba atapandisha mishahara ya watumishi wa umma kati ya 30% - 40%. Lakini ukweli ni kwamba kilichokuja kuongezwa kwenye mishahara ni kati ya 30,000/- - 40,000/- na sio 30% - 40% ya gross salary. Subirini hiyo JULY muone, I will be vindicated.
 
Mwaka jana ongezeko kwa watu walio kwenye tax band ya juu (zaidi ya Shs. 720,000) kwa mwezi ilikuwa Shs. 4,900 kwa mwezi! Tafakari!!!, ccifweero
 
Back
Top Bottom