Mishahara juu, kupanda Julai kwenye bajeti

Mishahara juu, kupanda Julai kwenye bajeti

Mimi siungi sana mishahara kuongezwa ila ningependa Serikali kuongeza uthibiti wa bei ili kile kidogo kinacholipwa, mfanyakazi aweze kununua vitu vingi zaidi, ada za shule ziwe nafuu, nauli zishuke n.k. Ikumbukwe kuwa wakati wanafikiria kuongeza mishahara tayari taasisi zote za Serikali zilishaagizwa kubuni mikakati ya kuongeza mapato; hii ndiyo inapelekea kurudishwa kwa ada ya leseni ya kila mwaka, halmashauri kudai Service levy kwa nguvu, taasisi zisizofanya biashara kutozwa SDL, ada za posta kupanda, nk. Ada na tozo mbalimbali serikalini zilipanda toka mwaka huu wa fedha.

Mabadiliko yote hayo yanapelekea gharama za kufanya biashara Tanzania kuwa kubwa sana na matokeo yake moja ya njia wa wenye viwanda na wafanya biashara kudhibiti matumizi ni kusitisha ajira mpya.

Hilo la kuongeza kima cha chini kama ongezeko hilo litafikia tarakimu 6, uwezekano wa kufungwa kwa viwanda au kupunguza wafanyakazi ni dhahiri. Chukulia kiwanda chenye wafanyakazi 4,000; ongezeko la TZS 100,000 maana yake Basic salary itaongezeka kwa TZS 400,000,000 kwa mwezi; Mchango wa akiba ya uzeeni utaongezeka kwa TZS 40,000,000 kwa mwezi SDL itaongezeka kwa TZS 20,000,000 kwa mwezi, Likizo zitaongezeka kwa TZS 400,000,000 kwa mwaka; kwa mwaka gharama zitaongezeka kwa TZS 5,920,000,000 ongezeko hili haliwezihamia kwa mlaaji (bei) kutokana na ushindani wa bidhaa toka nje. Ukichagiza na uvivu makazini na umeme usio na uhakika, hakika ongezeko la mishahara kama litafika tarakimu sita linakwenda kudidimiza uchumi badala ya kuukuza.

NB: mimi nami ni mwajiri mdogo, namaanisha ongezeko la mishahara litaenda sambamba na down sizing ya idadi ya wafanyakazi kwenye sekta binafsi ili kumudu ushindani wa bei to be competitive in the market.
You are the poorest employer!
 
Mshahara ukiogezeka mfanyakaz silazma akafanyie shopping bongo,wafanyabiashara wa bongo hawatufai.
 
Hiyo imekuwa kauli ya kawaida kwa rais kutamka ongezeko la mshahara, lakini nawaambia msitegemee unafuu kwani kwa hapa kwetu ukisikia mfanyakazi kapandishiwa mshahara kesho anapandishiwa bei ya bidhaa muhimu kama maji, umeme,vyakula,ada kodi nk.
Na nimesema hivyo kwa sababu pia serikali yetu haina mfumo wa kudhibiti mfumuko wa bei, kitu ambacho kinasabibisha bei za bidhaa kupanda kila siku, kwahyo hakuna kipya kutoka kwa kauli ya mhe. rais.
 
acha umbea wewe, umeshaanza siasa za buku7, utamkumbuka kwa lipi? kuiba, kuwa mzembe, legelege, docrate za kupewa...endelea kujazilisha.

We mnywa gongo huwezi mkumbuka coz gongo imekutafuna kila kitu wacha sie alotundea makubwa tumkumbuke
 
Habari wadau,

Habari za kuaminika kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya serikali zinasema sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimetumia gharama kubwa kupita kiasi mpaka kupelekea serikali kushindwa kulipa mishahara ya watumishi wake kwa wakati.

Habari zinasema pesa nyingi zimekwapuliwa ili kugharamia sherehe hizo kwa mategemeo ya kupata pesa kutoka chanzo kingine, "serikali imekwama vibaya baada ya kutegemea pesa kutoka kwa wafadhili lakini imekwenda kinyume" ameeleza mtonyaji huyo kutoka serkalini.Hivi sasa serikali inahaha kuokoa jahazi baada ya kufanya matumizi ya hovyo kabisa kwenye sherehe za muungano.

Hbari zaidi zinasema serikali inajipanga kulipa mishahara kwa awamu kulingana na upatikanaji wa pesa na uzito wa halmashauri au ofisi husika,kuna uwezekano mkubwa kwa baadhi ya watumishi kupata mishahara kuanzia tarehe 15/05 na kuendelea.

Wafanyakazi kazi kwenu.
 
Halafu bado tuendelee na serikali 2 yenye muungano wa jina na madaraka na maslai makubwa kwa watawala tuuu.hapana
 
Ninauhakika asilimia kubwa ya wachangiaji ktk habari hii siyo wafanyakazi/waajiriwa.
 
Walimu waje hapa watujibu mkuu wapo wengi sana hapa jf
madeni ya walimu hayapo kisheria ndo maana yanapuuziwa, bora tuongeze muda wa bunge la katiba na posho za wajumbe wa bunge hilo kuliko kulipa madeni ya walimu ambao hawana maana yoyote hapa nchini.
 
mimi mwaka wa jana niliongezewa 33,000/- nalo likaitwa ONGEZEKO LA KUFURU!
 
Back
Top Bottom