WATU WENGINE BWANA!? Hivi hamjaridhika na maneno na mbwembwe za Mh Rais JMK? Mbaya zaidi mnaanza kupamba magazeti yenu hata bila kuomba ufafanuzi wa ongezeko kwa tarakimu (asilimia ngapi) na uthibitisho wa maneno yake majukwaani!
Mnachekelea na kufurahia maneno tu ya kisanii??!
Mwaka 2010 PAYE ilipungua kwa Tzs 7,500
Mwaka 2011 PAYE hakubadilika
Mwaka 2012 alisema kwa madaha kuwa kodi itapungua PAYE ikashuka kwa Tzs 4,900 nikajiuliza hili ndilo lililo tangazwa kwa mbwembwe zote zile?
Mwaka 2013, kwa mbwembwe zile zile PAYE kwa MASIKITIKO MAKUBWA ikapungua kwa Tzs 1,900 TU bila kujali nani analipa kodi kiasi gani kulingana na mshahara wake??! Hivi Mfanyakazi kupunguzia Tshs 1,900 kwa mwezi kuna muongezea ahueni ganiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii????????????????????????????????????????????????????????????????
Kwa mtiririko huo wa kuendelea kupungua kwa kiwango kinacho tolewa na Serikali sikivu badala ya kupanda, mfano mwaka 2010 PAYE ilishuka kwa 7,500; ilitakiwa kiwango cha PAYE kipungue (kwa maana ya kuongezeka kwa mshahara wa mfanyakazi) tuseme 2012 kiwe Tsh 10,000 ; na mwaka 2013 kiwe mfn 15,000!
Sina hata wasiwasi record ya Mwaka 2014 PAYE itapungua kwa Tsh 900! Tuwe wa kweli punguzo la Tshs 7,500; 4,500; 1,900 lina weza kuonyesha unafuu wowote katika kuendesha maisha ya miaka hii?
Halafu pia, kwa nini Serikali sikivu isipunguze PAYE kwa kuzingatia asilimia badala ya viwango ambavyo ni constant kwa kila level ya PAYE formula??? Na kwa nini kama kweli Serikali ina nia ya (hata isiyofikia dhati)kumuondelea adha mfanyakazi kwa nini kiasi cha PAYE kisiongezeke kama nilivyo toa mfano hapo juu badala ya kupungua kila mara kwa maana ya kuwa PAYE ikipungua kwa kiasi kikubwa kiasi hicho hicho ndicho kinacho ongezeka kwenye mshahara wa mfanyakazi kwa kila mwezi?
Napendekeza UNAFUU WA KULIPA KODI (kupungua kwa kodi) PAYE uendane na viwango vya mishahara kama ilivyo formula yenyewe ya PAYE na kiwe ni kiasi ambacho kina uhalisia wa kuwa nafuu haswa!