Mishahara juu, kupanda Julai kwenye bajeti

Mishahara juu, kupanda Julai kwenye bajeti

ifweero

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2013
Posts
7,957
Reaction score
1,341
Friday, May 2, 2014MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAR 02.05.2014 VICHWA VIKUBWA JK ATANGAZA NEEMA KWA WAFANYAKAZI,MADENI YA WALIMU YAGEUZWA DILI


Rais Kiwete ametangaza neema hiyo jana kwenye sherehe za mei mosi ambapo hivi sasa kima cha chini kitaongezeka maradufu na kodi kushuka hadi tarakimu moja yaani chini ya asilimia 10.

Kima cha chini kinatarajiwa kuwa 315 000 ambacho kilikuwa ni kilio cha TUCTA,pia wakala wa ajira wamepigwa marufuku na mifuko ya hifadhi ya jamii imeboroshwa.

source. Magazeti ya leo

Dar/mikoani. Rais Jakaya Kikwete ametoa ahadi mbili za kuwafurahisha wafanyakazi. Kwanza ametangaza nia ya kuongeza mishahara yao na pili, kupunguza kodi inayokatwa kwenye mishahara hiyo mambo ambayo ameahidi kutekelezwa katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema anatambua kuwa wafanyakazi wana hamu ya kujua Serikali itasema nini kuhusu masilahi yao.

Alisema malalamiko ya wafanyakazi wengi ni kutaka kuona kima cha chini cha mshahara kinaongezwa huku kodi kwenye mishahara (Paye), ikipungua.

"Mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kufanya hivyo, tumethibitisha miaka iliyopita na tutaendelea kuwa hivyo," alisema.

Huku akishangiliwa na wafanyakazi waliofurika katika Uwanja wa Uhuru, Rais Kikwete alisema: "Najua kuwa nyongeza tuliyotoa mwaka jana si kubwa kama wafanyakazi walivyotaka iwe... hata mimi nisingependa iwe hivyo."

"Kwa nyongeza iliyofanywa mwaka jana, hivi sasa Serikali inatumia asilimia 44.9 ya Bajeti kulipa mishahara ambayo ni asilimia 10 ya Pato la Taifa."

Akifafanua namna Serikali ilivyofikia uamuzi wa kuongeza mishahara kwa mwaka huu, Rais Kikwete alisema kulikuwa na mjadala mkali baina ya wafadhili waliodai nyongeza ni kubwa mno.

"Ni kweli mapato yetu ni madogo lakini kwa kuwa mishahara ni midogo, lazima tuendelee kuongeza, hata hicho kidogo lazima ukitoe ili uijenge ile nafuu, alisema bila kutaja kiwango kitakachoongozwa.

"Hata sasa kumekuwa na ubishi mkali kati ya Wizara ya Utumishi na Hazina kuhusu nyongeza ya mwaka huu iwe mpaka kiasi gani, nikaingilia kati nikakubaliana na utumishi, Hazina walikuwa wanataka ipingue kidogo," alisema.

Walimu na shemeji yao

Suala la mshahara lilijitokeza kwa namna nyingine kwenye maandamano ya wafanyakazi pale walimu walipoamua kusimama mbele ya jukwaa kuu na kumweleza Rais Kikwete ambaye walimtaja kama shemeji yao, kwamba hawajapata mshahara wa Aprili wakimtaka aingilie kati.

"Shemeji, shemeji, shemeji, hatujapata mishahara yetu ya Aprili, tunaomba utusaidie," walitoa ujumbe huo kwa njia ya wimbo.

Tofauti na wafanyakazi wengine ambao walipita mbele ya mgeni rasmi bila kusimama, walimu walisimama kwa dakika moja kuhakikisha ujumbe huo unamfikia.

Wakati hayo yakitokea, Rais Kikwete na viongozi wengine walikuwa wakicheka huku wakiwaangalia walimu hao waliokuwa wakiendelea kuimba wimbo huo.

Ajira kwa wageni

Rais Kikwete aliagiza yafanyike marekebisho kwenye sheria ya vibali vya ajira ili kudhibiti ongezeko la wafanyakazi wa kigeni nchini ambao wanafanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania.

Aliagiza hatua hiyo itekelezwe haraka hata ikibidi kwa kupeleka bungeni hati ya dharura ili kuhakikisha jambo hilo linaanza mara moja.

Malalamiko ya Tucta

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholas Mgaya alisema pamoja na ongezeko la mishahara kufanyika kila mwaka, limekuwa dogo mno kiasi cha kushindwa kufikiwa kima cha chini ya mshahara kinachotakiwa.

Alisema kwa upande wa sekta binafsi, Serikali imeongeza mshahara kutoka Sh100,000 hadi Sh450,000 mwaka jana, huku sekta ya kilimo ikiwa ya mwisho kwa kuwa na kiwango cha chini zaidi.

"Hali hii imesababisha kuwapo kwa upungufu mkubwa wa wafanyakazi mashambani na hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao," alisema na kuongeza:

"Tunapenda kuikumbusha Serikali kwamba kumlipa mfanyakazi mshahara unaokidhi mahitaji muhimu ya maisha siyo jambo la fadhila, bali ni mojawapo ya haki za msingi za binadamu zinazosisitizwa na jumuiya za kimataifa."

Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Hafsa Mtassiwa alisema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili wafanyakazi zikiwamo za kodi ya mishahara kuwa juu na kwamba inazifanyia kazi.

Mbeya

Mratibu wa maadhimisho hayo mkoani Mbeya, Joseph Sayo ameiomba Serikali iache kuwanyonya wafanyakazi na kuwa mwajiri msumbufu kuliko wengine nchini.

"Serikali inadaiwa na wafanyakazi fedha nyingi na pia inawakopa wafanyakazi kwa njia mbalimbali zikiwamo za kupitia kwenye mifuko ya hifadhi za jamii na kushindwa kurudisha kwa wakati," alisema.

Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amewataka waajiri kufuata sheria na taratibu za kazi katika kuhakikisha kuwa wanawalipa wafanyakazi wao stahili zao ikiwamo nyongeza ya mishahara, kupandishwa vyeo na motisha kwa wanaostahili.

Geita

Wafanyakazi mkoani Geita, wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kutekeleza ahadi mbalimbali ilizotoa kuboresha maisha yao, hivyo kulazimika kufanya kazi kwenye mazingira magumu.

Morogoro

Mratibu wa Tucta Mkoa wa Morogoro, Charles Luvunzu amesema rushwa na ukosefu wa uadilifu ni miongoni mwa mambo yanayokiukwa na waajiri wengi licha ya vyama vya wafanyakazi kuyapigia kelele.

Shinyanga

Tucta imewataka waajiri kuacha tabia ya kuwafukuza wafanyakazi kama kuku. Imeshauri wakae meza moja kujadiliana ili kutatua matatizo yanayowakabili sehemu za kazi.

Mwanza

Mratibu wa Tucta Mwanza, Evarist Mwalongo ameutaka uongozi wa mkoa kuwachukulia hatua za kisheria waajiri wasiofuata sheria za kazi huku akiitaka Serikali kubadilisha sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ili itoe mafao mazuri kwa wastaafu na kiwango cha kodi kwenye mshahara kipungue hadi asilimia moja.

Mara

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Henjewelle amewaagiza waajiri kuwalipa wafanyakazi masilahi yao kwa wakati ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara kazini.

Imeandikwa na Goodluck Eliona, Raymond Kaminyoge, Aidan Mhando, Salum Maige, Happy Lazaro, Ernest Magashi, Dinna Maningo, Veronica Modest, Lilian Lucas, Stella Ibengwe, Lauden Mwambona na Salim Mohammed.

Source: Mwananchi
 
Sidhani kama ongezeko hilo litafika hata elfu hamsini
 
  • Thanks
Reactions: JPN
Rais Kikwete atangaza punde kuwa ataongeza mishahara kwa wafanyakazi wa umma katika bajeti ya mwaka huu, asema changamoto ni mapato
Wafanyakazi wa tanzania mpoo...sitarajii tena kuona maandamano ya wafanyakazi tz
Wakidai ongezeko la mshahara
Au ni chaga la macho waajiriwa wenzangu?
Kwani madeni ya walimu yamelipwa..??
 
  • Thanks
Reactions: JPN
Kwa jinsi formla ya kodi ilivyo, ukiongezewa mshahara na kodi inaongezeka. Alitakiwa apunguze kiwango cha kodi
 
  • Thanks
Reactions: JPN
Unaongezewa mshahara wanakupandishia bei za bidhaa....
mambo pale pale
bei ya vitu hupanda automatically pindi mishahara inapopanda na hivyo thamani ya pesa inakua chini.kupandisha mishahara sio solution,lakini mtoto akililia wembe...
 
mbayuwayu akili za kuambiwa changanya na zako
 
Watu wengine huwa hamfikiri au sijui ni uboya tuu..., kwani akiongeza mshahara hiyo pesa ya kulipa mshahara ye anatoa wapi.., si anakupiga kodi laki anakuongeza mshahara 50k.., sasa si anajiongezea yeye.., vitu vitapanda bei na utannunua na hako kamshahara kako hela inarudi kwake.., wafanyakazi ni slaves (by definition).., watumwa kabisa..!!
 
Kwa jinsi formla ya kodi ilivyo, ukiongezewa mshahara na kodi inaongezeka. Alitakiwa apunguze kiwango cha kodi

Angalie kwanza tofauti ya mishahara kati ya wizara na taasisi/wakala
 
Back
Top Bottom