Nimeisoma Sredi hapa busatini iliyoshushwa na Member anaekwenda na username
tpaul , akidondoa misamiati iliyo heat Bunge la
escrow .
Mimi nishuke na baadhi ya semi ambazo kimtazamo , naamini zimekimbiza .
SEMI :-
1 .
"Mfumo mzima wa Serikali , ni kama ulipigwa ganzi , ama uliganzishwa"
- By Deo Filikunjombe
2 .
"Mlikaa Kunduchi beach , mkaanza kugawana fedha za Serikali kama chakula cha njaa"
- By Ole Sendeka.
3.
(Akim'quote Mwl Nyerere , Filikunjombe alisema) :
"Tukianza kuwavumilia Masultani wa kuchaguliwa , tutapanda Masultani wa kuzaliwa."
4 .
"Kuna wanaofikiri ukishakua Sultani, utakufa Sultani , nadhani wanakosea!"
5.
"Watu wa mfano wa Rashidi Kawawa ni wachache sana duniani , na hawazaliwi kila siku"
6.
Akim'quote Thabit Kombo Filikunjombe alisema :
"Ongea uwongeavyo , lakini wacha/weka akiba ya maneno"
7.
"Ni rushwa pekee inayofanya mwenye macho asione! Mwenye maskio awe kiziwi , na huweza kumfanya mwanaume akawa mwanamke , na mwanamke kuwa mwanaume"
- By Ole Sendeka.
8.
"Waliomuua Yesu, baada ya kumuua walimfunikia shimoni/pangoni jiwe kubwa sana na kuhakiki asingewezatoka kivyovyote vile! Lakini wauwaji walipoondoka kwenda Galilaya , walimkuta Yesu kafika Galilaya kabla yao"
- By Kangi Lugola.
'