Waliobeba Mabilioni ya ESCROW kwenye Simba Trust wamtelekeza Sethi

kamati ya ufundi

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
416
438
Ni wabia wenza katika kampuni ya PAP, waliochota mabilioni ya ESCROW kupitia IPTL

Yabainika ndio waliobeba fedha kwenye masandarusi na kuzikimbiza nje ya nchi na kununua majumba ya kifahari

Wamtekeleza mwenzao gerezani huku wakihaha kuitapeli serikali mabilioni mengine kupitia TANESCO

Vyombo vya dola vyatakiwa kuwachukulia hatua sanjari na mwenzao

Na Mwandishi Wetu

MCHEZO mchafu unaofanywa na Kampuni ya Simba Trust iliochota mabilioni ya shilingi kwenye akaunti ya ESCROW yazidi kufichuka ikiwemo mpango wao wa kutaka kuitapeli tena serikali kupitia Shirika la Umeme nchini(TANESCO)

Kampuni hiyo, ambayo katika sakata la ESCROW ilichota mabilioni ya fedha na kwenda kuzificha nje ya nchi kwa kununua majumba ya kifahari kwenye nchi mbalimbali, baada ya kuzichukua fedha hizo kupitia kwenye masandarusi.

Taarifa ilizozipata gazeti hili, zilieleza kuwa kampuni hiyo imeanza mikakati ya utapeli pamoja na kumtekeleza mbia mwenza wao, ambaye sasa anashikiriwa na serikali, ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya PAP/IPTL, Habinder Singh Sethi, ambao ni wamiliki wenza wa kampuni hiyo.

Sethi pamoja na aliyekuwa mmiliki wa Kampuni Kampuni ya VIP Engineering And Marketing, James Rugemalira, wapo mahabusu kwa sasa wakikabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh. bilioni 300.

Taarifa za ndani zinaelez kuwa Kampuni ya Simba Trust ambayo ilinunua hisa asilimia 50 kwenye kampuni ya PAP iliyonunua hisa zote za IPTL iliyoliingiza taifa kwenye hasara, sasa inadaiwa kumtekeleza mbia wake Harbither Sing Sethi huku ambaye amenunua hisa zaidi ya asilimia 50 kwenye kampuni hiyo.

Simba Trust ambayo imesajiliwa nchini Australia chini ya uwakilishi wa mwanasheria mmoja wa Australia mwenye ukaribu na baadhi ya waliowahi kuwa viongozi serikali katika awamu zilizopita.

Kwa hapa nchini kampuni hiyo ni moja inatajwa kunufaika na uchotwaji wa mabilioni ya fedha ya Escrow huku taarifa ya iliyokuwa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), katika Bunge la 10 chini ya Spika mstaafu Anne Makinda, iliihoji serikali kuhusu uhalali wa kampuni hiyo na wamiliki wake.

Hata hivyo ilidaiwa kuwa wapo vigogo kadhaa walihusishwa na kuhusika kwao kwa namna moja ama nyingine kwenye sakata hilo ambalo lilisababisha kuwajibishwa kwa mawaziri wa serikali ya awamu ya nne akiwamo aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye alijiuzulu mwenyewe.

Katika sakata hilo ambalo pia liliwahusu watumishi kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Tanesco na Benki Kuu (BoT).

Gazeti hili lilipomtafuta Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola, ili kupata ufafanuzi kuhusu uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo hakupatikana na alipotafutwa Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba, aliomba atafutwe leo kwani yupo nje ya ofisi kwa majukumu mengine.

Naye, mmoja wa wachambuzi wa masuala ya rasilimali, Joseph Patrick alisema ni lazima vyombo vya dola kuichunguza kampuni hiyo na kuwafikisha mahakamani kwa kuwa wanachofanya sasa ni kutumia ukaribu wao wa waliokuwa viongozi wa awamu ya zilizopita kuficha kichaka chao cha fedha.

"Vyombo vya dola wawachukulie hatua kwani, haiwekani katika kuwakamata kuwa na upendeleo baadhi wanakamatwa na wengine hawakamatwi lazima sheria ifuate mkondo wake na sio kukamata baadhi na wengine unawaacha," alisema.

CHANZO: Magazeti ya Leo - Mtanzania, Majira, Tanzania Daima na JAMVI LA HABARI
 
Attachments

  • SETTTII.jpg
    SETTTII.jpg
    68.3 KB · Views: 61
Ni bora kuishi maisha mafupi ya raha sana kuliko kuishi maisha marefu ya dhiki kubwa kama mimi
 
Hata huyo Seth hawezi kufungwa maana ili umfunge, ni lazima na washirika wake waingie mataani.

Mwisho wa siku utasikia hiyo kesi imefutwa.

Ni swala la muda.
 
Sio Muda mwanasheria mkuu we serikali atasema hana Muda wa kuendelea na hiyo kesi
 
Siyo kumtekeleza ni kumtelekeza, kongoro na korongo ni vitu viwili tofauti, ndivyo ilivyo kwa tekeleza na telekeza.
 
Wakimkamata Chenge, tibaijuka, ngeleja na maaskofu basi siku hiyo hiyo nitataacha kukwepa kodi

Hawa uliyowataja hapa walipewe zawadi tu na hawakuhusika na uchotaji fedha serikalini!wajusika wanajulikana ila itabidi Rais Dr Magufuli(Nyerere II) akibali kufukua makaburi and call it a spade a spade kwani Ikulu ya enzi hizo ilihusika kwa njia moja au nyingine yaani wafanyakazi ambao siyo waadilifu walijusika kwenye madili haya. Hii ni eavesdropping! Msiwaonee wabunge na maaskofu ambao ni vijukuu vilipewa chokoleti tu, wahusika wapo! Simba Trust ni ya nani, board members wao na share holders ni wanani, hii ilikuwa kazi ya kamanda Mlowola na wenzake! Mfichaficha maradhi kilio kitamfika, kama ni watoto wa viongozi serikali kazi kwa Rais wetu, ndiyo maana Rais Magufuli anafuatilia kila kitu kwani kithungu tunasema ‘you delegate power but never abdicate power’ else they fix you!
 
Ni wabia wenza katika kampuni ya PAP, waliochota mabilioni ya ESCROW kupitia IPTL

Yabainika ndio waliobeba fedha kwenye masandarusi na kuzikimbiza nje ya nchi na kununua majumba ya kifahari

Wamtekeleza mwenzao gerezani huku wakihaha kuitapeli serikali mabilioni mengine kupitia TANESCO

Vyombo vya dola vyatakiwa kuwachukulia hatua sanjari na mwenzao

Na Mwandishi Wetu

MCHEZO mchafu unaofanywa na Kampuni ya Simba Trust iliochota mabilioni ya shilingi kwenye akaunti ya ESCROW yazidi kufichuka ikiwemo mpango wao wa kutaka kuitapeli tena serikali kupitia Shirika la Umeme nchini(TANESCO)

Kampuni hiyo, ambayo katika sakata la ESCROW ilichota mabilioni ya fedha na kwenda kuzificha nje ya nchi kwa kununua majumba ya kifahari kwenye nchi mbalimbali, baada ya kuzichukua fedha hizo kupitia kwenye masandarusi.

Taarifa ilizozipata gazeti hili, zilieleza kuwa kampuni hiyo imeanza mikakati ya utapeli pamoja na kumtekeleza mbia mwenza wao, ambaye sasa anashikiriwa na serikali, ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya PAP/IPTL, Habinder Singh Sethi, ambao ni wamiliki wenza wa kampuni hiyo.

Sethi pamoja na aliyekuwa mmiliki wa Kampuni Kampuni ya VIP Engineering And Marketing, James Rugemalira, wapo mahabusu kwa sasa wakikabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh. bilioni 300.

Taarifa za ndani zinaelez kuwa Kampuni ya Simba Trust ambayo ilinunua hisa asilimia 50 kwenye kampuni ya PAP iliyonunua hisa zote za IPTL iliyoliingiza taifa kwenye hasara, sasa inadaiwa kumtekeleza mbia wake Harbither Sing Sethi huku ambaye amenunua hisa zaidi ya asilimia 50 kwenye kampuni hiyo.

Simba Trust ambayo imesajiliwa nchini Australia chini ya uwakilishi wa mwanasheria mmoja wa Australia mwenye ukaribu na baadhi ya waliowahi kuwa viongozi serikali katika awamu zilizopita.

Kwa hapa nchini kampuni hiyo ni moja inatajwa kunufaika na uchotwaji wa mabilioni ya fedha ya Escrow huku taarifa ya iliyokuwa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), katika Bunge la 10 chini ya Spika mstaafu Anne Makinda, iliihoji serikali kuhusu uhalali wa kampuni hiyo na wamiliki wake.

Hata hivyo ilidaiwa kuwa wapo vigogo kadhaa walihusishwa na kuhusika kwao kwa namna moja ama nyingine kwenye sakata hilo ambalo lilisababisha kuwajibishwa kwa mawaziri wa serikali ya awamu ya nne akiwamo aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye alijiuzulu mwenyewe.

Katika sakata hilo ambalo pia liliwahusu watumishi kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Tanesco na Benki Kuu (BoT).

Gazeti hili lilipomtafuta Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola, ili kupata ufafanuzi kuhusu uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo hakupatikana na alipotafutwa Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba, aliomba atafutwe leo kwani yupo nje ya ofisi kwa majukumu mengine.

Naye, mmoja wa wachambuzi wa masuala ya rasilimali, Joseph Patrick alisema ni lazima vyombo vya dola kuichunguza kampuni hiyo na kuwafikisha mahakamani kwa kuwa wanachofanya sasa ni kutumia ukaribu wao wa waliokuwa viongozi wa awamu ya zilizopita kuficha kichaka chao cha fedha.

"Vyombo vya dola wawachukulie hatua kwani, haiwekani katika kuwakamata kuwa na upendeleo baadhi wanakamatwa na wengine hawakamatwi lazima sheria ifuate mkondo wake na sio kukamata baadhi na wengine unawaacha," alisema.

CHANZO: Magazeti ya Leo - Mtanzania, Majira, Tanzania Daima na JAMVI LA HABARI
Makaburi
 
Hata huyo Seth hawezi kufungwa maana ili umfunge, ni lazima na washirika wake waingie mataani.

Mwisho wa siku utasikia hiyo kesi imefutwa.

Ni swala la muda.
Seth anaombewa afie jela ili kila kitu kifutwe hilo ndilo Dua lao
 
Back
Top Bottom