PostGE2025 Rasmi, Bunge la Ulaya lapiga kura zote 539 za NDIYO kuzuia misaada Tanzania, wahusika wa kadhia ya Oktoba 29 kuwekewa vikwazo

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
448
Reaction score
3,359
Bunge la Ulaya limeitaka Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya kusitisha msaada kwa serikali ya Tanzania na kuwawekea vikwazo wahusika wa ukandamizaji uliofanywa baada ya uchaguzi mkuu. Wabunge wa Ulaya wamelaani vikali vitendo hivyo na kutaka kuachiwa kwa wapinzani waliokamatwa.

Wamesisitiza kuwa mauaji, majeruhi na taarifa za makaburi ya halaiki baada ya uchaguzi wa 2025 ni ushahidi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Wametaka pia kuachiliwa kwa mwanasiasa Tundu Lissu mara moja na bila masharti. Azimio kuhusu Tanzania limepitishwa bila kupingwa kwa kura 539.

1000521424.jpg
1000521425.jpg

Pia soma > Bunge la Ulaya lapitisha maazimio 9 kwa Tanzania. Lakata misaada na kutangaza Uchaguzi haukuwa huru na haki. Waliohusika na ukiukwaji kuwekewa vikwazo
 
Umoja wa Ulaya umesitisha Mpango wa Maendeleo wa Tanzania 2025, ukitaja uzito wa hali ya nchi kufuatia ghasia zilizoambatana na uchaguzi tata wa Oktoba 29.

Kwa mujibu wa Maria Luís Albuquerque, Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na Uthabiti wa Kifedha, Huduma za Kifedha na Masoko ya Mitaji, uchaguzi mkuu wa Tanzania ulikuwa na dosari, idadi ndogo ya wapiga kura ikijitokeza, na ghasia zilizowagharimu mamia ya raia maisha yao.

Vile vile Maria Luis alibainisha kuwa kipindi kabla ya uchaguzi kulishuhudia kupungua kwa nafasi ya kiraia, utekaji nyara, na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani kama vile Tundu Lissu ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini, mashtaka ambayo wengi wanaona yamechochewa kisiasa.

"...Kwa uzito wa hali hii, EU imesitisha Mpango wa Maendeleo wa Tanzania 2025 na inasisitiza uchunguzi wa kuaminika ili kurejesha imani."alisema Maria Luis katika kikao cha Bunge hilo.
Kwishaaaa!
 
Hawa wana influence kubwa IMF,World Bank, AFDB wadau wakubwa wa mikopo na misaada Tanzania.

Influence yao inaenda mbali zaidi kwenye sekta zote.
Sio influence ile AfDB nchi.zinatoa pesa na watoaji wakubwa ni USA canada na nchi za umoja wa ulaya. Japan.

Japo ni independent lakini wenye hela wakikukazia ujue Marekani nayo itakata misaada.
 
Umoja wa Ulaya umesitisha Mpango wa Maendeleo wa Tanzania 2025, ukitaja uzito wa hali ya nchi kufuatia ghasia zilizoambatana na uchaguzi tata wa Oktoba 29.

Kwa mujibu wa Maria Luís Albuquerque, Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na Uthabiti wa Kifedha, Huduma za Kifedha na Masoko ya Mitaji, uchaguzi mkuu wa Tanzania ulikuwa na dosari, idadi ndogo ya wapiga kura ikijitokeza, na ghasia zilizowagharimu mamia ya raia maisha yao.

Vile vile Maria Luis alibainisha kuwa kipindi kabla ya uchaguzi kulishuhudia kupungua kwa nafasi ya kiraia, utekaji nyara, na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani kama vile Tundu Lissu ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini, mashtaka ambayo wengi wanaona yamechochewa kisiasa.

"...Kwa uzito wa hali hii, EU imesitisha Mpango wa Maendeleo wa Tanzania 2025 na inasisitiza uchunguzi wa kuaminika ili kurejesha imani."alisema Maria Luis katika kikao cha Bunge hilo.

Pia soma > Bunge la Ulaya lapitisha maazimio 9 kwa Tanzania. Lakata misaada na kutangaza Uchaguzi haukuwa huru na haki. Waliohusika na ukiukwaji kuwekewa vikwazo
Mungu awabariki wazungu
 
Jana nilijua wanatishia nyau kumbe kweli?
 
Back
Top Bottom