Mirathi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mirathi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by jlm, Dec 28, 2009.

 1. jlm

  jlm Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  hello..natumai wote wazima
  naamini hapa kuna wataalamu wa mambo ya sheria na ushauri pia.
  kuna situation ambayo ipo hivi..kwenye familia imetokea kuwa baba ana mtoto wa nje ambaye alizaa kabla hajaoa. lakini baadae akaoa akawa na familia yake..imetokea baba kafa bila kuacha wosia..sasa je kisheria yule mtoto wa nje ana haki ya kurithi?? and if not why? help me with this pliz.
   
 2. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Inategemea na sheria za mila za makabila. Mfano kwa waislamu mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hawezi kurithi. Labda baba mwenyewe amuandikie vitu vyake na amkabidhi kabla hajafa.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ulitakiwa uweke sawa dini ya wahusika, maana ni ishu sana kwa hapa!Lakini pia, suala la huyo mtoto kama alikuwa na ukaribu gani na familia hii ya baba yake pia lina parameter kubwa. Imagine kama mtoto huyu anatokea mara baada ya baba yake kufariki, atakuwa considered vipi!...Lakini kama walikuwa nae ndani, basi kiubinadamu anastahili urithi!
   
 4. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Ninavyoelewa mimi karibu dini zote hazitambui mwanaharamu [mtoto aliyezaliwa kutokana na zinaa] na mila nyingi ili akubaliwe inabidi mambo fulani fulani yafanyike lakini ufahamu kuwa baada kifo kunakuwa na opportunist wengi tu hivyo huwezi kumkosesha huyo mtoto haki yake [mtoto hakuwa na chaguo la namna ya kuzaliwa kwake] hivyo ni bora baba mtu kutambua kosa lake hilo na kumpatia huyo mtoto zawadi yake au haki yake [siyo mirathi] ungali hai
   
 5. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,165
  Trophy Points: 280
  Mtoto wa nje ya ndoa huwa harithi kwa sheria ya kimila. ndhani hii iliwekwa makusudi kuzuia UZINZI ingawa sasa naona serikali inataka kuruhusu uzinzi inapoweka sheria ya kuwatambua wanaharamu (bastards) kwa mantiki hiyo hakuna sababu ya kuwa na kuweka viwango vya kuoa wake, ruksa kuoa kuoa!!!!
   
 6. I

  Irizar JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 217
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa nje ya ndoa harithi kitu, vitu vyake vyoteeee anatakiwa apewe na baba au mama mzazi kabla hajafa ampe kabisaa viwe vyake full stop. Haijalishi ni dini gani, hata serikali pia haitampa kitu labda tu kama wazazi wameandikia kwenye urithi wao. na bado itakuwa ni ngumu.
  Kama ni mwanao ndiye hakurithishwa isikupe taabu, mpeleke mtoto wako shule akasome aelimike atapata kazi na siku moja atapata mali zake mwenyewe nyingiiiii kuliko hata hizo za kuachiwa na mzazi wake, hazina mpango sana. Mimi mwenyewe baba yangu alipokufa sikupewa kitu hata kimoja sababu ni mtoto wa nje, na sasa nina elimu,afya nzur,i pesa, kazi na mengineyo mengi tu, naishi raha msitarehe kuliko watoto wa kwenye ndoa, hao waliorithi wakiniona wanajibeba hawana kitu nimewapita woteeeeee!!!!
  Usitegee mali za kurithi ukipewa sawa ukikosa tafuta chako na uweke mambo yako sawa.

  Ila pia jamani wanaume waache kuzaa zaa ovyo ovyooo inawapa shida sana watoto maisha yamekuwa magumu sana.
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Safi kabisa. Watu tujitahidi tuzae watoto wetu ndani ya ndoa. Hii ina heshima yake kwa dini na mila zote.
   
 8. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,755
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  kwa ujumla sheria iwe ya kiserikali au ya kimila haziruhusu mtoto wa nje ya ndoa kurithi mali.
   
 9. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Juu ya suala kama hili inategemea unataka liamuliwe/litatuliwe/lishauriwe kwa njia ipi!
  1.ki-serikali(ki-mahakama)
  2.ki-dini (BAKWATA)
  3.ki-mila
  au4.ki-familia
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Watoto wanaozaliwa nje ya ndoa ni wa mama na kwa msingi huo baba mhusika anatakiwa wakati wa uhai wake akamilishe taratibu zote za kumhalalisha na kutambulika na ikiwezekana amwachie urithi kwa wosia vinginevyo atatoka kapa.Sheria za Tz za mirathi bado hazijahuishwa - kwa maana kuna sheria tatu zinazosimamia mirathi:
  1. Sheria za Kidini hasa ya Kiislam zenye kufuata maagizo ya kurani.Kwa uislam mtoto wa namna hii hata inyeshe mvua liwake jua, mtoto wa nje ya ndoa hapati urithi na mahakama itaamua kufuatana na sheria hii ya kiislam kama mirathi itafunguliwa mahakamani.
  2. Sheria za kimila - hapa inategemea mhusika kama alikuwa kweli anaishi kufuatana na mila na desturi za kabila lake,Fikiria baba ambaye ni mmakonde, mama msegeju. Wanaishi Dar es salaa wakifuata dini ya Kiislamu! Unadhani huyo mtoto ataokota kitu? La hasha.Mila na dini vitajadiliwa sana mahakamani na mwisho wa siku nina hakika utaratibu wa dini ya kiislam utatumika.
  3. Sheria ya serikali - hapa napo mtoto huyu hapati kitu!
   
 11. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 526
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  all we need is to be empathetical and love one another we dont need whatever those laws says. love is the big law
   
Loading...