Mirathi katika ndoa ya wawili

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
13,559
21,040
Wajuzi wa sheri.a naomba mnisaidie kuhusu yafuatayo yanayohusu mirathi haswa kwa ndoa za kikristo za mme mmoja mke mmoja:

1) Je mali mlizochuma ndani ya ndoa umiliki wake ukoje? mfano tuna nyumba tatu na zote zimeandikwa jina la baba je mama hana umiliki katika mali hizo na je kama baadhi ya magari yameandikwa jina la mama je baba hana umiliki katika magari hayo?

2) Je kama mmoja wa wanandoa anataka kuandika mirathi atarithisha asilimia zake tu za umiliki wa mali au atarithisha mali yote? mfano tunamiliki nyumba na mke wangu je mimi kama mme nina uwezo wa kumwandika mrithi bila kumshirikisha mwanandoa mwenzangu?

3) Je kuna uwezekano wa kuandikisha mali zenu kwa majina ya wawili kwa pamoja ili kuonyesha kwambq mnamiliki kwa kushare?

Wataalam wa sheria na wenye uzoefu na hivi vitu naomba mnipe majibu ya maswali haya na nina uhakika wengi watapata elimu katika hili

cc Mshana Jr ,
 
Kwa ufahamu wangu mdogo... Mali mtagawana nusu kwa nusu hats zile ulizo zitafuta kabla hamuaingia kwenye ndoa na Mali ambayo uliyoandika jina la mke wako itahesabika ni Kama zawadi umempatia hivyo hiyo aijumishwi kwenye Mali mtakazo gawana. Hayo Maelezo kutokana uelewa wangu tu.
NB:Mimi sio mwanasheria.
 
Wajuzi wa sheri.a naomba mnisaidie kuhusu yafuatayo yanayohusu mirathi haswa kwa ndoa za kikristo za mme mmoja mke mmoja:

1) Je mali mlizochuma ndani ya ndoa umiliki wake ukoje? mfano tuna nyumba tatu na zote zimeandikwa jina la baba je mama hana umiliki katika mali hizo na je kama baadhi ya magari yameandikwa jina la mama je baba hana umiliki katika magari hayo?

2) Je kama mmoja wa wanandoa anataka kuandika mirathi atarithisha asilimia zake tu za umiliki wa mali au atarithisha mali yote? mfano tunamiliki nyumba na mke wangu je mimi kama mme nina uwezo wa kumwandika mrithi bila kumshirikisha mwanandoa mwenzangu?

3) Je kuna uwezekano wa kuandikisha mali zenu kwa majina ya wawili kwa pamoja ili kuonyesha kwambq mnamiliki kwa kushare?

Wataalam wa sheria na wenye uzoefu na hivi vitu naomba mnipe majibu ya maswali haya na nina uhakika wengi watapata elimu katika hili

cc Mshana Jr ,
Kimsingi mali ambazo wanandoa wamechuma pamoja ktk kipindi cha ndoa zina umiliki wa pamoja. Wakati mwingine mwanandoa mmoja anaweza akawa amechuma mali kabla ya kufunga ndoa, ikitokea baadaye mwanandoa mwingine akazikuta mali na kuziendeleza yaani akafanya 'exhaustive improvements' basi naye anastahili kuwa na share ktk mali hizo.

Kwenye mali walizochuma wote ama zenye umiliki wa pamoja, mwanadoa mmoja hatakiwi kufanya lolote linaloathiri maslahi ya mwenza wake kama vile kuhamisha umiliki kwa njia ya wosia, kuuza, kuweka rehani, kutoa zawadi nk bila ruhusa ya mwenza wake.

Vile vile, mali walizochuma pamoja, mwanandoa mmoja pekee hapaswi kuziandikia wosia maana akifa yeye basi mwenza wake atakuwa mrithi tunasema kuna 'survivorship' labda kama wosia unaandikwa basi 'joint will' yaani wosia wa pamoja wafaa ktk mazingira haya.

Hata hivyo, sheria inaruhusu mwanandoa kumiliki mali binafsi ambayo haitakuwa sehemu ya ndoa na hii anaweza kumua nini cha kufanya bila ridhaa ya mtu
 
Je kuna vifungu vyovyote vya sher.ia unaweza kutuwekea hapa kwa faida ya wengi? Nashukuru sana kwa maelezo yako mazuri.

Na je ukitaka kuandika mirathi inakuwaje kaa mna mali wewe na mkeo?
 
Mimi ni bush lawyer;ila katika familia yangu Kuna Mali alizochuma Mama pekee na alizochuma mzee.Lakini baada ya mzee kufariki tulikwenda mahakamani kufungua mirathi tulipewa muongozo kuwa Mali zote walizochuma wazazi wetu ndani ya ndoa kisheria ni Mali ya wanandoa wote pamoja na watoto wao.
Hivyo endapo atafariki mzazi mmoja Basi Mali yote itabaki kwa watoto na mzazi aliyebaki.Ila kama wanandoa hawakubahatika kupata watoto Basi endapo mmoja wapo atafariki Basi Mali inagawanywa nusu kwa nusu ambapo nusu inakwenda kwa ndugu wa marehemu aliyefariki.
 
Wajuzi wa sheri.a naomba mnisaidie kuhusu yafuatayo yanayohusu mirathi haswa kwa ndoa za kikristo za mme mmoja mke mmoja:

1) Je mali mlizochuma ndani ya ndoa umiliki wake ukoje? mfano tuna nyumba tatu na zote zimeandikwa jina la baba je mama hana umiliki katika mali hizo na je kama baadhi ya magari yameandikwa jina la mama je baba hana umiliki katika magari hayo?

2) Je kama mmoja wa wanandoa anataka kuandika mirathi atarithisha asilimia zake tu za umiliki wa mali au atarithisha mali yote? mfano tunamiliki nyumba na mke wangu je mimi kama mme nina uwezo wa kumwandika mrithi bila kumshirikisha mwanandoa mwenzangu?

3) Je kuna uwezekano wa kuandikisha mali zenu kwa majina ya wawili kwa pamoja ili kuonyesha kwambq mnamiliki kwa kushare?

Wataalam wa sheria na wenye uzoefu na hivi vitu naomba mnipe majibu ya maswali haya na nina uhakika wengi watapata elimu katika hili

cc Mshana Jr ,
Kama ikitokea ndoa ya kikristo ikavunjika kinachofuata ni taratibu za kisheria kugawana mali nusu kwa nusu.... I mean mali mlizochuma pamoja na zenye usajiri wa majina yenu wote wawili ama mmojawapo (kwa uthibitisho wa mmoja kuhusika nayo)
Zaidi ni kwamba kisheria inaruhusiwa kuandika majina ya watoto wenu kama warithi..... Vingine nje ya hapo unaweza kutoa kwa upendo sheria haikubani....

NB: mali zinazotambulika kisheria kuwa ni zenyu ni zile zenye nyaraka zenye majina yenu tuu
 
Uislam raha sana.

Yote hayo yapo ndani ya Qur'an na hakuna longo longo.

Jisalimisheni kwa muumba wenu muondokane na makandokando hayo ya ulimwengu.
 
Hata mimi nashangaa vitu muhimu kama hivi watu hawavijali kabisa
Yaani hapa ianzishwe mada ihusuyo mambo ya "tigo" utaona thread inavyokimbia. Sijui tumerogwa na nani sisi waTZ. Yaani mambo ya kipuuzi na yanoyadhalilisha utu ndio yanayoshabikiwa na hasa vijana wa sasa.
 
Kama ikitokea ndoa ya kikristo ikavunjika kinachofuata ni taratibu za kisheria kugawana mali nusu kwa nusu.... I mean mali mlizochuma pamoja na zenye usajiri wa majina yenu wote wawili ama mmojawapo (kwa uthibitisho wa mmoja kuhusika nayo)
Zaidi ni kwamba kisheria inaruhusiwa kuandika majina ya watoto wenu kama warithi..... Vingine nje ya hapo unaweza kutoa kwa upendo sheria haikubani....

NB: mali zinazotambulika kisheria kuwa ni zenyu ni zile zenye nyaraka zenye majina yenu tuu
Je kama unataka kumrithisha mtu baki let say Rafiki yako inabidi umrithishe kwenye asilimia zako za umiliki?

Asante kwa ufafanuzi
 
Yaani hapa ianzishwe mada ihusuyo mambo ya "tigo" utaona thread inavyokimbia. Sijui tumerogwa na nani sisi waTZ. Yaani mambo ya kipuuzi na yanoyadhalilisha utu ndio yanayoshabikiwa na hasa vijana wa sasa.
Ndio nchi ilipofikia hapo kiongozi
 
Mimi ni bush lawyer;ila katika familia yangu Kuna Mali alizochuma Mama pekee na alizochuma mzee.Lakini baada ya mzee kufariki tulikwenda mahakamani kufungua mirathi tulipewa muongozo kuwa Mali zote walizochuma wazazi wetu ndani ya ndoa kisheria ni Mali ya wanandoa wote pamoja na watoto wao.
Hivyo endapo atafariki mzazi mmoja Basi Mali yote itabaki kwa watoto na mzazi aliyebaki.Ila kama wanandoa hawakubahatika kupata watoto Basi endapo mmoja wapo atafariki Basi Mali inagawanywa nusu kwa nusu ambapo nusu inakwenda kwa ndugu wa marehemu aliyefariki.
Okay nashukuru kwa ufafanuzi mzuri na je mmoja wa wazazi akifariki inatakiwa mali zigawanywe kwa watoto wake kwa mujibu wa share yake yaani 50% (yake)? mfano ameacha mashamba hekari 100 na yapo say matano
 
Jinsi wana'sheria' walivyochuna hapa unaweza fikiri JF hawamo. Sasa subiri polisi watawanye maandamano ya saccos,kila mtu atajifanya lawyer..
 
Okay nashukuru kwa ufafanuzi mzuri na je mmoja wa wazazi akifariki inatakiwa mali zigawanywe kwa watoto wake kwa mujibu wa share yake yaani 50% (yake)? mfano ameacha mashamba hekari 100 na yapo say matano
Mali huwa inagawanywa kwa asilimia baada ya kupatikana thamani ya Mali husika.Labda kwa ushauri naomba ingia Google tafuta Sheria ya mirathi Tanzania utapata maelezo vizuri ikiwa ni pamoja na mgawanyo wa Mali za marehemu unavyofanyika.
Kanuni ya kisheria inaelekeza kuwa mzazi aliyebaki anapewa 1/3 na watoto 2/3 ya thamani ya mali,hii ni kwa wakristo.Maana Sheria imegawanyika katika uislamu,ukristo,wahindi au wa-Asia na watu walioishi au kufungua ndoa kimila(mila za makabila husika)
 
Back
Top Bottom