Miradi ya World Bank (Benki ya Dunia) wanatuibia Watanzania!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,327
24,208
Miradi ya World Bank hapa nchini ni mingi, lakini ina walakini.

Miradi hii inawekewa masharti ambayo serikali huwa inayakubali bila kupitia vipengele vya utekelezaji miradi yenyewe.

Hi ina maana Wizara yetu ya Fedha inaingia hii miradi kichwa kichwa bila kupitia vipengele vya masharti.
Miaka karibia minne iliyopita, wadau wa ujenzi tulishuhudia tenda za aina mbili zikitangazwa.

UHURU STREET: Tenda ya kurehabilitate barabara hii maarufu yenye magari mengi sana. Aliyeshinda ni mkandarasi mzalendo na aliifanya kazi kwa bidii na mpaka leo(2023) iko katika hali nzuri. Tenda ilitangazwa na kusimamiwa na TANROADS na ilijegwa na mkandarasi mzalendo.

LINDI STREET: Tenda ya kurehabilitate hii barabara vile vile . Barabara ina congestion kubwa na haichukui magari makubwa. Barabara ilijengwa kwa kiwango cha lami, lakini leo 2023 barabara hii ni mbovu na ina mashimo maeneo mengi.

Tenda ilitangazwa kuwa mfadhili ni World Bank, msharti ya Tenda ati mpaka uwe na mzunguko(turnover ya mamilioni ya dola, na uwe umefanya kazi za mamilioni ya dola kwa mfululizo wa miaka minne au mitano.
Kazi ilifanywa na kampuni ya Kichina. Masharti yaliyowekwa ni ili kuwaondoa makandarasi wa kitanzania na vile vile ili kukimbiza fedha nje. Mradi huu ni wa DMDP chini ya Halmashauri ya Wilaya Ilala.

Tumezoea kuwa wenzetu walio maofisini na vuongozi na watendaji serikalini HAWASOMI MASHARTI ya mikopo ya World Bank. Wananchi tutaishia klipia mikopo ya miradi iliyofanywa hovyo hovyo tu na huku fedha zimeliwa na wajanja.

Tunaibiwa na World Bank hhivihivi tunatazama na kuchekelea.
 
Hii ni tetesi au...? Anyway, ripoti ya SIAGI imekosewa ~ Gerson Msigwa..
 
Hii ni tetesi au...? Anyway, ripoti ya SIAGI imekosewa ~ Gerson Msigwa..
Hii kitu ipo, nenda leo kaangalie hali ya hizo barabara mbili.
Moja imejengwa na mzalendo na nyingine imefadhiliwa na World Bank kwa kuhujumiwa kwa kuwashirikisha DMDP na Halmashauri ya Ilala.
 
Back
Top Bottom