Ole
JF-Expert Member
- Dec 16, 2006
- 2,157
- 980
Umeweka maneno mengi huku ukikwepa hoja yangu ya msingi, nimesema kama hii miradi ni ya pesa za ndani kwanini deni la taifa limepaa kiasi hicho? Suala la kukopa hakuna mwenye tatizo nalo maana huo ndio uhalisia. Halafu hizo data zinazotolewa na mawaziri sio za kuziamini sana, kwa sababu serikali hii inapika sana data ili kuhadaa umma kuwa mambo ni mazuri. Uchumi kukua kwa asilimia 7 nako ni utata mtupu, nakumbuka world Bank walitaka kuweka taarifa ya ukuaji wa uchumi ikawa ni mvutano wa hali ya juu. Hayo yote ni udhibitisho kuna utata mkubwa.
Mkuu Data za WB na IMF zinasema hivyo uchumi kwa miaka kumi iliyopita ndiyo hiyo plus minus 7% sasa weka za kwako tulinganishe uchumi unakua kwa asilimia ngapi? SGR phase I Dar Morogoro ni pesa za ndani hakuna aliyetukopesha. Kama una uhakika nani katukopesha weka hapa. Barabara njia nane kutoka Dar to Chalinze pesa za ndani etc. Data zipo BOT kama una ushahidi data zinapikwa weka hapa tujadili nani kapika na Je, kama amepika ameivisha kama pilau? Hakuna mradi wowote ambao ni ''white elephant? kama upo weka hapa, utaje maana tunazunguka mbuyu tu.
As far as I know, Wilayani kote Tanzania hivi sasa kuna Hospitali ya uhakika na bado zingine zinajengwa. Umeme kila kijiji kitapata umeme katika Afrika we are the leaders, maji safi kila mahali awamu hii ya 5 inaboresha achilia mbali miundo mbinu ya barabara etc. nafahamu tulikotoka hakukuwa na Serikali iliyokuwa inakiri nini inafanya lakini awamu hii mambo yako wazi. nawashauri doubting Thomas's wafungue macho na wanuse kahawa. Get out and smell the coffee.