Wanandugu.
Serikali ya awamu ya 5 imejipambanua kama ya wanyonge na imekuja na miradi lukuki inayotafuna mabilioni ya pesa za walalahoi, lakini miradi hii haina na wala haionyeshi dalili ya kuwa na tija yoyote huko mbeleni. miaka mitano hiyo inakatika tunapigwa porojo lakini mabilioni yanateketea.
Daraja la Mfugale
Huu ni mradi wa hovyo niliowahi kuuona na unareflect hisia kwamba utawala huu umejaa ubinafsi.
Daraja limejengwa kimkakati kuwapa upendeleo wanasiasa wanaowahi ndege airport.
Wanyonge wanaotoka na kwenda Tandika na maeneo mengine ya Temeke inawachukua wastani wa dakika 45 kuvuka Tazara, ni kero kuliko ilivyokuwa kabla halijajengwa.
Rais ajae alibomoe ndani ya siku 100 lijengwe upya watu wote walifaidi.
SGR
Huu mradi miaka minne sasa inaenda mitano hakuna cha maana zaidi ya kuona minguzo na minondo tu inasimikwa kila siku.
Nguzo zenyewe zinaonekana kujengwa sehemu zinazopitwa na watu wengi ionekane kuna kitu kinajengwa kumbe ni uzugaji.
Ndege
Kila nikilitizama anga naona ndege za biashara ni zilezile tu: SwisAir, Turkish, Emirates.
Hizi za Rubondo island mbona hatuzioni zinabeba nini kwenda wapi?
Dar es salaam
Huu ni mji lakini ni mradi tosha. Toto pendwa hajatatua hata kero moja; foleni, maji, mafuriko na hata usafi siku za jumamosi umemshinda.
Miaka mitano inakatika bado miradi inayowapa unafuu watanzania inabaki kuwa ile ile iliyobuniwa awamu zilizopita; daraja la Kigamboni, mwendokasi, shule za kata, barabara za lami kila kona, treni za Mwakyembe, watu wengi wameajiriwa sekta binafsi awamu zilizopita.
Sasa huu utawala kuna mradi gani wa maana umefanya ukafanikisha? Muda unaenda miaka mitano hiyo inakatika jamani.